Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
Hakikisha kuwa insha yako ina mpangilio mzuri na mtiririko unaofuata hoja kuu.Kuandika insha ni mchakato wa kutumia maneno na sentensi kuwasilisha wazo, mtazamo, au maoni juu ya suala fulani. Hapa kuna hatua muhimu za kuandika insha:
0 Comments
Majibu
SWALI LA 1. -Mwanafunzi aandike insha yenye kuhusu mazungumzo au majibizano kati ya wahusika hawa watatu -Insha ifuate mtindo wa mchezo wa kuiguza - Azingatie kisa cha utovu wa nidhamu kama vile kupigana na mwanafunzi mwenzake, kuchelewa, kutovaa sare za shule n.k - Mwanafunzi atumie maneno mia nne (400). Asiyefikia maneno mia nne aondolewe maki 2 yaani 2u - Asipozingatia sura aondilewe maki 4 yaani 4s. SWALI LA 2
Faida ya kuelimisha motto wa kike
Maana ya methali SWALI LA 4 -Mwanafunzi atunge kisa ambacho kitaonyesha kuwa anajuta baada ya kutozingatia mawaidha -aliyopewa hapo awali -Mwanafunzi asiyemalizia kwa maneno haya awekwe katika kiwango cha D (alama3) -Akiongeza au kupunguza maneno matano aondolewe alama 2 yaan 2M MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)a) Eleza matumizi ya kiambishi ‘ka’ katika sentensi hizi ( alama 3) (i) Juma alikuja akachukua kitabu akaondoka ……………………………………………………………… (ii) Mti ulikatika ukaanguka ……………………………………………………………… (iii) “Nyanya anashona nguo”.Hamisi akasema ………………………………………………………………………… b) Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya jedwali (alama 4) Watoto wale wanafanya kazi lakini wazazi wao wanazungumza nyumbani. ……………………………………………………………………………………… c) Unda nomino kutokana na vitenzi hivi ( alama 2) (i) Onea …………………………………………………………………………… (ii) Umia …………………………………………………………………………………… d) Akifisha sentensi ifuatayo (alama 2) Tulifika tukaagana na mjomba hamisi aishiye mombasa …………………………………………………………………………………………… e) Kwa kutoa mifano mwafaka, eleza tofauti baina ya dhana zifuatazo (alama 4) Sauti ghuna na sauti sighuna ……………………………………………………………………………… f) Onyesha kiima, yambwa, na yambiwa, katika sentensi hii (alama 3) Mwanafunzi alimfutia mwalimu ubao ………………………………………………………………………… g) Andika sentensi hii kwa usemi wa taarifa (alama 2) “Lo! Kube wazuri hawajazaliwa,” Omari alisema baada ya kumwona kisura huyo. ……………………………………………………………………… h) Tunga sentensi moja moja kudhihirisha matumizi ya (alama 2) i. Posa ……………………………………………………… ii. Poza ……………………………………………………… i) Andika sentensi zifuatazo katika hali zilizo kwenye mabano (alama 4) i. Kijikombe chake kilivunjika baada ya kuangukia kijiwe (ukubwa) ………………………………………………………………………… ii. Mtu yule haachi kuandamana na mbwa wake aliyedhoofika kisiha (udogo) ………………………………………………………… j) Eleza maana mbili zinazotokana na sentensi ifuatayo (alama 4) Mtoto alitimua mbio, kuona nyoka …………………………………………………………………………… k) Andika sentensi ifuatayo katika kauli ya kutendesha (alama 2) Nguo zote zimekaushwa na jua …………………………………………………………………………… l) Tunga sentensi kudhibitisha mwingiliano wa maneno yafuatayo (alama 2) Nomino kuwa kivumishi …………………………………………………………………………………… m) Andika kwa wingi (alama 2) Kuwepo kwa mshauri wake kulimfurahisha waziri ……………………………………………………………………………… n) Geuza sentensi ifuatayo katika hali ya mazoea huku ukiondoa -amba (alama 2) Mtoto ambaye alikula ndiye ambaye alilia ……………………………………………………… o) Kamilisha methali ifuatayo (alama 1) Asiye na nadhari… ……………………………………………………… p) Eleza maana ya msemo huu (alama 1) Kwenda mbago… …………………………………………………………… MWONGOZO
a) i) Mfululizo wa vitendo wakati uliopita
ii) Hali ya kutendeka / kuwezekana kwa jambo iii) Katika usemi halisi (Alama 3) c) i) Maonevu, kuonea (kitenzi jina) ii) Umio, maumivu (Alama 4) d) Tulifika, tukaagana na mjomba Hamisi aishiye Mombasa. (Alama 2) e) i) Sauti ghuna zinapotamkwa husababisha kutikisika kwa nyuzi za glota km /b/, /g/, /w/. ii) Sauti si ghuna zinapotamkwa, nyuzi za glota hazitisiki kg /ch/, /sh/, /h/, /l/, /n/. (Alama 4) f) Mwanafunzi – Kiima Ubao – Yambwa Mwalimu – Yambiwa (Alama 3) g) Omari alishangaa baada ya kuona kisura yule kuwa wazuri hawakuwa wamezaliwa Baada ya kumwona kisura yule, Omari alishangaa kuwa wazuri hawakuwa wamezaliwa (Alama 2) h) Posa – Maombi ya kuoa Poza – Tuliza / poesha (Alama 2) i) i) Kombe lake lilivunjika baada ya kuangukia jijiwe (Alama 2) ii) Kijitu kile hakiachi kuandamana na kijibwa chake kilichodhoofika kisiha (Alama 2) j) i) Alikimbia kwenda kuona nyoka ii) Alikimbia alipoona nyoka (Alama 4) k) Jua limekausha nguo zote (Alama 2) l) Nomino kuwa kivumishi Kijana mkulima alituzwa (Alama 2) m) Kuwepo kwa washauri wao kuliwafurahisha mawaziri (Alama 2) n) Mtoto alaye ndiye aliaye ( Alama 2) o) Asiye nadhari siandamane naye (Alama 1) p) Kuenda kandokando (Alama 1) UFUPISHO (Alama 15)Vipindi mbalimbali vya historia vimeshuhudia kuibuka kwa magonjwa ya ajabu. Magonjwa hayo yamewahangaisha watu na kuzishughulisha bongo za wanasayansi na madaktari katika kutafuta tiba. Magonjwa kama vile tauni, kifua kikuu, homa ya matumbo na ndui ni baadhi ya yale yaliyotisha sana nyakati fulani za historia ya binadamu. Magonjwa haya yaliwauwa maelfu ya watu na kuibua mifumo na taratibu za maisha ya watu. Hata hivyo , magonjwa hayo yaliweza kuchunguzwa na kutafutiwa tiba kabla ya kumaliza kabisa kizazi cha binadamu. Lakini hii ni baada ya kuwasukuma maelfu ya watu kaburini. Ulimwengu wa sasa unashuhudia janga jingine la maradhi sugu ya ukimwi. Neno ‘UKIMWI’ lilitolewa kutokana na athari za ugonjwa huo mwilini. Neno “UKIMWI” humaanisha ukosefu wa kinga mwilini, ambapo herufi za kwanza za maneno matatu ziliunganishwa pamoja na kuunda neno hilo. Ugonjwa huu ambao tayari umewaua mamilioni ya watu kote ulimwenguni unazidi kuenea kwa kasi, mfano wa moto katika kicheka. Kutokana na kasi yake ya kuua watu, ugonjwa wa UKIMWI umepewa majina kama vile “umeme” na pia “ugonjwa wa vijana”. Watu wengi wanaoambukizwa virusi vya UKIMWI ni wale walio na miaka kati ya 15 hadi 49. Kundi hili kwa kweli ndilo linalohesabiwa kuwa na nguvu za kutunza jamii kwa njia nyingi. Iwapo wengi katika kundi hili watakumbwa na maradhi haya, watasalia wakongwe na watoto wachanga wasioweza kujimudu. Nchini Kenya, UKIMWI uligunduliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka wa 1984. Kufikia mwezi wa Juni 1996, inakisiwa kuwa ugonjwa huu ulikuwa umewaua watu wapatao 65,647 nchini. Hivi sasa, inasemekana kuwa takribani watu zaidi ya 500 hufa kila siku nchini Kenya kutokana na janga hili. Aidha, imedhibitishwa kwamba takriban watu milioni mbili unusu tayari watapoteza maisha yao kutokana na kuaambukizwa virusi vya ugonjwa huu humu nchini. Maradhi haya sasa yamekuwa janga la kitaifa. Kutokana na kuongezeka kwa visa vya UKIMWI, hospitali na zahanati nyingi kote nchini zinashindwa kukidhi mahitaji ya wagonjwa. Kwa hivyo, makundi ya kujitolea na mashirika mbalimbali yameundwa ili kuwahudumia wagonjwa wa UKIMWI. Baadhi ya makundi hayo hutoa tiba ya kisaikolojia pamoja na kuwapa ushauri wa hima ya kuishi, badala ya kukata tamaa. Wagonjwa wengi pia huishia kutibiwa nyumbani kwao. Ugonjwa huu umeathiri jamii kwa njia nyingi. Hali ya maisha na woga, ukosefu wa matumaini, ongezeko la mayatima na kuzorota kwa uchumi kutokana na kutoweka kwa kizazi chenye nguvu za kutoa huduma kwa jamii, na baadhi ya athari za maradhi haya. Lakini jambo la kuzingatia ni hili, tujifunze kutokana na historia.Tuwe na matumaini kwamba siku moja, tiba ya ugonjwa huu itapatikana. Hii ni kwa sababu tumethibitishiwa haya kutoka katika historia yetu wenyewe. Ikiwa magonjwa yaliyosababisha vifo vya wengi kutokana na ukosefu wa tiba yalitokomezwa kupitia juhudi za kimatibabu, sembuse huu ugonjwa tulio nao sasa? Huku tukijikinga kutokana na maradhi haya, tusife moyo bali tuwe na matumaini kwani subira hufuta heri. a) Kwa kutumia maneno yako mwenyewe na bila kupoteza maana, fupisha aya nne za mwanzo (maneno 90 - 100) (alama 3 kwa mtiririko) (alama 12 ) Nakala chafu/maadalizi ……………………………………… Jibu ……………………………………………………………… b) Eleza mambo yanayoleta matumaini kwa wagonjwa wa ukimwi kulingana na aya tatu za mwisho (maneno 40- 45) (alama 1 kwa mtiririko) Nakala chafu …………………………………………………… Nakala Safi ………………………………………………………………… MWONGOZO
