Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
Maswali na Majibu ya Isimu Jamii
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
1. Barua rasmi
Wasifu kazi Maelezo ya kibinafsi
Ndoa Anwani Uana Simu Maelezo ya kielimu Chuo kikuu Shule ya sekondari Shule ya msingi (Shule ulizosomea, mitihani uliyofanya na vyeti Tajriba – kazi ulizowahi kufanya, vyeo na muda Uraibu 1. 2. Maandisha na machapisho Uanachama 1. 2. Warejelewa 1. Jina / Anwani 2. Jina / Anwani Mwanafunzi azingatie vichwa vidogo vidogo Makosa ya sarufi, hijai na mtindo yaandhibiwe 2. Serikali yafaa kufanya yafuatayo
3. Hii ni insha ya methali
ii) Na vile mhusika Yule ataishia kufanikiwa Tanbihi: mtahiniwa akionyesha upande mmoja apate chini ya 10/20. 4. Insha ya mdokezo Mtahiniwa aandike kisa kitakachoonyesha majuto baada ya kujipata taabani. Hii iwe baada ya maelekezo kutoka kwa mwalimu mkuu; yaliyoambulia patupu. Au Mwanafunzi aandike kisa kitakachoonyesha furaha baada ya kufuata ushauri wa mwalimu mkuu. Ushindi wake usababishe furaha isiyo na kifani inayoambatana na kilio na machozi ya furaha.
0 Comments
MATUMIZI YA LUGHAa) Eleza matumizi ya kiambishi ‘ka’ katika sentensi hizi ( alama 3)
(i) Juma alikuja akachukua kitabu akaondoka …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… (ii) Mti ulikatika ukaanguka …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… (iii) “Nyanya anashona nguo”.Hamisi akasema …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… b) Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya jedwali (alama 4) Watoto wale wanafanya kazi lakini wazazi wao wanazungumza nyumbani. …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… c) Unda nomino kutokana na vitenzi hivi ( alama 2) (i) Onea ………………………………………………………………………………………………… (ii) Umia ………………………………………………………………………………………………… d) Akifisha sentensi ifuatayo (alama 2) Tulifika tukaagana na mjomba hamisi aishiye mombasa …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… e) Kwa kutoa mifano mwafaka, eleza tofauti baina ya dhana zifuatazo (alama 4) Sauti ghuna na sauti sighuna …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… f) Onyesha kiima, yambwa, na yambiwa, katika sentensi hii (alama 3) Mwanafunzi alimfutia mwalimu ubao …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… g) Andika sentensi hii kwa usemi wa taarifa (alama 2) “Lo! Kube wazuri hawajazaliwa,” Omari alisema baada ya kumwona kisura huyo. …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… h) Tunga sentensi moja moja kudhihirisha matumizi ya (alama 2) i. Posa ………………………………………………………………………………………………… ii. Poza ………………………………………………………………………………………………. i) Andika sentensi zifuatazo katika hali zilizo kwenye mabano (alama 4) i. Kijikombe chake kilivunjika baada ya kuangukia kijiwe (ukubwa) ………………………………………………………………………………………………… ii. Mtu yule haachi kuandamana na mbwa wake aliyedhoofika kisiha (udogo) ………………………………………………………………………………………………… j) Eleza maana mbili zinazotokana na sentensi ifuatayo (alama 4) Mtoto alitimua mbio, kuona nyoka …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… k) Andika sentensi ifuatayo katika kauli ya kutendesha (alama 2) Nguo zote zimekaushwa na jua ………………………………………………………………………………………………… l) Tunga sentensi kudhibitisha mwingiliano wa maneno yafuatayo (alama 2) Nomino kuwa kivumishi ………………………………………………………………………………………………… m) Andika kwa wingi (alama 2) Kuwepo kwa mshauri wake kulimfurahisha waziri ………………………………………………………………………………………………… n) Geuza sentensi ifuatayo katika hali ya mazoea huku ukiondoa -amba (alama 2) Mtoto ambaye alikula ndiye ambaye alilia ………………………………………………………………………………………………… o) Kamilisha methali ifuatayo (alama 1) Asiye na nadhari… ………………………………………………………………………………………………… p) Eleza maana ya msemo huu (alama 1) Kwenda mbago… ………………………………………………………………………………………………… UFUPISHOVipindi mbalimbali vya historia vimeshuhudia kuibuka kwa magonjwa ya ajabu. Magonjwa hayo yamewahangaisha watu na kuzishughulisha bongo za wanasayansi na madaktari katika kutafuta tiba. Magonjwa kama vile tauni, kifua kikuu, homa ya matumbo na ndui ni baadhi ya yale yaliyotisha sana nyakati fulani za historia ya binadamu. Magonjwa haya yaliwauwa maelfu ya watu na kuibua mifumo na taratibu za maisha ya watu. Hata hivyo , magonjwa hayo yaliweza kuchunguzwa na kutafutiwa tiba kabla ya kumaliza kabisa kizazi cha binadamu. Lakini hii ni baada ya kuwasukuma maelfu ya watu kaburini. Ulimwengu wa sasa unashuhudia janga jingine la maradhi sugu ya ukimwi. Neno ‘UKIMWI’ lilitolewa kutokana na athari za ugonjwa huo mwilini. Neno “UKIMWI” humaanisha ukosefu wa kinga mwilini, ambapo herufi za kwanza za maneno matatu ziliunganishwa pamoja na kuunda neno hilo. Ugonjwa huu ambao tayari umewaua mamilioni ya watu kote ulimwenguni unazidi kuenea kwa kasi, mfano wa moto katika kicheka. Kutokana na kasi yake ya kuua watu, ugonjwa wa UKIMWI umepewa majina kama vile “umeme” na pia “ugonjwa wa vijana”. Watu wengi wanaoambukizwa virusi vya UKIMWI ni wale walio na miaka kati ya 15 hadi 49. Kundi hili kwa kweli ndilo linalohesabiwa kuwa na nguvu za kutunza jamii kwa njia nyingi. Iwapo wengi katika kundi hili watakumbwa na maradhi haya, watasalia wakongwe na watoto wachanga wasioweza kujimudu. Nchini Kenya, UKIMWI uligunduliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka wa 1984. Kufikia mwezi wa Juni 1996, inakisiwa kuwa ugonjwa huu ulikuwa umewaua watu wapatao 65,647 nchini. Hivi sasa, inasemekana kuwa takribani watu zaidi ya 500 hufa kila siku nchini Kenya kutokana na janga hili. Aidha, imedhibitishwa kwamba takriban watu milioni mbili unusu tayari watapoteza maisha yao kutokana na kuaambukizwa virusi vya ugonjwa huu humu nchini. Maradhi haya sasa yamekuwa janga la kitaifa. Kutokana na kuongezeka kwa visa vya UKIMWI, hospitali na zahanati nyingi kote nchini zinashindwa kukidhi mahitaji ya wagonjwa. Kwa hivyo, makundi ya kujitolea na mashirika mbalimbali yameundwa ili kuwahudumia wagonjwa wa UKIMWI. Baadhi ya makundi hayo hutoa tiba ya kisaikolojia pamoja na kuwapa ushauri wa hima ya kuishi, badala ya kukata tamaa. Wagonjwa wengi pia huishia kutibiwa nyumbani kwao. Ugonjwa huu umeathiri jamii kwa njia nyingi. Hali ya maisha na woga, ukosefu wa matumaini, ongezeko la mayatima na kuzorota kwa uchumi kutokana na kutoweka kwa kizazi chenye nguvu za kutoa huduma kwa jamii, na baadhi ya athari za maradhi haya. Lakini jambo la kuzingatia ni hili, tujifunze kutokana na historia.Tuwe na matumaini kwamba siku moja, tiba ya ugonjwa huu itapatikana. Hii ni kwa sababu tumethibitishiwa haya kutoka katika historia yetu wenyewe. Ikiwa magonjwa yaliyosababisha vifo vya wengi kutokana na ukosefu wa tiba yalitokomezwa kupitia juhudi za kimatibabu, sembuse huu ugonjwa tulio nao sasa? Huku tukijikinga kutokana na maradhi haya, tusife moyo bali tuwe na matumaini kwani subira hufuta heri. a) Kwa kutumia maneno yako mwenyewe na bila kupoteza maana, fupisha aya nne za mwanzo (maneno 90 - 100) (alama 3 kwa mtiririko) (alama 12 )
