USHAIRI MASWALI NA MAJIBU
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswali yafuatayoNyoosha mkono, uviringe ngumi, unyanyuwe kwa hasira. Nyoosha mkono, sema hunitumi, ila haki ujira. Nyoosha mkono, alama ya kukataa. Alama ya nguvu Nyoosha mkono, na macho makali, uwaonyeshe kukerwa Nyoosha mkono , wataka halali , kwamba hutaki kuporwa Nyoosha mkono, alama ya kukataa Alama ya nguvu. Nyoosha mkono, umekula njama, uyakatae madhila Nyoosha mkono, nyanyua kwa hima, watambue hukulala Nyoosha mkono, alama ya kukataa Alama ya nguvu. Nyoosha mkono, jiunge umoja, na wateswaji wenzako Nyoosha mkono, mwonyeshe miuja, yaondoke masumbuko Nyoosha mkono, alama ya kukataa Alama ya nguvu. Nyoosha mkono, ivume sauti, inayojaa kitisho Nyoosha mkono, mumejizatiti kwa mengi maamrisho Nyoosha mkono,alama ya kukataa Alama ya nguvu. Nyoosha mkono, mumeshikamana, huo ukuta wa chuma Nyoosha mkono, kitisho hakuna , wao watarudi nyuma Nyoosha mkono, alama ya kukataa Alama ya nguvu. Maswali a) Bainisha bahari tatu zinazojitokeza katika shairi.(alama 3) b) Andika ujumbe mkuu unaojitokeza katika shairi hili.(alama 4) c) Andika ubeti wa pili kwa lugha ya nathari. (alama 4) d) Onyesha tamathali mbili za lugha zilizotumiwa. (alama 2) e) Bainisha kwa njia tatu ni vipi mtunzi amefanikiwa kutumia uhuru wa kishairi .(alama 3) f) Tambua toni ya shairi hili (alama 1) g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumiwa katika shairi hili. (alama 2) i) Madhila ii) Jizatiti MAJIBU
a) Ukawafi – Mishororo ya kwanza mitatu ina vipande vitatu Msuko- Kibwagigo ni kifupi Tarbia – Mishororo minne kila ubeti Ukaraguni – Vina vinavyoftofautiana Kikwamba kianzio nyoosha mkono b) Msimamo dhabiti katika utetezi wa haki, kataa kudhulimiwa na uungane na wenzako, lazima uwe na usajiri. 2x2 =4 c) Inuka kwa ujasiri kama ishara ya kutoridhika kwa sababu unadai haki yako kwa njia halali. - Simama imara na ukatae kudhulumiwa na utashinda. 4x1 alama 4 d) Taswira – nyooosha mkono -Misemo - Kula njama- - Uhuishi/ tashihisi – Sauti inayojaa kitisho. Inksari jiunge – ujiunge e) Lahaja – Mangi,- Kuboronga- yaondoke masumbuko, masumboko yaondoke f) Toni ya – kutoridhika/kulalamika kuhamasisha/kuzindua. (alama 2) g) i) Mateso, taabu ii) JIkaze/ Jikakamue/Jitolee/Kujibiidisha. 2x1= alama 2
0 Comments
Leave a Reply. |
AuthorAtika School Team Archives
June 2024
Categories
All
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|