UFUPISHO a) i) Vipindi mbalimbali vya historia vimeshuhudia kuibuka kwa magonjwa ya ajabu- tauni, kifua kikuu, homa ya matumbo n.k. ii) Magonjwa haya yamewahangaisha watu na kuzishughulisha bongo za wanasayansi na madaktari katika kutafuta tiba. iii) Magonjwa haya yaliwaua maelfu ya watu na kutibua mifumo na taratibu za maisha ya watu / yaliwaua watu wengi. iv) Magonjwa hayo yaliweza kuchunguzwa na kutafutiwa tiba. v) Ulimwengu wa sasa unashuhudia janga jingine la maradhi sugu ya ukimwi. vi) Ukimwi unazidi kuenea kwa kasi. Umewaua mamilioni ya watu kote ulimwenguni. vii) Ukimwi unazidi kuenea kwa kasi ulimwengu (lazima wazo la kazi litokee). viii) Wengi wa walioambukizwa ni kati ya miaka 15 – 49 ix) Kundi hili lina nguvu / linatunza jamii / wanaosalia ni watoto na wakongwe wanaoachwa. x) Ukimwi uligunduliwa Kenya mwaka wa 1984 (lazima ataje Kenya). xi) Watu zaidi ya 500 hufa kila siku xii) Ukimwi sasa ni janga la kitaifa. b i) Mashirika na makundi ya kujitolea kuwahudumia wagonjwa ii) Makundi hutoa tiba ya kisaikolojia na kuwapa ushauri na hima ya kuishi badala ya kukata tamaa. iii) Wengi hutibiwa nyumbani kwao. iv) Matumaini ya tiba kutokea. Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yoteMgomo uliingia siku ya tano. Asubuhi hii ilikuwa mbaya. Watu mbalimbali walikwisha kamatwa mjini na shamba, wakiwemo wote waliohudhuria kikao maalumu kibandani mwa Fumu. Siku ya pili ya mgomo, Makame aliuawa upenuni pa kibanda chake.Alipatikana amechomwa visu vitano vya mbavu. Mauaji ya kikatili lakini hayakuwa ya siri. Boga, yule kijana aliyehudhuria kikao cha pamoja na Fumu, ambaye toka mwanzo hadi mwisho wa kikao hakusema lolote, saa sita za usiku, aliingia kibandani na kumchopeka Makane visu mbele ya mkewe na wanawe, kisha aliikokota maiti na kuitupa upenuni. Asubuhi, Boga alikuwa mtu wa kwanza katika mkumbo mzima. Yeye alikamatwa kwa uuaji, makosa makubwa zaidi kuliko wenzake. Kukamatwa kwa watu hakukusaidia kitu - mgomo uliendelea. Kule shamba, vilio vya wanawake walioachwa pweke vilisikika. ‘Maskini mume wangu ….maskini, bora, bora ungaliwapeleka hao ng’ombe wakapigwa sindano; kufa kwa ng’ombe si kufa kwa nafsi yako,’ alilia bibi mmoja. ‘Ee, kufa kwa wengi arusi ndugu yangu we. Mimi nimelia we, hata macho yamenivimba kwa mume wangu; ati kakataa kupeleka mazao mjini na kuwajibu askari ufidhuli, lakini halafu nimeona haina maana kulia. Bora tufunge vibwebwe na sisi tuwasaidie kucheza ngoma - wafugaji mia wamekamatwa, wakulima mia mbili na hamsini, na bado wanaendelea kukamata, mji umebaki na wanawake tu; lakini watu wenyewe wana vioja, wanapochukuliwa utawaona wanacheka, sisi tulie nini?’ Mjini kulikuwa na vilio vyake. ‘Mwanangu wamemchukua , wanasema watamfunga au watamwua, kafanyaje? Daima kawatumikia , kapoteza nguvu zake juu yao na sasa…’Alimnung’unikia bibi mmoja. ‘Nini bibi we, wachukuzi na makuli watapata haki zao, na wale wanaozurura iko siku wataajiriwa na watakuta mambo mazuri, na wafanyikazi viwandani watachoka kufukuzwa ovyo ; hivyo ndivyo alivyonambia mwanangu alipokuwa akitoka, pingu mikononi. Nililia bibi, uchungu wa mwana unaujua bibi yangu, lakini baadaye nilipofikiri, nikachanganyisha na yale aliyokuwa akaniambia Ali mwanangu, kila siku; niliuhisi uzito wa maneno yake, nikafuta chozi babu.’ Wasaliti walikuwepo, lakini nafasi ya kusaliti haikupatikana. Kwenye lango la bandarini makuli na wachukuzi walisimama imara na marungu na mapanga tayari kuwang’ariba wahaini wowote. Ng’ambo, vikundi vilitawanyika na kufanya kazi; Wengine walitembea mipini mikononi, tayari kumtia adabu yeyote aliyetokwa na imani ya mgomo. Kikundi kingine kiliwekwa sokoni. Hakuna kitu kilichoingia wala kilichotoka. Magari hayakuwa na safari za shamba wala mjini. Askari walitembea ovyo na kumkamata waliyetaka kumkamata, lakini hakukutokea ghasia wala kupigwa mtu. Mgomo uliendelea, ukimuathiri kila mtu, lakini wale waliodai haki zao hawakuvunja kani. ( Dunia Mti Mkavu-Saidi Ahmed Mohamed) MASWALI 1. Toa anwani mwafaka kwa makala haya. (alama 1) ………………………………………………………………… ……………… 2. Thibitisha kuwa asubuhi hiyo ilikuwa mbaya. ( alama 1) …………………………………………………………………… ………… 3. Mauaji ya Makame yalikuwa ya kikatili. Eleza. (alama 4) …………………………………… …………………… 4. ‘Kufa kwa wengi arusi’. Thibitisha ukweli wa methali hii kwa kurejelea taarifa uliyosoma.(alama 4) …………… ………………………………… … 5. Watu walikamatwa kwa nini? (alama 2) ………………………………………………………… 6. Kwa nini wasaliti hawakupata nafasi yao kusaliti ? (alama 2) ………………………………………………… 7. Eleza maana ya (alama 2) i) makuli …………………… ii) Ukimuathiri ………………………… majibu
MAJIBU
INSHA
MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA
MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA 1. Mtahiniwa azingatie yafuatayo; Mbinu za kupambana na ufisadi -Kuelimisha wananchi kuhusu madhara ya ufisadi kupitia kwa redio, magazeti, runinga n.k. -Kuwaadhibu wahusika – wapelekwe mahakamani na wafungwa jela. -Wananchi waadilike (wawe na maadili mema). -Viongozi wawajibike katika kazi zao. -Sheria za kupambana na ufisadi zibuniwe na kutekelezwa. -Kubuni nafasi zaidi za kazi -Kuimarisha elimu -Kuongeza mishahara kwa wafanyikazi -Tume zaidi za kukabiliana na ufisadi zibuniwe. SURA YA MAHOJIANO -Insha iwe na kichwa kinacholenga mada -Kuwe na mhoji na mhojiwa -Njia ya maswali na majibu -Njia ya kitamthilia ufuatiwe kwa mfano; Juma: Bakari: TAHADHARI -Atakayefululiza bila kufuata mtindo wa mahojiano aondolewe alama (4) sura baada ya kutuzwa. 2. i) Kilimo cha mboga ii) Upanzi wa miti iii) Utengenezaji wa matofali na kuyauza. iv) Ukarabati wa barabara v) Kushirikiana na polisi katika kutoa usalama kwa umma. 3. Maana ya methali Ikiwa umekwisha jitayarisha kufanya jambo, basi bora ulikabili / ulifanye na ulimalize. -Mtahiniwa aandike kisa kitakachothibitisha ukweli wa methali. -Aonyeshe mtu aliyeanza jambo licha ya vikwazo / matatizo, alijibidiisha kulikamilisha. 4. Sharti mtahiniwa aanze insha kwa maneno aliyopewa bila kubadilisha wala kuongeza. Insha ionyeshe harakati za kumtafuta baba mzazi Asimulie jinsi alivyotambua / alivyokutana na babake kwa mara ya kwanza. Hisia alizozipata kv. Furaha / chuki Iwapo mkutano huu ulifaulisha maisha yake ya usoni au la. Ugunduzi wake ulivyoathiri maisha yake TAZ: Kisa kisimuliwe kwa njia ya kuvutia na kusisimua. ISIMU JAMII4. ISIMU JAMII (i) Eleza maana ya lugha sanifu. (alama 1) (ii) Eleza maana ya lafudhi (alama 1) (iii) Jadili matatizo manne yanayokumba ukuaji wa lugha ya Kiswahili nchini Kenya. (alama 8) ISIMU JAMII majibu
4. ISIMU JAMII Lugha Sanifu (i) Ni ile lahoja iliyochanguliwa na kufanyiwa marekebisho ya kimatamushi, kisarufi, kimaana na kimaandishi ili iweze kutumika katika shughuli rasmi kwa mfano — kiunguja. (ii) Lafundi Matamshi ya mzungumzaji yatokanayo na kuathiriwa na lugha ya kwanza au lugha zilizo katika eneo anamoishi. Al -1 au Matamshi ya sauti za lugha yanayomtambulisha mtu au jamii ya lugha Fulani. (iii) Matatizo manne yanayokumba ukuali wa Iuha ya Kiswahili nchini Kenya. 1. Udhaifu na kutekelezwa kwa sera. 2. Matatizo katika mitaala 3. Matumizi mabaya ya lughaushindani wa lugha nyingine 4. Mielekeo hasi 5. Shule za kimataifa na za kibinafsi 6. Ukosefli wa vyombo rasmi vya kukuza Kiswahili 7. Utafiti 8. Msamiati na istilahi MATUMIZI YA LUGHA(a) Pigia mstari iliko shadda mara mbili kwenye neno hili ili kuleta maana zake mbili tofauti. Eleza maana hizo. (i) Ala …………………………..…… (ii) Ala (alama 2) ……………..…… (b) Unda kitenzi an nomino kutokana na nomino an kitenzi ulichopewa kwa kufuata mfano uliopewa. (c) Andika kinyume cha sentensi ifuatayo ukizingatia maneno yaliyopigiwa mstari. Zilizala ilipotokea wanafunzi walitulia na kuanza kucheka. (alama 1) ..……………………………………………………………………………… (d) Kamilisha jedwali kwa kauli ifaayo. (alama 4 1/2) (e) Tambua na uainishe vitenzi katika sentensi ifuatayo. (alama 2) Kuzaa si kazi, kazi ni kuvyeleza. ......................................................... (f) Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia vielelezo vya matawi. (alama 4) Wengi wataitwa lakini wachache watateuliwa .................................................................. (g) Onyesha hali katika sentensi zifuatazo (alama 1) 1. Mwizi akamatwa mtaani Kondele. ............................................................... 2. Nyumba hufagiliwa asubuhi. ................................................................... (h) Kanusha sentensi ifuatayo. (alama 1) Nimemwona Fuchingo na paka wake. ........................................................................ (i) Tunga sentensi yenye kuhusishi cha ‘A’-Unganifu katika ngeli ya I-I, wingi. (alama 1) ............................................................... (j) Andika katika wingi (alama 1) Zigo la kuliwa halilemei .................................................................... (k) Tambua na ueleze aina ya yambwa katika sentensi zifuatazo (i) Mtoto alipigwa vibaya sana na mamake (alama 2) ........................................................................... (ii) Osama alipigwa risasi na wanajeshi (alama 2) ............................................................ (l) Tumia vitate vifuatavyo kutungia sentensi moja moja ili kutofautisha maana zake. 1. Pango (alama 1) .................................................. 2. Bango (alama 1) ............................................................... (m) Onyesha silabi funge kwenye maneno yafuatayo 1. Baiskeli (alama 1) ............................................................................ 2. Muhtasari (alama 1) .............................................. (n) Taja na utofautishe vikwamizo vya meno. (alama 2) .......................................................................................... (o) Geuza katika usemi wa taarifa “Sitatoka hapa leo bila kunilipa. Uliniambiajana nije leo utanilipa. Mbona tena unataka nije kesho?” Mwajiriwa aliteta. (alama 4) ............................................... (p) Onyesha kishazi huru na tegemezi katika sentensi ifuatayo. (alama 2) Mateka wote waliokamatwa leo watafikishwa mahakamani. ................................................................... (q) Tunga sentensi sahihi ukitumia viunganishi vifuatavyo ipasavyo. (alama 2) (i) Lau ............................................ (ii) Waama ................................................. (r) Pambanua viambishi awali, mzizi na viambishi tamati katika kitenzi. (alama 2) Alituwiaje? ............................................ MAJIBU YA MATUMIZI YA LUGHA
