USHAIRI MASWALI NA MAJIBU
Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswaliKwanza matatu muhimu, ni utu uke na ume Pili kwa mwanadamu, awe na kitu atume, Tatu awe na fahamu, ye dini isimhame, Haya ni mambo adhimu, kwa mke na mwanamume, Mambo ye adimu, huyataka kwa. shime. Kwa la kwanza twaanzana, twaendelea kudumu, Na kitu tunaonana, gharama twaweza kimu, Maisha hayani laana, wala hayawi magumu, La tatu shaka halina, humpamba mwenadamu, Kwa fikira na kuoka, mambo yaliyolazimu. Kwa uwezowe Mwenyezi, mdumisha kila kitu, Matatu haya azizi, karibu kwa kila mtu, Yana hawa na mapenzi, katika nafsi zetu, Na katika matembezi, dunia hii yetu, Kuyakasa hatuwezi, na ndiyo utumwa. Ni utumwa madhabuti, hatuwezi kuuvua, Umetushika kifatu, kwa tadi na kwa takua, Katuizi hatujuti, tumo tunachukua, Na nafasi hatujati, kidogo. ya kuumua, Mpaka yaje mauti, uhuru kutuletea. MASWALI (a) Shairi hili ni la aina gani? Kwa nini? (alama 2) (b) Taja mambo matatu muhimu ambayo sharti binadamu awe nayo kulingana na Mshairi.(alama 3) (c) Eleza umuhimu wa kila mojawao katika mambo hayo matatu kama yaliyofafanuliwa na mshairi. (alama 6) (d) Taja bahari zmnazojitokeza katika shairi hili. (alama 2) (e) Uandike ubeti wa kwenza katika lugha nathari. (alama 5) (f) Onyesha kwa kutumia namna ambavyo mtunzi ametumia uhuru wa kishairi. (alama 2)
0 Comments
Leave a Reply. |
AuthorAtika School Team Archives
June 2024
Categories
All
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|