Nakala chafu/maadalizi ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… b) Eleza mambo yanayoleta matumaini kwa wagonjwa wa ukimwi kulingana na aya tatu za mwisho (maneno 40- 45) (alama 1 kwa mtiririko) Nakala chafu ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… Nakala Safi ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… UFAHAMUSoma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yote Mgomo uliingia siku ya tano. Asubuhi hii ilikuwa mbaya. Watu mbalimbali walikwisha kamatwa mjini na shamba, wakiwemo wote waliohudhuria kikao maalumu kibandani mwa Fumu. Siku ya pili ya mgomo, Makame aliuawa upenuni pa kibanda chake.Alipatikana amechomwa visu vitano vya mbavu. Mauaji ya kikatili lakini hayakuwa ya siri. Boga, yule kijana aliyehudhuria kikao cha pamoja na Fumu, ambaye toka mwanzo hadi mwisho wa kikao hakusema lolote, saa sita za usiku, aliingia kibandani na kumchopeka Makane visu mbele ya mkewe na wanawe, kisha aliikokota maiti na kuitupa upenuni. Asubuhi, Boga alikuwa mtu wa kwanza katika mkumbo mzima. Yeye alikamatwa kwa uuaji, makosa makubwa zaidi kuliko wenzake. Kukamatwa kwa watu hakukusaidia kitu - mgomo uliendelea. Kule shamba, vilio vya wanawake walioachwa pweke vilisikika. ‘Maskini mume wangu ….maskini, bora, bora ungaliwapeleka hao ng’ombe wakapigwa sindano; kufa kwa ng’ombe si kufa kwa nafsi yako,’ alilia bibi mmoja. ‘Ee, kufa kwa wengi arusi ndugu yangu we. Mimi nimelia we, hata macho yamenivimba kwa mume wangu; ati kakataa kupeleka mazao mjini na kuwajibu askari ufidhuli, lakini halafu nimeona haina maana kulia. Bora tufunge vibwebwe na sisi tuwasaidie kucheza ngoma - wafugaji mia wamekamatwa, wakulima mia mbili na hamsini, na bado wanaendelea kukamata, mji umebaki na wanawake tu; lakini watu wenyewe wana vioja, wanapochukuliwa utawaona wanacheka, sisi tulie nini?’ Mjini kulikuwa na vilio vyake. ‘Mwanangu wamemchukua , wanasema watamfunga au watamwua, kafanyaje? Daima kawatumikia , kapoteza nguvu zake juu yao na sasa…’Alimnung’unikia bibi mmoja. ‘Nini bibi we, wachukuzi na makuli watapata haki zao, na wale wanaozurura iko siku wataajiriwa na watakuta mambo mazuri, na wafanyikazi viwandani watachoka kufukuzwa ovyo ; hivyo ndivyo alivyonambia mwanangu alipokuwa akitoka, pingu mikononi. Nililia bibi, uchungu wa mwana unaujua bibi yangu, lakini baadaye nilipofikiri, nikachanganyisha na yale aliyokuwa akaniambia Ali mwanangu, kila siku; niliuhisi uzito wa maneno yake, nikafuta chozi babu.’ Wasaliti walikuwepo, lakini nafasi ya kusaliti haikupatikana. Kwenye lango la bandarini makuli na wachukuzi walisimama imara na marungu na mapanga tayari kuwang’ariba wahaini wowote. Ng’ambo, vikundi vilitawanyika na kufanya kazi; Wengine walitembea mipini mikononi, tayari kumtia adabu yeyote aliyetokwa na imani ya mgomo. Kikundi kingine kiliwekwa sokoni. Hakuna kitu kilichoingia wala kilichotoka. Magari hayakuwa na safari za shamba wala mjini. Askari walitembea ovyo na kumkamata waliyetaka kumkamata, lakini hakukutokea ghasia wala kupigwa mtu. Mgomo uliendelea, ukimuathiri kila mtu, lakini wale waliodai haki zao hawakuvunja kani. ( Dunia Mti Mkavu-Saidi Ahmed Mohamed) MASWALI
Tanakali za Sauti: Kuwasiliana kwa Ufanisi kwa Kutumia Sauti PekeeMaelezo ya Tanakali za Sauti