3. MAJIBU YA MATUMIZI YA LUGHA
(a) (i) Ala I Ala I Ala - Tamko la mshangao (ii) Ala / Ala / Ala - Mfhko Wa kubeba ala (b) (i) Kuhukumu / hukumu (ii) Riziki (iii) Husudu / Kuhusudu (iv) Rithi / kurithi (c) Zilizala ilipotokea wanafunzi walibabaika na kuanza kulia. (d) (i) Wangapi? wepi / wapi? gani? (ii) Wangapi? wapi / wepi? gani? (iii) Ngapi? zipi? gani? (e) - Kuzaa - kitenzi jina - Si - t/kitenzi kishirikishi kipungufu - Kuvyeleza - kitenzi jina - Ni - kishirikishi kipundufu / t (g) (i) Hali ya - ka / wakati usiodhihirika / wowote. (ii) Hali ya - hu mazoea (h) Sijamwona Fuchingo wala paka wake. (i) Chumvi, sukari, mvua, chai, njia, asali (j) Mjizigo ya kuliwa hayalemei. (k) (i) Mtoto — Yambwa kitondo (ii) Osama — (a) Yambwa kitondo (b) Risasi - Yambwa ala (1) Pango - Tundu, shimo Bango - Maandishi ya kutangaza, tangazo linalobebwa na waandamanaji, tangazo la kampem (m) (i) Baiskeli - bais (ii) Mukhtasati - muh (n) v - ghuna f - sighuna (o) Mwajiriwa aliteta kuwalkwamba asingetoka hapo siku hiyo bila ya kulipwa kwa sababu aliambiwa siku iliyotangulia kuwa aende hapo siku hiyo alipwe I angelipwa. Alitaka kujua sababu ya kumtaka aende siku iliyofuata I keshoye. (p) Tegemezi - Mateka wote waliokamatwa leo Hutu - Watafikishwa mahakamani (q) (i) Kama - Neno lao sharti liwe mwanzoni mwa sentensi (ii) Kwa kweli (r) A — Kiima / mtendo / Nafsi ya 3 — umoja ii — wakati wakati uliopita njeo, tu — Yamwa / watendendewa Nafsi ya — wingi w — mzizi i— kauli kinyambulishi a — kiishio kimalizio je — kiulizi. Ukiwa mtoto unadhani ulimwengu ni kipande kimoja cha keki kilicho kitamu mithili ya asali.17/12/2023 Jibu makala yafuatayo kisha ujibu maswali.UFUPISHO Ukiwa mtoto unadhani ulimwengu ni kipande kimoja cha keki kilicho kitamu mithili ya asali. Hakuna dhiki, hakuna mateso, hakuna kuhuzunika kwa ama yoyote. Neno huzurn linasikika masikioni kama neno lisiloelekea kwenye uhalisia wowote. Kwa watoto duma imejaa raha, starehe na vcheko visivyoisha. Maisha ni ahadi njema, yenye matokeo ya kufurahisha na kustarehesha tu sio kudhikisha na kuhuzunisha. Huyu tunayemzungumzia hapa ni mtoto mdogo ambaye hajajua kubainisha kitendekacho mkono wake wa kushoto wala idle kinachofanyika hasa katika mkono wake wa kulia. Hata hivyo, jinsi mtoto anavyoendelea kukua na kufahamikiwa na mambo, vigambo na kadhia zinazoendelea katika mazingira yake, anabainikiwa na mengi machungu ambayo huleta huzuni, sb raha. Hebu tuanze na nyumbani kwao mtoto. Aghalabu, watoto wote hupendwa kwao nyumbani, iwapo wazazi wao ni watu wangwana na wana nafasi ya kulea watoto wao bila taabu. Hata hivyo watoto huchapwa pale wanapokuwa watundu, jambo ambalo huwahuzunisha sana, japo ni wajibu wa wazazi sababu, kama isemwavyo, meha mwana kulia hulia yeye. Pili, inajulikana wazi kwamba watoto wengi siku hizi huenda shule. Huko shule, wao hupendelea sana kucheza kuliko kusoma. Iii wasome kama inavyotakikana, m sharti waelekezwe barabara katika njia hiyo na walimu wao. Katika kuelekezwa huku, walimu wanaweza kulazimika kuwaacthibu, hasa wale watoto ambao huzembea na kutofanya kazi zao wanazopewa kufanya nyumbani kama kawaida ya mfumo wa shule ulivyo. Watoto wa ama hii wanapotiwa adabu raha hujitenga na buzuni huwatawala. Huzuni, hivyo basi, maonekana ya kuwa m uso wa pili katika maisha ya wanadamu, uso wa kwanza ukiwa raha. Na kwa hakika wanaohuzunika si watoto peke yao. Kila mtu duniani ni sharti, katika wakati mmoja au mwingine, azongwe na huzuni. Inajulikana wazi kwamba wanadamu wote hawapendi huzuni asilani na hakika kabisa, kila binadamu huchukia huzuni na kustahabu raha. Hata hivyo, raha humjia binadamu kwa nadra sana, ilhali huzuni humvamia wakati wowote, hata akiwa yumo katikati ya kustarehe. Si tu, inajulikana dhahiri kwamba hakuna mtu asiyewahi kuonja huzuni, japo wapo wengi kweli kweli wasiowahi kuonja raha maishani mwao. Zingatia mtoto anayezaliwa, halafu wazazi wake wanaaga dunia, pengine katika ajali, kabla mtoto mwenyewe hajaweza kujikimu. Mtoto huyu anaishi kutegemea jamaa za wazazi wake. Watu hawa wasipokuwa na nafasi wao wenyewe kimaisha pamoja na ukarimu unaohitajika basi mtoto anateseka na kuhuzunika sana katika maisha yake yote. Ama zingatia mtoto anayetupwa na mamake kijana, anayempata bila kupanga. Hata mtoto huyu akiokotwa na kulelewa na wahisani, maisha yake yatakuwa ya taabu, dhiki na huzuni. Au zingatia mtoto anayelelewa na mama wa kambo anayeondokea kuwa mwovu. Mtoto huyu atakayoijua ni huzuni tu. Ama zingatia mtoto ambaye babake ni mievi na analojua ni kurudi nyumbani usiku akiimba nyimbo za kilevi, kuita mkewe kwa sauti kubwa, kuitisha chakula na kufurahia kupiga watoto wote na mama yao ndipo apate usingizi mnono. Mtoto mwenye baba wa ama hiyo atakayoijua ni huzuni tu, si raha asilani. MASWALI (a) Ukitumia maneno yako mwenyewe na bila kupoteza maana, fupisha aya nne za mwanzo. (Maneno-100). (Alama 9) Nakala chafu ………………………………………………………………………………………………… Nakala safi ………………………………………………………………………………………………… (b) Ukizingatia aya ya mwisho eleza hali mbalimbali zinazowatia watoto buzuni. (Maneno 40-45) (Alama 4) Nakala chafu ………………………………………………………………………………………………… Nakala safi ………………………………………………………………………………………………… Majibu
Majibu (a) (i) Mtoto hudhani/hufikiri ulimwengu umejaa raha na hauna huzuni/hauna mateso/haudhikishi. (ii) Mtoto huyu ni yule mdogo ambaye hajajua kubainisha mambo. (iii) Anavyoendelea kukua, anafahamishwaanabainikiwa na mengi yaletayo huzuni. (iv) Nyumbani ingawa hupendwa, huadhibiwa wanapokuwa watundu na kuhuzunika. (v) Shuleni wanapozembea kazi, wanaadhibiwa na hili huwahuzunisha. (vi) Huzuni basi ni uso wa pili katika maisha ya binadamu, uso wa kwanza ukiwa raha. (vii) Kila mtu duniani huzongwa na huzuni / huhuzunika (viii) Raha humjia mwanadamu kwa nadra ilhali huzuni humuvamia wakati wowote. (ix) Wako watu wengi wasiowahi kuonja raha maishani mwao (Hoja 9-al-1 =9) (b) (i) Mtoto anapofiwa na wazazi (ii) Mtoto anayetupwa na mamake kijana baada ya kuzaliwa. (iii) Mtoto anayelelewa na mama wa kambo mwovu. (iv) Mtoto ambaye babake ni mlevi Hoja4-Al-1 —4 Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.UFAHAMU Wanasaikolojia wanabainisha kati ya sehemu mbili kuu katika akili ya binadamu; ung’amuzi na ung’amuzibwete. Ung’amuzi ni sehemu ya ubongo ambayo kimsingi hupanua na kudadavua yanayotendeka hususan mchana. Ung’amuzibwete ni kibinimethali chake; hufanya kazi wakati binadamu anapolemazwa na usingizi. Baadhi ya mambo anayoshuhudia binadamu mchana yanaingia kwenye ung’amuzibwete wake na kutokeza katika ndoto zake usiku. Kwa mujibu na mawazo ya Sigmund Freud, mwanasaikolojia wa jadi anayechukuliwa na wengi kama mwasisi wa taaluma ya saikolojia, mambo yanayopatikana katika ang’amuzibwete yana sifa hasi. Freud alidahuli kuwa binadamu huyaficha na kuyabania kwenye ang’amuzibwete mambo ambayo hawezi kuyasema kadamnasi. Alieleza kuwa matamanio yasiyokubalika, makatazo ya jamii, fikra na kauli zilizobaramishwa na miko ya kijamii hubanwa katika ang’amuzibwete. Shehena hiyo ndiyo inayochipuza kwa njia ya ishara za ndoto, mitelezo ya kauli, yaani maneno au kauli zinazotutoka bila wenyewe kukusudia, ishara na lugha ya kitamathalu katika uandishi wa kibunifu na kadhalika. Ung’amuzibwete una uwezo mkubwa wa kuathiri matendo ya bmadamu. Huu ndio msmgi unaowafanya wanasaikolojia wengi, ukiwemo Freud, kusema kuwa tajriba ya mtoto maweza kufichwa kwenye sehemu hiyo na hatimaye kuishia kutokeza katika utu uzima wake. Kwa kuwa tunapoingiliana na binadamu wenzetu kila siku tunayang’amua tuyafanyayo, ung’amuzi unaotuwezesha kutambua jema na ovu unatawala. Ung’amuzibwete unapotawala binadamu wenzetu watashindwa kutuelewa. Hii ndiyo hali anayokuwa nayo mwendawazimu. Ung’amuzibwete wake hutawala. Sisi tunaotawaliwa na ung’amuzi tunashindwa kumwelewa; naye bila shaka anashindwa kutuelewa. Carl Gustav Jung, aliyewahi kuwa mwanafiinzi wa Freud, aliupinga mwelekeo wa Freud na kuungalia ung’amuzibwete kamajaa la mawazo mabaya, matamanio, nia, fikira tuli na dhana ambazo ni hasi. Jung alizuka na dhana mbili muhimu: Ung’amuzibwete wa kibinafsi na ung’a,izibwete jumuishi. Alisema mambo, fikra na uzoefu wowote mbaya unaomuhusu mtu binafsi hupatikana katika ung’amuzibwete wa kibinafsi. Dhana ya ung’amuzibwete jumuishi aliitumia kuelezea sehemu ya akili ya binadamu ambayo inamfanya ayatende matendo fulani kama binadamu wenzake licha ya tofauti zao kiwakati na kijiografia. Kwa mfano, binadamu wengi wana sherehe za kuzaliwa mtoto, kuoa, ibada au mviga unaohusiana na kifo licha ya tofauti zao. Jung alisema kuwa kinachochochea hali hii ni urithi Fulani wa kila mwanadamu. Urithi huo unaopatikana katika ung’ amuzibwete una uwezo wa kuathiri ung’amuzi na matendo ya binadamu ya king’amuzi. Wanasaikolojia wanashikilia kuwa binadamu hawezi kukamilika bila kuzuhusisha sehemu zote mbili kwa sababu zinaathiriana. MASWALI(a) Kwa nini ung’amuzibwete unaelezwa kama kinyume cha ung’amuzi? (alama 2) .