USHAIRI MASWALI NA MAJIBU
SOMA SHAIRI LIFUATALO KISHA UJIBU MASWALI.Msambe naja kuteta, nina wema wa kalima, Moto wanikatakata, maini yangu yachoma, Ili nipate takata, ukweli wote ‘tasema, Anayekataa pema, pabaya panamuita. Bahati ni kama nyota, humemeta na Kuzima, Sikimbilie mafuta, ukatae Kula sima, Anayekataa pema, pabaya Panamuita. Haraka zina matata, angaza mbele na Nyuma, Tenda mambo kwa kusita, Usije ukalalama, Keti pako ukipata, Kwa muradi wa uzima, Anayekataa Pema, pabaya panamuita. Pema si penye mafuta, au pa wali Na nyama, Pema watu hutafuta, Utulivu na hekima, Si hoja penye Ukata, pa watu hali ya nyuma, Anayekataa pema, pabaya Panamuita Mahali pema ambata, kwa vitendo na huduma, Sikae penye matata, palipojaa hasma, Lau kama pamemeta, hapafai kwa daima, Anayekataa pema, pabaya panamuita Maswali a) Lipe anwani mwafaka shairi hili. (alama 1) b) Bainisha bahari mbili za shairi hili. (alama 2) c) Eleza muundo wa shairi hili. (alama 4) d) Fafanua dhamira ya mshairi. (alama 1) e) Andika ubeti wa tatu kwa lugha ya nathari. (alama 4) f) Onyesha jinsi mshairi alivyotumia uhuru wake. (alama 3) g) Kwa kutoa mifano, bainisha tamathali mbili za usemi zilizotumika katika shairi hili. (alama 2) h) Eleza maana ya msamiati ufuatao. (alama 3) i) Kalima ii) Mafuta iii) Ukata Majibu
a) Lipe anwani mwafaka shairi hili (al 1) Anayekataa pema, pabaya pamuita b) Bahari mbili za shairi hili (al 2) i) sakarani ii) Masivina – halina urari wowote wa vina c) Muundo wa shairi hili (al 4) - Beti nne - Lina kibwagizo ‘Anayekataa pema, pabaya pamuita’. - Halijazingatia mtoshelezo wa mishororo ktk kila ubeti - Halina urari wa vina d) Dhamira ya shairi ni kuhimiza kuhusu umuhimu wa uadilifu na mienendo inayofaa. (al 1) hakiki e) Mahali pema si pale ambapo pana vizuri bali palipo na utulivu na hekima. Hata kama pana umaskini, mtu anapokataa mahali pema huitwa na pabaya. (al 4) f) (i) Inkisan - Tasema - sikimbilie (ii) Msamiati wa kale- mato badala ya macho (iii) Kuboronga sarufi – keti pako ukipata (iv) Tabdila – muradi (zozote 3) g) Tamathali mbili za usemi (al 2) Tashbihi – Bahati ni kama nyota. Jazanda - mafuta, wali na nyama zimetumika kijazanda (zozote 2) h) Maana ya (i) Kalima – usemi (ii) Mafuta – mng’aro (iii) Ukata - umaskini
0 Comments
|
AuthorAtika School Team Archives
June 2024
Categories
All
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|