Tanakali za sauti, au masimulizi ya sauti, ni aina ya mawasiliano ambayo hutumia sauti pekee bila kutumia picha au maandishi. Katika tanakali za sauti, hadithi au ujumbe huwasilishwa kupitia sauti na sauti za watu wanaoigiza. Hii inaruhusu hadhira kuvutiwa na kuelewa ujumbe kupitia mazungumzo, athari za sauti, na muziki. Tanakali za sauti zina historia ndefu, na zimekuwa maarufu katika redio, vipindi vya televisheni, na hata katika ulimwengu wa podcasting. Zinaweza kuwa na mifano mingi, kama vile hadithi za uhalifu, hadithi za kusisimua, makala za kielimu, na hata mafundisho ya lugha. Mara nyingi, tanakali za sauti zinahitaji maandalizi ya kutosha ili kuunda uzoefu wa kusikiliza wenye ubora. Hii inaweza kujumuisha kuandika hadithi au script, kuchagua sauti za watu wanaoigiza, kupanga athari za sauti, na kuchagua muziki unaofaa. Kwa kuongezea, mbinu za uigizaji na ubora wa sauti ni muhimu ili kuvutia na kushirikisha hadhira. Kuna faida kadhaa za kutumia tanakali za sauti. Kwanza, zinaruhusu hadhira kujenga picha za kujisikia na kufikiria mazingira na wahusika wa hadithi. Hii inaweza kuwa na athari ya kina na kusisimua, ikiruhusu hadhira kujenga uzoefu wa kipekee na wa kibinafsi. Pia, tanakali za sauti zinaweza kupatikana na kusikilizwa kwa urahisi, na kutoa nafasi kwa watu kufurahia hadithi au ujumbe wakati wowote na mahali popote, hata bila kuwa na ufikiaji wa picha au maandishi. Kwa kumalizia, tanakali za sauti ni njia nzuri ya mawasiliano ambayo hutumia sauti pekee. Zinaweza kuwa na mifano mbalimbali na zinahitaji maandalizi ya kutosha ili kuunda uzoefu wa kusikiliza wenye ubora. Tanakali za sauti zinatoa fursa ya kusisimua na kuunda picha za kujisikia katika akili za hadhira, na zinaweza kupatikana kwa urahisi na kusikilizwa mahali popote. Maswali
a) Taja na ueleze sifa za mtambaji bora katika fasihi simulizi. (alama 10)
b) Nyimbo zina wajibu gani katika jamii. (alama 4) c) i) Eleza maana ya vitendawili. (alama 2) ii) Onyesha sifa za kitendawili. (alama 4) Majibu
a) Sifa za mtambaji bora
b) Wajibu wa nyimbo
c)
i) Kitendawili ni fumbo/msemo wa kimafumbo ambao hufumbua jambo fulani na hutolewa kwa hadhira au wasikilizaji ili waufumbue. 1 x 2= 2 ii) Hutangulizwa kwa njia maalumu a) Ujumbe wake ni wa kimafumbo b) Ufananisho wa kijazanda c) Ni fupi kwa maelezo d) Hutegemea mazingira/sehemu Fulani 4 x 1 = 4 Maswali
a) Taja na ueleze aina nne za hadithi (alama 8)
b) Eleza mbinu tatu ambazo mtambaji anaweza kutumia kuishirikisha hadhira yake.(alama 6) c) Fafanua vipera vifuatavyo vya fasihi simulizi. (alama 6) i) Majigambo ii) Mivigha iii) Lakabu Majibu
a)
i) Visasili - Hadithi zinazosimulia asili ya watu, vitu ama tabia Fulani. ii) Ngano za mazimwi - Husimulia kuhusu mazimwi iii) Hurafa - Hadithi ambazo zina wahusika wanyama lakini waliopewa tabia za binadamu. iv) Hekaya - Ngano fupi zinazosimulia matukio ya kushangaza yanayoonyesha hila au ujanja wa mwanadamu v) Mighani - Ngano za ushujaa Mighani huwa na lengo la kueleza visa na mikasa ya watu ama mashujaa wa jamii fulani.( mwalimu akadirie aina nyingine)
b)
c)
i) Majigambo – Mazungumzo yanayotolewa na mtu fulani ili kujitapa ii) Mivigha – sherehe maalum za kitamaduni ambazo hufanywa na jamii katika kipindi maalum. iii) Lakabu – Majina ya utani au kupanga ambayo watu hujipa au kupewa
Soma maagizo yafuatayo kisha ujibu maswali
(Alfajiri kuu. Vijana wanazunguka kinu, vifua wazi. Nyusoni wamepakwa masizi na aina ya tope jeupe. Wako katikati yam situ. Mzee Jando ameketi kwenye namna yam to wa nyasi.)