……………………………………………………………………………………………… (b) Eleza mtazamo wa Freud kuhusu ung’amuzibwete (alama 3) ……………………………………………………………………………………………….. (c) Kwa mujibu wa Freud yaliyomo kwenye ung’amuzibwete hudhihirika vipi? (alama 4) ……………………………………………………………………………………………….. (d) Eleza tofauti ya mawazo kati ya Sigmund Freud na Carl Gustav Jung. (alama 4) ……………………………………………………………………………………………….. (e) Taja hoja inayowafungamanisha Jung na Freud. (alama 2) .……………………………………………………………………………………………… Majibu
(a) Ung’amuzibwete hufanya kazi mtu akiwa amelala/usiku kinyume na ung’amuzi ambao hufanya kazi mtu akiwa macho/mchana. 1x2 = 2 (b) Mambo yanayopatikana katika ung’amuzi bwete (i) Yana sifa hasi / hubana sifa hasi (ii) Huficha mambo ambayo mwanadamu hawezi kuyasoma wazipeupembele ya kadamnasi (iii) Hubana matamanio yasiyokubalika na jamii (iv) Hubania kauli zilizoharamishwa na miiko ya jamii. 1x3= Hojayoyote mojaAl— 3 (c) (1) Kwa ishara za ndoto (ii) Kwa mitelezo ya kauli (iii) Kwa ishara (iv) Kwa matumizi ya lugha ya kitamathali katika uandishi 4x1= 4 AIa,na-4 (d) Freud anawaza kuwa ung’amuzibwete ni jai la mambo hasi ilhali Jung ana dhana mbili kuhusu ung’amuzibwete (i) Ile ya kibinafsi (ii) Ile ya jumuishi au Freud ana mtazamo wa dhana hasi katika ung’amuzibwete ilhali Jung anawaza dhana ya jumuishi. 2x2=4 Mwanafunzi aonyesha dhana zote mbili ya Freud na ya Jung (e) Ung’amuzibwete una uwezo wa kuathiri ung’amuzi na matendo ya binadamu ya king’amuzi. Al-2 Insha
Mwongozo huu unatumika sambamba na mwongozo wa kudumu wa Insha [102/1]
1. Andika hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kupambana na Ufisadi nchini kwa washika dau wote katika Kaunti ya Kakamega. -Insha ihusishe hoja zisizopungua sita kati ya hizi na nyingine zinazorejelea maswala yoyote ya ufisadi nchini: --Chanzo cha ufisadi k.m. umaskini, tamaa, kuiga wengine, kutaka kuhepa adhabu, n.k. --Kunakotokea ufisadi, k.m. ofisini, hospitali, shuleni, mahakamani, katika vyombo vya usafiri, n.k. --Athari za ufisadi k.m. ufujaji wa pesa, nchi/mashirika kutoendelea, n.k. --Adhabu kwa ufisadi k.m. kushikwa, kufungwa, kufutwa, kulazimishwa kulipia, n.k. --Hatua zinazochukuliwa na shirika lake kupambana na ufisadi. --Mapendekezo yake kwa umma kuhusu jinsi ya kupambana na ufisadi. SURA Ionyeshe kuwa ni hotuba kutokana na kianzio, kinachotambua au kuiamkua haadhira. Pia kiishio. Insha yenyewe iandikwe kwa mtiririko ikitumia nafsi ya kwanza. Adhabu ya kawaida ichukuliwe kwa insha isiyochukua sura inayostahili (-04s) 2. Eleza chanzo cha ongezeko la bei ya bidhaa nchini mwako, huku ukionyesha athari za ongezeko hili. CHANZO --Ufisadi --Tamaa --Shilingi ya Kenya kukosa nguvu dhidi ya Dola ya Marekani.
ATHARI
3. Aiszfuye mvua imemnyea. Ni methali. Insha iwe na kisa (au visa) kinachoonyesha ukweli wa methali. Methali ina maana kuwa anayelizungumzia jambo, kulieleza au kulisifu ana tajriba nab. Insha ionyeshe sifa itolewayo na pia alivyonyewa. 4. “Karne ya 21 imeleta ongezeko kubwa la vyombo tofauti vya habari nchini, pamoja na athari anuwai” Jadili kauli hii. ONGEZEKO Insha ithihirishe ukweli kwamba vyombo vya habari vimeongezeka kwa kutoa mifano ya magazeti, majarida, stesheni za redio, runinga, n.k. atakayejaribu kuipinga kauli hii atakuwa amepotoka. ATHARI Ni nzuri na mbaya • Habari zinapatikana kwa urahisi. • Hakuna usiri usiofaa wa serikali tena. • Kuna burudani tele. • Vinaelimisha. • Watu (hususan wale mashuhuri) wamekoseshwa siri katika maisha yao. • Vyombo vingine vinachochea makabila, n.k. • Kuna ongezeko la picha/habari za ngono. • Maadili yamezorota. • N.K. Insha ihusishe hoja zozote sita au zaidi katiya hizi na nyingine. ZIADA YA JUMLA Tumia mwongozo wa kudumu wa insha ili kutuza insha katika viwango kati ya A+ na D-. hoja katika maswali 1,3 na 4 itambulike kwa mkwaju (‘f) kushoto, pembezoni mwa aya iliyobeba hoja. ISIMU JAMII (Alama10)a) Eleza maana ya istilahi zifuatazo i) Lafudhi (alama 1) __________________________________________________________________________ ii) Pijini (alama 1) __________________________________________________________________________ iii) Lahaja (alama 1) __________________________________________________________________________ b) Eleza njia tatu za kupunguza tofauti za kilahaja (alama 3) __________________________________________________________________________ c) Fafanua sababu zozote zinazosababisha makosa katika matumizi ya lugha ya Kiswahili (alama 4) Mwongozo
a) i) Lafudhi – ni upekee unaojitokeza baina ya watumiaji mbalimbali wa lugha moja. ii) Pijini – ni lugha inayoibuka panapotokea mwingiliano wa watu wanaozungumza lugha tofauti kwa lengo la kurahisisha mawasiliano. iii) Lahaja ni tofauti katika matamshi, maumbo na matumizi ya maneno zitokanazo na tofauti katika maeneo mbalimbali kwa lugha yenye asili moja. b) i) Kusanifisha lugha ii) Kuimarisha njia za usafiri baina ya maeneo ambapo lugha inatumiwa km barabara iii) Kuwepo kwa mfumo mmoja wa elimu ambapo lugha moja inatumiwa iv) Maendeleo ya njia za kupashana habari km simu magazeti, redio n.k v) Kuweka utawala mmoja k.v. muungano wa Afrika Mashariki. c) Lugha ya kwanza Hali – uchovu / ugonjwa wa mzungumzaji Uwili lugha / uwingi lugha Kwa kukusudia km. waigizaji. Kutozingatia ngeli Kutoelewa lugha/msamiati Kutozingatia upatanisho wa ngeli Kutozingatia tahajia/hijai/maendelezo SARUFI NA MATUMIZI YA LUGHA (Alama40) a) Tofautisha sauti zifuatazo. (alama 2) /a/ /u/ __________________________________________________________________________ b) i) Ngeli ni nini? (alama 1) __________________________________________________________________________ ii) Maneno haya yamo katika ngeli gani? (alama 2) Tayo __________________________________________________________________________ Kipepeo __________________________________________________________________________ c) Akifisha sentensi hii kwa njia tatu tofauti kuleta dhana tatu tofauti. (alama 3) Babu alimchapa nyanya __________________________________________________________________________ d) Ainisha mofimu katika neno lifuatalo (alama 3) Sikumkaribisha __________________________________________________________________________ e) Andika katika usemi wa taarifa (alama 3) “Mtapata mwaliko wenu kesho,” alisema Salim __________________________________________________________________________ f) Andika kwa wastani (alama 2) Magoma hayo yatachezwa mawanjani __________________________________________________________________________ g) Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya mistari Wanafunzi wenye bidii hufuzu mtihani h) Tofautisha sentensi zifuatazo. (alama 2) i) Ningekuwa na pesa ningenunua simu nzuri ii) Ningalikuwa na pesa ningalinunua simu nzuri __________________________________________________________________________ i) Tunga sentensi ukitumia vihusishi vya: (alama 3) a) Kulinganisha __________________________________________________________________________ b) Sababu __________________________________________________________________________ c) Wakati __________________________________________________________________________ j) Kwa kutoa mifano katika sentensi onyesha matumizi mawili ya parandesi (alama 2) __________________________________________________________________________ k) Tambua kiima, shamirisho, chagizo na kiarifa katika sentensi ifuatayo (alama 4) Nyanya alimjengea mjukuu nyumba kwa matofali mwaka jana. __________________________________________________________________________ l) Eleza tofauti ya kimaana katika sentensi hizi (alama 2) i) Nisimamapo huchekwa ii) Ninaposimama huchekwa __________________________________________________________________________ m) Andika sentensi hii upya bila kubadilisha maana ukitumia ‘o’ rejeshi na kiambishi ngeli mwanafunzi alitumwa nyumbani juzi na hajapata karo hadi leo. __________________________________________________________________________ n) i) Eleza dhana ya kishazi tegemezi (alama1) __________________________________________________________________________ ii) Bainisha aina za vishazi (alama 2) Konde iliyopaliliwa ilituletea mazao mengi sana __________________________________________________________________________ o) Tunga sentensi kuonyesha maana mbili za neno chuma (alama 2) __________________________________________________________________________ Mwongozo
