Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
FASIHI SIMULIZI MODEL20240619001 a) Nini maana ya maghani ? (alama 2) b) Eleza aina za maghani zifuatazo. (alama 10) i) Vivugo ii) Tondozi iii) Sifo iv) Tendi v) Rara c) Eleza sifa nne za maghani. (alama 4) d) Taja umuhimu wa maghani. (alama 4) MAJIBU
FASIHI SIMULIZI a)Maghani ni utungo wa kishairi ambao hutongolewa kwa kutumia sauti iliyo kati ya uimbaji na uzungumzaji, yaani kalimia na watu wanaojigamba kuhusu ufanisi au kusifu watu wengine, vitu au viumbe. b) i) Vivugo : Ni utungo wa kujisifia unaotungiwa papo aghalabu na fanani mwanamme. Majisifu yenyewe huwa ni baada ya ushindi katika harakati ngumu k.m. kumuua simba, kuoa msichana aliyependwa na wengi n.k. Fanani hutaja jina lake. ii) Tondozi : Ni utungo wa kutukuza watu, wanyama, vitu, magari, miti, ng’ombe – Husifu maumbile, sura, tabia , matendo n.k iii) Tendi : Usimulizi mrefu wa kishairi unaotungwa papo kwa papo na hueleza tukio kuu la kihistoria kwenye jamii au taifa. iv) Rara : Hadithi fupi ya kishairi yenye ubunifu mkubwa unaokusudiwa kusisimua. Unatongolewa kwa kuimbwa au kughanwa ukiandamanishwa na ala za muziki. c) Sifa za maghani 1.Hukaririwa au kusemwa bila kuimbwa. 2.Huwahusu mashujaa au vitu kwa sababu Fulani. 3.Hufanyika zaidi wakati wa sherehe. 4.Huhusisha majigambo, majitapo. d)Umuhimu wa maghani
0 Comments
|
Categories
All
Archives
June 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|