a) /a/ ni irabu ya kati (hutamkwa kwa kutumia sehemu ya kati ya ulimi) midomo hutandanzwa inapotamkwa. /u/ ni irabu ya nyuma (ulimi huinuliwa juu na kupindwa nyuma ya inapotamkwa. midomo kuviringwa inapotamkwa. b) i) Ngeli ni kundi la nomino za aina moja ii) Tayo – LI – YA Kipepeo – A – WA c) Babu alimchapa nyanya? (swali) Babu alimchapa nyanya! (mshangao) Babu alimchapa nyanya. (maelezo / taarifa) d) si – kiwakilishi cha ukanushaji ku – kiwakilishi cha wakati uliopita m – kiwakilisha cha mtendwa karib – mzizi ish – kiwakilishi cha kauli a – kiishio e) Salim alisema kwamba wangepata mwaliko wao siku iliyofuata au Salim alisema kuwa tungepata mwaliko wetu siku iliyofuata. f) Ngoma hizo zitachezwa uwanjani g) S – KN + KT KN – N + V + N N - Wanafunzi V – wenye N – bidii KT – T + N T – hufuzu N – mtihani h) i) Nge – huonyesha wakati ujao na kuwa kuna uwezekano ii) Ngali – huonyesha wakati uliopita na hakuna uwezekano / ni majuto i) a) Abunuwasi ni mjanja kama sungura Dhahabu ni ghali kuliko shaba b) Juma ametuzwa kwa uhodari wake c) Jogoo huwika kabla ya saa tisa usiku j) Jona (kijana mpole) anasafiri leo kwenda mjini? maelezo ya ziada Aziza (mhusika mkuu) aliomba talaka Mjomba: (akikohoa) habari? – tamthilia / mazungumzo Kufungia nambari (1) (2) (3) k) Nyanya – kiima Mjukuu – shamirisho kitondo Nyumba – shamirisho kipozi Chagizo – i) mwaka jana ii) kwa matofali Shamirisho ala – matofali Alimjengea – kiarifa l) i) Wakati wowote ii) Wakati maalumu m) Mwanafunzi aliyetumwa nyumbani juzi, hajapata karo hadi leo. n) Kishazi tegemezi – ni kundi la maneno lililo na kiima na kiarifa lakini haliwezi kujisimamia pekee kama sentensi. hutegemea kishazi huru ili kupata maana. o) Watoto hao wanachuma machungwa Nondo za madirisha hutengenezwa kwa chuma Mimi ninafanya kazi ili kuchuma pesa Soma makala haya kisha ujibu maswali yafuatayo HAKI ZA BINADAMU Binadamu wana mazoea ya kufikiria kuwa jinsi wafanyavyo, waongeavyo na wafikiriavyo kuhusu vitu ndivyo inavyopasa kuwa. Kama binandamu tunaamini njia yetu ndiyo sahihi, yenye mantiki na inayopasa kufuatwa na kila mtu. Msingi huu huu unakwenda kinyume na kutambua kila binadamu ana haki ya kufikiri, kusema au kuongea na kutenda mradi asikiuke haki ya mwenzake iliyo sawa na yake. Nguzo mojawapo inayogongomelea hoja hii ni Haki za Binadamu. Azimio kutangaza Haki Bia za Binadamu liliafikiwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 10 Desemba 1948. Baraza kuu hilo liliyasisitizia mataifa wanachama umuhimu wa kuyasambaza, kuenezea, na kusisitiza kusambazwa kwa azimio hilo katika shule na taasisi za kielimu. Msingi wa uhuru, haki na amani ulimwenguni ni kutambua binadamu wote wana haki sawa. Ingawa kimsingi jamii na mataifa yote ya ulimwengu yanapaswa kuthamini, kusambaza na kuhimiza umuhimu wa Haki za Binadamu zipo jamii ambazo hukiuka haki hizo. Matokeo ya ukiukaji huu yana athari hasi sana kama ilivyotokea nchini Rwanda na Bosnia. Herzegovina kulikotokea mauaji ya halaiki. Azimio la Haki za Binadamu linajumuisha vipengele kadha ambavyo ni mihimili mikuu ya Azimio lenyewe. Kipengele msingi kabisa kinasisitiza kuwa kila kiumbe anazaliwa huru na ana haki na hadhi sawa na kiumbe mwingine. Ukweli wa kauli hii ulikokotezwa na kauli ya mwanafalsafa maarufu Jean Jacques Rosseau aliyesema kuwa kila kiumbe huzaliwa huru lakini huwa katika pingu ulimwengu mzima. Kauli hii ilitambua ukiukaji huu wa kipengele hiki. Kipengele cha pili kinasisitiza kuwa binadamu wote wana haki za kufurahia uhuru wao pasi na kutengwa au kubezwa kwa misingi yoyote ile si rangi, kabila, jinsia, lugha, dini, asilia, utajiri au chochote kile. Vipengele vingine vinatukumbusha kuwa kila mtu ana haki ya kuishi na kupata ulinzi. Hamna mtu anayepaswa kuishi maisha ya utumwa au unyonge wa kutumikishwa kwa namna yoyote ile. Suala hili linasisitizwa na kipengele cha sita kinachokataza kudhalilishwa kwa watu au kutunzwa kwa namna yoyote ambayo inamfedhehesha kama kiumbe. Azimio la Haki za Binadamu linasisitiza kuwa binadamu yoyote nyule ana haki ya kupata ulinzi wa kisheria. Binadamu huyo hapaswi kubaguliwa na ana haki ya kupata fidia ya kisheria taraa haki zake za kimsingi zikikiukwa. Hata hivyo sio watu wote ulimwenguni ambao wanazifurahia haki hizi za kimsingi. Zipo lukuki za jamii ulimwenguni ambako haki za kimsingi zinakiukwa. Katika nchi ambazo zinaongozwa na watawala wa kiimla, si ajabu kuona haki za binadamu zikikiukwa. Viongozi wa aina hiyo huwa wamegeuzwa ng’ombe wa shemere na tamaa, ubinafsi na ukatili usiojua thamani ya utu. Viongozi wa aina hii wanasahau kuwa kila binadamu ana haki ya kuishi maisha huru, asipotumikishwa wala kulanguliwa kama bidhaa. Nchi za kiimla aghalabu huongozwa na itikadi kuwa kiongozi ndiye pekee ambaye ana uwezo wa kufikiri, kuamua na kutenda. Watu wengine wanapaswa kumfuata kisilka kama yule mbwa wa Pavlov ambaye alitokwa na mate kila kengele ilipopigwa. Viongozi wa ama hii hawachelei kuwatenza nguvu raia zao: Kuwadhalilisha kwa namna nyingi. Viongozi wa aina hiyo huiona sheria ya nchi kama iliyowekwa kwa watu wengine bali sio wao. Msimamo huu unakwenda kinyume na kipengele cha saba cha Haki Bia za Binadamu kisemacho kuwa watu wote ni sawa mbele ya sheria. Baadhi ya haki zinazokiukwa katika jamii za kimabavu ni haki ya watu kuungana, kuwaza, kushiriki katika maamuzi ya serikali, kuwa mwanachama wa jumuia waitakayo, kumiliki mali, kutembea, kuishi anakotaka kutohukumiwa bila ya kuwako na utaratibu wa kisheria. Ni muhimu hata hivyo kujua ni muhimu kwa raia wenyewe kujielimisha na kuzijua haki zao. Serikali inapaswa kuwa mlinzi wa sheria zenyewe. Lakini muhimu kujua pia kuwa mlinzi naye hulindwa pia. Maswalia) Kwa maneno kati ya 90 – 100 fafanua Haki Bia za Binadamu zilizoafikiwa na Baraza kuu la umoja wa Mataifa. (alama 10) Nakala Chafu __________________________________________________________________________ Nakala Safi __________________________________________________________________________ b) Kwa nini viongozi wa kiimla hukiuka haki za binadamu. (Maneno 50 – 60). Nakala Chafu __________________________________________________________________________ Nakala Safi __________________________________________________________________________ Mwongozo
a) Kwa maneno kati ya 90- 100 fafanua Haki Bia za Binadamu Zilizoafikiwa na Baraza kuu la Umoja wa mataifa Kila kiumbe anazaliwa humu na ana haki na hadhi sawa na kiumbe mwingine’ • Binadamu wote wana haki za kufurahia uhuru wao pasi na kutengwa au kubezwa kwa misingi yoyote ile si rangi, kabila, jinsia, lugha, dini, asilia au chochote kile. • Kila mtu ana haki ya kuishi na kupata ulinzi • Hamna mtu anayepaswa kuishi maisha ya utumwa, kutumikishwa, kudhalilishwa au kutunzwa kwa namna inayomfedhehesha kama kiumbe. • Haki ya kupata ulinzi wa kisheria • Kutobaguliwa na ana haki ya kupata fidia ya kisheria taraa haki zake za kimsingi zikikiukwa . Alama 8 utiririko alama 2) b) Kwa nini viongozi wa kiimla hukiuka haki za binadamu • Tamaa ya uongozi • Ubinafsi • Ukatili, hawajui thamani ya utu • Kiburi cha kujiona kuwa wao ndio wanaofahamu mambo zaidi • Husahau kuwa binadamu ana haki ya kuishi maisha huru bila kutumikishwa au kutanguliwa kama bidhaa • Hudhani wao tu ndio wana uwezo wa kufikiri, kuamua na kutenda na wananchi wanapaswa kufuata tu • Huona kuwa sheria ya nchi imewekewa wengine na wala sio wao hivyo huwatenza nguvu raia zao Alama 4, utiririko alama 1) Maswali na Majibu ya UFAHAMU (Alama15)Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali Tokea muundo mpya wa serikali ya ugatuzi uanze kutekelezwa miaka miwili iliyopita, kumeendelea kushuhudiwa matatizo mengi hali iliyopelekea kushuhudiwa kwa msururu wa migomo na maandamano ya raia. Fujo za karibuni kabisa ni zile zinazoshuhudiwa katika miji mikubwa za wachuuzi na wafanyibiashara wakipinga hatua za serikali za kaunti kuwatoza ushuru takribani kwa kila huduma na bidhaa ikiwemo wanyama, kuku na ndege. La kuhuzunisha zaidi katika baadhi ya majimbo imeripotiwa kuwa raia wamelazimishwa kulipa ushuru kwa kutaka tu kuona maiti za jamaa zao kwenye vyumba vya kuhifadhi maiti. Wanasiasa wameonekana kuwa na wakati mgumu kutetea mfumo huu mpya wa ugatuzi huku baadhi wakisema kwamba matatizo yanayoshuhudiwa kwa sasa yametokana na ugeni wa mfumo huo. Wengine wameinyoshea kidole serikali ya kitaifa kwamba ndiyo inayosambaratisha muundo huu. Wengine wanahoji kuwa bado ni mapema na kwamba kunatajika muda mrefu ili kufaulu. Ni wazi kwamba kumekosekana nidhamu bora ya kusimamia maisha ya raia nchini Kenya. Matatizo yanayokumba raia kwa sasa ni dalili kuwa mfumo wa serikali ya ugatuzi umeongezea chumvi kwenye kidonda badala ya kutibu. Swali ni je, hadi lini nidhamu ya kusimamia raia itakuwa ni suala la majaribio na makosa? Hatua ya kuwarundikizia raia ushuru mkubwa ni kitendo cha unyonyaji na cha dhuluma kinachofaa kupingwa. La kufahamishiwa hapa ni kwamba ushuru ndio njia kubwa ya kuzalisha mapato ya serikali zinazojifunga na mfumo wa kimagharibi wa kiuchumi wa kibepari ikiwemo Kenya. Asilimia 90 ya mapato ya serikali za kibepari huegemea ushuru. Kwa hivyo hatua ya serikali za kaunti katika kuwanyonya raia kwa kuwalipisha ushuru si ajabu bali ni thibitisho kuwa jamii ya Kenya inaongozwa na nidhamu ya kiuchumi ya ubepari mfumo wa unyonyaji na ukandamizaji. Ukweli unabakia kuwa ndani ya serikali za kibepari raia ndio hubebeshwa mzigo wa ushuru unaoishia matumboni mwa viongozi! Miito ya mabadiliko ya katiba na ya miundo mipya ya kiutawala si lolote ila ni moja tu ya hatua za mfumo wa kibepari kujipa muda wa kuishi na kuziba aibu zake za kushindwa kusimamia maisha ya watu. Kufeli huku kwa mfumo huu kunashuhudiwa hadi kwenye nchi kubwa za kibepari kama Marekani na Uingereza hivyo nazo zimekumbwa tele na maandamano na fujo za raia wakilalamikia hali ngumu ya maisha. Maswali a) Yape makala haya anwani mwafaka. (alama 1) __________________________________________________________________________ b) Eleza mtazamo wa wanasiasa kuhusu utepetevu wa mfumo huu. (alama 3) __________________________________________________________________________ c) “Ugatuzi nchini Kenya ni mfumo wa kibepari” Thibitisha kauli hii kwa kurejelea makala. (alama 3) __________________________________________________________________________ d) Migomo ni zao la matatizo yaliyogatuliwa kutoka kuu. Toa sababu nyingine zinazosababisha migomo katika serikali za ugatuzi (alama 4) __________________________________________________________________________ e) Thibitisha jinsi mfumo wa ugatuzi umeongeza chumvi kwenye kidonda badala ya kutibu (alama 2) __________________________________________________________________________ f) Eleza maana ya maneno yafuatayo (alama 2) i) Ugatuzi __________________________________________________________________________ ii) Kibepari __________________________________________________________________________ MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA (a) Changamoto za Ugatuzi/Matatatito ya tigatuzi/Ugatuzi ( alama 1x1 = 01) (b) - Ugatuzi ni mfumo geni (Alama 3x1=03) - Serikali kuu kutowajibika - Kudai kuwa mfumo huu unahitaji mda zaidi (c) - Mfumo wa ugatuzi nchini umehusisha matendo ya kibepari kama vile; (alama 3x1=03) - Raia kupewa mzigo wa kulipa ushuru ili kuipa serikali mapato - ushuru ndio njia kubwa ya kuzalisha mapato ya serlkal zinazojifunga na mfumo wa kimagharibi wa kiuchumi - viongozi kuwanyonya raia walio maskini (d) - Hali mbaya ya muundo msingi (alama 4x1= 04) - Viongozi kuendeza ufisadi - Ukosefu wa usawa katika ugavi wa rasilimali - Viongozi kupuuza mchango wa wananchi (e) - Raia kulazimishwa kulipa ili kuona maiti za jamaa zao katika fuo (alama 2x1=02) - Raia kurundikiziwa mzigo wa kulipa ushuru mkubwa - Ushuru unaolipwa na wananchi hauwasaidii wananchi la huishia mifukoni mwa viongozi (f) (i) Ugavi wa mamlaka na raslimali kutoka serikali kuu hadi mashinani (alama 2x1 =02) (ii) mfumo wa kiuchumi wa watu wachache kumiliki raslilmali kwa kuwapora wengine Ondoa nusu alama kwa kila kosa la sarufi hadi makosa sita. Ondoa nusu alama kwa kila kosa la tahajia hadi makosa sita. Maswali na Majibu ya Isimu Jamii
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
1. Barua rasmi
Wasifu kazi Maelezo ya kibinafsi
Ndoa Anwani Uana Simu Maelezo ya kielimu Chuo kikuu Shule ya sekondari Shule ya msingi (Shule ulizosomea, mitihani uliyofanya na vyeti Tajriba – kazi ulizowahi kufanya, vyeo na muda Uraibu 1. 2. Maandisha na machapisho Uanachama 1. 2. Warejelewa 1. Jina / Anwani 2. Jina / Anwani Mwanafunzi azingatie vichwa vidogo vidogo Makosa ya sarufi, hijai na mtindo yaandhibiwe 2. Serikali yafaa kufanya yafuatayo
3. Hii ni insha ya methali
ii) Na vile mhusika Yule ataishia kufanikiwa Tanbihi: mtahiniwa akionyesha upande mmoja apate chini ya 10/20. 4. Insha ya mdokezo Mtahiniwa aandike kisa kitakachoonyesha majuto baada ya kujipata taabani. Hii iwe baada ya maelekezo kutoka kwa mwalimu mkuu; yaliyoambulia patupu. Au Mwanafunzi aandike kisa kitakachoonyesha furaha baada ya kufuata ushauri wa mwalimu mkuu. Ushindi wake usababishe furaha isiyo na kifani inayoambatana na kilio na machozi ya furaha. MATUMIZI YA LUGHAa) Eleza matumizi ya kiambishi ‘ka’ katika sentensi hizi ( alama 3)
(i) Juma alikuja akachukua kitabu akaondoka …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… (ii) Mti ulikatika ukaanguka …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… (iii) “Nyanya anashona nguo”.Hamisi akasema …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… b) Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya jedwali (alama 4) Watoto wale wanafanya kazi lakini wazazi wao wanazungumza nyumbani. …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… c) Unda nomino kutokana na vitenzi hivi ( alama 2) (i) Onea ………………………………………………………………………………………………… (ii) Umia ………………………………………………………………………………………………… d) Akifisha sentensi ifuatayo (alama 2) Tulifika tukaagana na mjomba hamisi aishiye mombasa …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… e) Kwa kutoa mifano mwafaka, eleza tofauti baina ya dhana zifuatazo (alama 4) Sauti ghuna na sauti sighuna …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… f) Onyesha kiima, yambwa, na yambiwa, katika sentensi hii (alama 3) Mwanafunzi alimfutia mwalimu ubao …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… g) Andika sentensi hii kwa usemi wa taarifa (alama 2) “Lo! Kube wazuri hawajazaliwa,” Omari alisema baada ya kumwona kisura huyo. …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… h) Tunga sentensi moja moja kudhihirisha matumizi ya (alama 2) i. Posa ………………………………………………………………………………………………… ii. Poza ………………………………………………………………………………………………. i) Andika sentensi zifuatazo katika hali zilizo kwenye mabano (alama 4) i. Kijikombe chake kilivunjika baada ya kuangukia kijiwe (ukubwa) ………………………………………………………………………………………………… ii. Mtu yule haachi kuandamana na mbwa wake aliyedhoofika kisiha (udogo) ………………………………………………………………………………………………… j) Eleza maana mbili zinazotokana na sentensi ifuatayo (alama 4) Mtoto alitimua mbio, kuona nyoka …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… k) Andika sentensi ifuatayo katika kauli ya kutendesha (alama 2) Nguo zote zimekaushwa na jua ………………………………………………………………………………………………… l) Tunga sentensi kudhibitisha mwingiliano wa maneno yafuatayo (alama 2) Nomino kuwa kivumishi ………………………………………………………………………………………………… m) Andika kwa wingi (alama 2) Kuwepo kwa mshauri wake kulimfurahisha waziri ………………………………………………………………………………………………… n) Geuza sentensi ifuatayo katika hali ya mazoea huku ukiondoa -amba (alama 2) Mtoto ambaye alikula ndiye ambaye alilia ………………………………………………………………………………………………… o) Kamilisha methali ifuatayo (alama 1) Asiye na nadhari… ………………………………………………………………………………………………… p) Eleza maana ya msemo huu (alama 1) Kwenda mbago… ………………………………………………………………………………………………… UFUPISHOVipindi mbalimbali vya historia vimeshuhudia kuibuka kwa magonjwa ya ajabu. Magonjwa hayo yamewahangaisha watu na kuzishughulisha bongo za wanasayansi na madaktari katika kutafuta tiba. Magonjwa kama vile tauni, kifua kikuu, homa ya matumbo na ndui ni baadhi ya yale yaliyotisha sana nyakati fulani za historia ya binadamu. Magonjwa haya yaliwauwa maelfu ya watu na kuibua mifumo na taratibu za maisha ya watu. Hata hivyo , magonjwa hayo yaliweza kuchunguzwa na kutafutiwa tiba kabla ya kumaliza kabisa kizazi cha binadamu. Lakini hii ni baada ya kuwasukuma maelfu ya watu kaburini. Ulimwengu wa sasa unashuhudia janga jingine la maradhi sugu ya ukimwi. Neno ‘UKIMWI’ lilitolewa kutokana na athari za ugonjwa huo mwilini. Neno “UKIMWI” humaanisha ukosefu wa kinga mwilini, ambapo herufi za kwanza za maneno matatu ziliunganishwa pamoja na kuunda neno hilo. Ugonjwa huu ambao tayari umewaua mamilioni ya watu kote ulimwenguni unazidi kuenea kwa kasi, mfano wa moto katika kicheka. Kutokana na kasi yake ya kuua watu, ugonjwa wa UKIMWI umepewa majina kama vile “umeme” na pia “ugonjwa wa vijana”. Watu wengi wanaoambukizwa virusi vya UKIMWI ni wale walio na miaka kati ya 15 hadi 49. Kundi hili kwa kweli ndilo linalohesabiwa kuwa na nguvu za kutunza jamii kwa njia nyingi. Iwapo wengi katika kundi hili watakumbwa na maradhi haya, watasalia wakongwe na watoto wachanga wasioweza kujimudu. Nchini Kenya, UKIMWI uligunduliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka wa 1984. Kufikia mwezi wa Juni 1996, inakisiwa kuwa ugonjwa huu ulikuwa umewaua watu wapatao 65,647 nchini. Hivi sasa, inasemekana kuwa takribani watu zaidi ya 500 hufa kila siku nchini Kenya kutokana na janga hili. Aidha, imedhibitishwa kwamba takriban watu milioni mbili unusu tayari watapoteza maisha yao kutokana na kuaambukizwa virusi vya ugonjwa huu humu nchini. Maradhi haya sasa yamekuwa janga la kitaifa. Kutokana na kuongezeka kwa visa vya UKIMWI, hospitali na zahanati nyingi kote nchini zinashindwa kukidhi mahitaji ya wagonjwa. Kwa hivyo, makundi ya kujitolea na mashirika mbalimbali yameundwa ili kuwahudumia wagonjwa wa UKIMWI. Baadhi ya makundi hayo hutoa tiba ya kisaikolojia pamoja na kuwapa ushauri wa hima ya kuishi, badala ya kukata tamaa. Wagonjwa wengi pia huishia kutibiwa nyumbani kwao. Ugonjwa huu umeathiri jamii kwa njia nyingi. Hali ya maisha na woga, ukosefu wa matumaini, ongezeko la mayatima na kuzorota kwa uchumi kutokana na kutoweka kwa kizazi chenye nguvu za kutoa huduma kwa jamii, na baadhi ya athari za maradhi haya. Lakini jambo la kuzingatia ni hili, tujifunze kutokana na historia.Tuwe na matumaini kwamba siku moja, tiba ya ugonjwa huu itapatikana. Hii ni kwa sababu tumethibitishiwa haya kutoka katika historia yetu wenyewe. Ikiwa magonjwa yaliyosababisha vifo vya wengi kutokana na ukosefu wa tiba yalitokomezwa kupitia juhudi za kimatibabu, sembuse huu ugonjwa tulio nao sasa? Huku tukijikinga kutokana na maradhi haya, tusife moyo bali tuwe na matumaini kwani subira hufuta heri. a) Kwa kutumia maneno yako mwenyewe na bila kupoteza maana, fupisha aya nne za mwanzo (maneno 90 - 100) (alama 3 kwa mtiririko) (alama 12 )
Nakala chafu/maadalizi ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… b) Eleza mambo yanayoleta matumaini kwa wagonjwa wa ukimwi kulingana na aya tatu za mwisho (maneno 40- 45) (alama 1 kwa mtiririko) Nakala chafu ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… Nakala Safi ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… UFAHAMUSoma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yote Mgomo uliingia siku ya tano. Asubuhi hii ilikuwa mbaya. Watu mbalimbali walikwisha kamatwa mjini na shamba, wakiwemo wote waliohudhuria kikao maalumu kibandani mwa Fumu. Siku ya pili ya mgomo, Makame aliuawa upenuni pa kibanda chake.Alipatikana amechomwa visu vitano vya mbavu. Mauaji ya kikatili lakini hayakuwa ya siri. Boga, yule kijana aliyehudhuria kikao cha pamoja na Fumu, ambaye toka mwanzo hadi mwisho wa kikao hakusema lolote, saa sita za usiku, aliingia kibandani na kumchopeka Makane visu mbele ya mkewe na wanawe, kisha aliikokota maiti na kuitupa upenuni. Asubuhi, Boga alikuwa mtu wa kwanza katika mkumbo mzima. Yeye alikamatwa kwa uuaji, makosa makubwa zaidi kuliko wenzake. Kukamatwa kwa watu hakukusaidia kitu - mgomo uliendelea. Kule shamba, vilio vya wanawake walioachwa pweke vilisikika. ‘Maskini mume wangu ….maskini, bora, bora ungaliwapeleka hao ng’ombe wakapigwa sindano; kufa kwa ng’ombe si kufa kwa nafsi yako,’ alilia bibi mmoja. ‘Ee, kufa kwa wengi arusi ndugu yangu we. Mimi nimelia we, hata macho yamenivimba kwa mume wangu; ati kakataa kupeleka mazao mjini na kuwajibu askari ufidhuli, lakini halafu nimeona haina maana kulia. Bora tufunge vibwebwe na sisi tuwasaidie kucheza ngoma - wafugaji mia wamekamatwa, wakulima mia mbili na hamsini, na bado wanaendelea kukamata, mji umebaki na wanawake tu; lakini watu wenyewe wana vioja, wanapochukuliwa utawaona wanacheka, sisi tulie nini?’ Mjini kulikuwa na vilio vyake. ‘Mwanangu wamemchukua , wanasema watamfunga au watamwua, kafanyaje? Daima kawatumikia , kapoteza nguvu zake juu yao na sasa…’Alimnung’unikia bibi mmoja. ‘Nini bibi we, wachukuzi na makuli watapata haki zao, na wale wanaozurura iko siku wataajiriwa na watakuta mambo mazuri, na wafanyikazi viwandani watachoka kufukuzwa ovyo ; hivyo ndivyo alivyonambia mwanangu alipokuwa akitoka, pingu mikononi. Nililia bibi, uchungu wa mwana unaujua bibi yangu, lakini baadaye nilipofikiri, nikachanganyisha na yale aliyokuwa akaniambia Ali mwanangu, kila siku; niliuhisi uzito wa maneno yake, nikafuta chozi babu.’ Wasaliti walikuwepo, lakini nafasi ya kusaliti haikupatikana. Kwenye lango la bandarini makuli na wachukuzi walisimama imara na marungu na mapanga tayari kuwang’ariba wahaini wowote. Ng’ambo, vikundi vilitawanyika na kufanya kazi; Wengine walitembea mipini mikononi, tayari kumtia adabu yeyote aliyetokwa na imani ya mgomo. Kikundi kingine kiliwekwa sokoni. Hakuna kitu kilichoingia wala kilichotoka. Magari hayakuwa na safari za shamba wala mjini. Askari walitembea ovyo na kumkamata waliyetaka kumkamata, lakini hakukutokea ghasia wala kupigwa mtu. Mgomo uliendelea, ukimuathiri kila mtu, lakini wale waliodai haki zao hawakuvunja kani. ( Dunia Mti Mkavu-Saidi Ahmed Mohamed) MASWALI
Tanakali za Sauti: Kuwasiliana kwa Ufanisi kwa Kutumia Sauti PekeeMaelezo ya Tanakali za Sauti
Tanakali za sauti, au masimulizi ya sauti, ni aina ya mawasiliano ambayo hutumia sauti pekee bila kutumia picha au maandishi. Katika tanakali za sauti, hadithi au ujumbe huwasilishwa kupitia sauti na sauti za watu wanaoigiza. Hii inaruhusu hadhira kuvutiwa na kuelewa ujumbe kupitia mazungumzo, athari za sauti, na muziki. Tanakali za sauti zina historia ndefu, na zimekuwa maarufu katika redio, vipindi vya televisheni, na hata katika ulimwengu wa podcasting. Zinaweza kuwa na mifano mingi, kama vile hadithi za uhalifu, hadithi za kusisimua, makala za kielimu, na hata mafundisho ya lugha. Mara nyingi, tanakali za sauti zinahitaji maandalizi ya kutosha ili kuunda uzoefu wa kusikiliza wenye ubora. Hii inaweza kujumuisha kuandika hadithi au script, kuchagua sauti za watu wanaoigiza, kupanga athari za sauti, na kuchagua muziki unaofaa. Kwa kuongezea, mbinu za uigizaji na ubora wa sauti ni muhimu ili kuvutia na kushirikisha hadhira. Kuna faida kadhaa za kutumia tanakali za sauti. Kwanza, zinaruhusu hadhira kujenga picha za kujisikia na kufikiria mazingira na wahusika wa hadithi. Hii inaweza kuwa na athari ya kina na kusisimua, ikiruhusu hadhira kujenga uzoefu wa kipekee na wa kibinafsi. Pia, tanakali za sauti zinaweza kupatikana na kusikilizwa kwa urahisi, na kutoa nafasi kwa watu kufurahia hadithi au ujumbe wakati wowote na mahali popote, hata bila kuwa na ufikiaji wa picha au maandishi. Kwa kumalizia, tanakali za sauti ni njia nzuri ya mawasiliano ambayo hutumia sauti pekee. Zinaweza kuwa na mifano mbalimbali na zinahitaji maandalizi ya kutosha ili kuunda uzoefu wa kusikiliza wenye ubora. Tanakali za sauti zinatoa fursa ya kusisimua na kuunda picha za kujisikia katika akili za hadhira, na zinaweza kupatikana kwa urahisi na kusikilizwa mahali popote. Maswali
a) Taja na ueleze sifa za mtambaji bora katika fasihi simulizi. (alama 10)
b) Nyimbo zina wajibu gani katika jamii. (alama 4) c) i) Eleza maana ya vitendawili. (alama 2) ii) Onyesha sifa za kitendawili. (alama 4) Majibu
a) Sifa za mtambaji bora
b) Wajibu wa nyimbo
c)
i) Kitendawili ni fumbo/msemo wa kimafumbo ambao hufumbua jambo fulani na hutolewa kwa hadhira au wasikilizaji ili waufumbue. 1 x 2= 2 ii) Hutangulizwa kwa njia maalumu a) Ujumbe wake ni wa kimafumbo b) Ufananisho wa kijazanda c) Ni fupi kwa maelezo d) Hutegemea mazingira/sehemu Fulani 4 x 1 = 4 Maswali
a) Taja na ueleze aina nne za hadithi (alama 8)
b) Eleza mbinu tatu ambazo mtambaji anaweza kutumia kuishirikisha hadhira yake.(alama 6) c) Fafanua vipera vifuatavyo vya fasihi simulizi. (alama 6) i) Majigambo ii) Mivigha iii) Lakabu Majibu
a)
i) Visasili - Hadithi zinazosimulia asili ya watu, vitu ama tabia Fulani. ii) Ngano za mazimwi - Husimulia kuhusu mazimwi iii) Hurafa - Hadithi ambazo zina wahusika wanyama lakini waliopewa tabia za binadamu. iv) Hekaya - Ngano fupi zinazosimulia matukio ya kushangaza yanayoonyesha hila au ujanja wa mwanadamu v) Mighani - Ngano za ushujaa Mighani huwa na lengo la kueleza visa na mikasa ya watu ama mashujaa wa jamii fulani.( mwalimu akadirie aina nyingine)
b)
c)
i) Majigambo – Mazungumzo yanayotolewa na mtu fulani ili kujitapa ii) Mivigha – sherehe maalum za kitamaduni ambazo hufanywa na jamii katika kipindi maalum. iii) Lakabu – Majina ya utani au kupanga ambayo watu hujipa au kupewa
Soma maagizo yafuatayo kisha ujibu maswali
(Alfajiri kuu. Vijana wanazunguka kinu, vifua wazi. Nyusoni wamepakwa masizi na aina ya tope jeupe. Wako katikati yam situ. Mzee Jando ameketi kwenye namna yam to wa nyasi.)
Mzee Jando: (Akiwahiza) haraka! Ongezeni kasi! Zunguka! Haya imbeni, barobaro!
Vijana: jua lachomoza! Muda umefika wa mbegu kuatika! Ichipuke na kuzalisha matunda! Ni leo, ni sasa!
Mzee Jando: haya ketini sasa
Vijana: (Vijana wanaketi katika mistari huku wameshikana mikono mabegani) Mzee Jando: tulisema mume nini? Vijana: (kwa pamoja na kwa sauti ya dhati) Mume ni kazi Sio ubazazi Ale jasho lake
Mzee Jando: Sawa kabisa, je mume ni nani?
Vijana: Ni mlinzi wa jamii Ni mfano mwema wa jitihada Apambane na adui Atende wajibu na maadili
Mzee Jando: Jambo linalovunja umoja!
Vijana: Likumbatiwe na kufunzwa hata watoto wachanga! Mzee Jando: Haya, semeni wenyewe leo! Vijana: Leo tumkomaa, si watoto tena Tumetimia barobaro kamili Sisi ni stadi Sisi ni wapevu! Tayari kwa majukumu ya kujenga jamii Sisi ni tegemeo la umma Sisi ndio chimbuko la wema Maadili na upendo
Mzee Jando: Nakubali mko tayari. Haya tuendelee na ada zetu zingine. Kijembe kukidhihaki!
Vijana: (Wanasimama kijasiri na kurindimisha sauti) Tuko tayari kuingia utuuzima! maswali
majibu
“La, Mzee…. Mbio za sakafuni zimefika ukingoni” (al 4) (a) Eleza muktadha wa dondoo hili (b) Mbio zipi zimefika ukingoni? (al 4) (c) Fafanua maudhui mawili yanayojitokeza katika dondoo lenyewe. (al 4) (d) Taja mbinu za lugha zinazojitokeza hapa. (al 4) (a) Eleza muktadha wa dondoo hili (al 4) (i) Maneno ya Kenga (ii) Anamwambia Majoka (iii) Nje ya lango la soko la Chapakazi (iv) Baada ya Majoka kulalamika kuwa Kenga alikuwa ameshindwa kazi kwa kuwakubali wapinzani kufika pale sokoni. (b) Mbio zipi zimefika ukingoni? (al 8)
(c) Fafanua maudhui mawili yanayojitokeza katika dondoo lenyewe. (al. 4)
(d) Taja mbinu za lugha zinazojitokeza hapa? (al. 4)
Soma makala yafwatayo kisha ujibu maswali yafwatayo
Hapo zamani za kale, paloindokea mtu mmoja kwa jina mzee Kata. Mzee Kata alikuwa na wake wawili. Mke wa kwanza aliitwa Neema na wa pili aliitwa Nduli. Kila mmoja wa wake hawa alikuwa na mtoto mmoja. Neema alikuwa na mtoto wa kike kwa jina Majaliwa. Majaliwa alikuwa ameumbwa akaumbika.Uso wake ulihimili macho meupe mfano wa theluji. Meno yake ya juu yalipangika kwa njia ambayo iliyafanya kuacha mwanya ambao ulifanya tabasamu yake kuwa ya mvuto wa sumaki. Urembo wa Majaliwa, kama walivyosema wengi, ungemtoa nyoka yeyote pangoni.
Kwa upande mwingine Kutu, bintiye Nduli, alikuwa mwenye sura mbaya ya kutisha.Uso wake usiopendeza ulimfanya kuonekana kama ajuza wa miaka mia moja! Tabia yake ya ukorofi ilikoleza mvuto wake hasi. Vijana wa kijijini walimfanyia inadi kila mara kwa kumkumbusha kuwa hakufaa kuringa. “Sura kama kiboko”, wangemtania
Tofauti za kiumbo kati ya Majaliwa na Kutu zilizua uhasama mkubwa kati ya ndugu hawa, sikwambii mama zao. Hali hii ilizidishwa Zaidi na nongwa za kila siku zilizotokana na ukewenza. Familia yam zee Kata ikawa medaniya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Hali ya mtafaruku iliendelea kuikosesha nyumba yam zee kata amani. Asubuhi moja, Mzee Kata aliamka kama kawaida yake, alijikohoza kama isharaya kutangaza kufika kwake. Daima hakupenda kuzungumza na wakeze asubuhi na mapema. Aliamini kuwa wangemletea nuksi. Kinyume na siku nyingine, mzee Kata hakuitikiwa. Ilibidi kujikaribisha nyumbani mwake. Mara tu alipovuka kizingiti cha kijumba hicho, alitupa macho yake juu yakitanda cha mayoweambapo mke wake alijinyosha twaa kakauka kama ukuni; hanapumzi. Weupe wa macho yake na mapovu yaliyomtoka kinywani yalimhakikishia Mzee Kata kuwa Neema kampungia mkono. Harufu kali ya sumu ilihanikiza hewa kumwarifu kuwa Mzee kata kuwa mkewe kafa kwa kutendwa na mkemwenza
Maisha ya Majaliwa yalichukua mkondo mpya baada ya tanzia hii. Mama wa kambo sasa alipata mwanya wa kumhini majaliwa. Kazi zote za nyumbani aliachiwa yeye.Huku Kutu akiachwa huru kucheza. Majaliwa alipewa chakula hapa; wengine wakila biriani yeye alipewa wali wa kawaida. Mavazi yake yaligeuka matambara.Siku zilivyozidi kusonga ndivyo mateso yalivyoongezeka. Mama wa kambo alizidisha wivu wake kwa majaliwa. Hata Majaliwa alipovunja ungo na wachumba kuja kumposa, mama wa kambo aliwafukuzia mbali. Wenine walihimizwa kumposa Kutu. Wachumba waliochachawa kutaka kumuoa majaliwa wakidai kuwa hawamtaki Kutu kwa sababu ya kiburi chake, walinyeshewa matusi, wakahizinika na kujiendea zao.
Siku moja alitokea kijana mmoja makini .alikuja amavalia gwanda jeusi lililojiinamia kwa uchovu. Viatu alivyovaa vilikuwa vimejichokea kwa kupiga lami. Kofia iliokuwa kichwani pake ilitosha kumhakikishia mama wa kambo kuwa huyu alikuwa fakiri. Mama mtu alikubali mara moja posa ya kijana huyu kwa Majaliwa akijua kuwa angeadhibika. Aliamini amemtokomeza Majaliwa ndani ya lindi la ulitima. Mzee Kata naye hakusita kumwoza Majaliwa kwa kiajana huyu maana aliiona hii kama fursa ya pekee ya kumwepusha vitimbi vya mama wa kambo Majaliwa aliandamana na mume wake hadi Kijiji cha peponi ambako kijana huyu allishi. Wallingia katika nyumba ya msonge ambamo Majaliwa alitarajia kuanza Maisha ya ndoa. Walitayarisha chajio, wakala na kulala.
Asubuhi, Majaliwa aliamshwa na nyimbo za ndege. Alipofunguamacho, alijikuta kalala ndani mya chumba chenye sakafu ya vigae. Ukuta wa chumba hicho ulikuwa wa rangi wa zari. Mapambo ya dhahabu yalitundkwa ukutani. Kumbe kijana aliyemuoa hakuwa maskini kama ilivyodhaniwa! Alikuwa mwana wa mfalme! Na hili lilikuwa kasri hasa! Majaliwa hakueza kuamini! Alikuwa ameamkia Maisha ambayo hakuwahi yawazia.
Alipoingia sebuleni alimpata mama yake mpenzi, akiwa na tabasamu ya milele usoni. Walikumbatiana kwa shauku kuu. Kumbe kijana huyo alikuwa ametumwa na mamake Majaliwa! Mumewe majaliwa alishuhudia kwa umbali. Machozi ya mama mtu na mwanawe yakilovya vifua vyao na kuyeyusha simanzi na kuyeyusha simanzi iliyokuwa imeyaandama Maisha yao. Tangu siku hiyi, watu hawa wallishi kwa raha mstarehe. Hadithi yangu inaishia hapo.
MASWALI
a) Taja na utolee mifano mbinu sita za kimtindo zilizotumiwa katika utungo huu (al.3)
b) Utungo huu unaweza kuainishwa kama ngamo, toa sababu (al.1) c) Fafanua umuhimu nne wa formula ya kumalizia katika utungo huu (al. 4) d) Taja shughuli moja ya kijamii katika jamii ya utungo huu (al. 1) e) Jadili tatizo moja la ukewenza katika utungo huu (al.1) f) Taja na ufafanue dhima tano ya utungo huu katika jamii yake (al.5) g) Taja mambo mawili ambayo fanani anaweza kutekeleza ili kuufanya utungo huu uwe wa kuvutia Zaidi (al. 1) h) Miviga ni nini? (al.1) i) Taja hasara tatu za miviga (al.3) MAJIBU
a) MBINU ZA KIMTINDO
i) Tashbihi -Sura kama kiboko ii) msemo/nahau -Kumtoa nyoka pangoni iii) Nidaa- Ajuza wa miaka mia moja iv) Taswira mnuso- Harufu v) Usimulizi- Hapo zamani za kale vi) Istiara- Mavazi kugeuka matambara vii) Majazi-Neema, Majaliwa, Nduli viii) Tashhisi- harufu kumwarifu ( 1/2x6= alama 3)
b) i) kuna formula ya ufunguzi- hapo zamani za kale
ii) kuna formula ya kumalizia- Hadithi yangu inaishia hapo (1x1=alama 1)
c) UMUHIMU WA FOMULA YA KUMALIZIA
i) Kurudisha wasikizaji kwa hali ya kawaida ii) Kubeba wazo au maudhui au ujumbe wa hadithi iii) Onyesha mwisho wa hadithi iv) Pahsa mtambali anayefuata. Pisha shughuli inayofuata v) Kitulizo kwa hadhira baada ya kumakinika kwa muda vi) Kutoa changamotomkwa hadhira. (4x1=alama 4)
D SHUGHULI ZA KIJAMII
i) Ndoa- Wake wawili, Nduli kukosa kupashashwa, Majaliwa kuolewa 1x1= alama 1
E MATATIZO YA UKEWENZA
i) Wivu- mamake majaliwa kupewa sumu ii) Mateso kwa wana wa wake wenza- majaliwa kuteswa na mamake Nduli (1x1= alama 1)
F DHIMA YA UTUNGO
i) Huelimisha ii) Huburudisha iii) Huadilisha iv) Hukuza utamaduni v) huleta utangamano vi) Hukuza ubunifu vii) Hukuza uwezo wa kukumbusha viii) Hutoa onyo ix) Ni kitambulisho cha jamii x) Hukuza ujasiri xi)Hukuza historia (5x1=alama 5) mwanafunzi atoe maelezo Zaidi ndiposa apewe
G) MAMBO YA KUFANYA HADITHI KUVUTIA
i) Kutumia Ishara kama miondoko ii) Kutumia ala za muziki iii) kutumia maleba iv) Kushirikisha hadhira v) kuimba vi) Kucheka (2x1/2=alama 1)
H) MIVIGA- sherehe za kitamaduni ambazo hufanywa na jamii katika kipindi au wakati maalumu wa mwaka (1x1=alama 1)
I) HASARA ZA MIVIGA
ii) Zingine zimepitwa na wakati kama vile tohara ya wanawake. Huhatarisha Maisha ya waathiriwa ii) Zingine hukinzana na malengo ya taifa kama vile ukeketaji wa Watoto wa kike iii) Zingine hujaza watu hofu kama zile zinazotumia kafara ya binadamu iv) zingine huleta uhasama kati ya koo hasa zile za kufukuza mapepo v) Zingine ni ghali kwani huhitaji fedha nyingi na kusababisha umaskini (3x1=alama 3) b) Fafanua majukumu yoyote manne ya nyimbo katika jamii. (Al 8)Fafanua majukumu yoyote manne ya nyimbo katika jamii. (Al 8)
|
Primary Resources
College Resources
|
Secondary Resources
|
Contact Us
Manyam Franchise
P.O Box 1189 - 40200 Kisii Tel: 0728 450 424 Tel: 0738 619 279 E-mail - sales@manyamfranchise.com |