Mzee Jando: (Akiwahiza) haraka! Ongezeni kasi! Zunguka! Haya imbeni, barobaro!
Vijana: jua lachomoza! Muda umefika wa mbegu kuatika! Ichipuke na kuzalisha matunda! Ni leo, ni sasa!
Mzee Jando: haya ketini sasa
Vijana: (Vijana wanaketi katika mistari huku wameshikana mikono mabegani) Mzee Jando: tulisema mume nini? Vijana: (kwa pamoja na kwa sauti ya dhati) Mume ni kazi Sio ubazazi Ale jasho lake
Mzee Jando: Sawa kabisa, je mume ni nani?
Vijana: Ni mlinzi wa jamii Ni mfano mwema wa jitihada Apambane na adui Atende wajibu na maadili
Mzee Jando: Jambo linalovunja umoja!
Vijana: Likumbatiwe na kufunzwa hata watoto wachanga! Mzee Jando: Haya, semeni wenyewe leo! Vijana: Leo tumkomaa, si watoto tena Tumetimia barobaro kamili Sisi ni stadi Sisi ni wapevu! Tayari kwa majukumu ya kujenga jamii Sisi ni tegemeo la umma Sisi ndio chimbuko la wema Maadili na upendo
Mzee Jando: Nakubali mko tayari. Haya tuendelee na ada zetu zingine. Kijembe kukidhihaki!
Vijana: (Wanasimama kijasiri na kurindimisha sauti) Tuko tayari kuingia utuuzima! maswali
majibu
“La, Mzee…. Mbio za sakafuni zimefika ukingoni” (al 4) (a) Eleza muktadha wa dondoo hili (b) Mbio zipi zimefika ukingoni? (al 4) (c) Fafanua maudhui mawili yanayojitokeza katika dondoo lenyewe. (al 4) (d) Taja mbinu za lugha zinazojitokeza hapa. (al 4) (a) Eleza muktadha wa dondoo hili (al 4) (i) Maneno ya Kenga (ii) Anamwambia Majoka (iii) Nje ya lango la soko la Chapakazi (iv) Baada ya Majoka kulalamika kuwa Kenga alikuwa ameshindwa kazi kwa kuwakubali wapinzani kufika pale sokoni. (b) Mbio zipi zimefika ukingoni? (al 8)
(c) Fafanua maudhui mawili yanayojitokeza katika dondoo lenyewe. (al. 4)
(d) Taja mbinu za lugha zinazojitokeza hapa? (al. 4)
Soma makala yafwatayo kisha ujibu maswali yafwatayo
Hapo zamani za kale, paloindokea mtu mmoja kwa jina mzee Kata. Mzee Kata alikuwa na wake wawili. Mke wa kwanza aliitwa Neema na wa pili aliitwa Nduli. Kila mmoja wa wake hawa alikuwa na mtoto mmoja. Neema alikuwa na mtoto wa kike kwa jina Majaliwa. Majaliwa alikuwa ameumbwa akaumbika.Uso wake ulihimili macho meupe mfano wa theluji. Meno yake ya juu yalipangika kwa njia ambayo iliyafanya kuacha mwanya ambao ulifanya tabasamu yake kuwa ya mvuto wa sumaki. Urembo wa Majaliwa, kama walivyosema wengi, ungemtoa nyoka yeyote pangoni.
Kwa upande mwingine Kutu, bintiye Nduli, alikuwa mwenye sura mbaya ya kutisha.Uso wake usiopendeza ulimfanya kuonekana kama ajuza wa miaka mia moja! Tabia yake ya ukorofi ilikoleza mvuto wake hasi. Vijana wa kijijini walimfanyia inadi kila mara kwa kumkumbusha kuwa hakufaa kuringa. “Sura kama kiboko”, wangemtania
Tofauti za kiumbo kati ya Majaliwa na Kutu zilizua uhasama mkubwa kati ya ndugu hawa, sikwambii mama zao. Hali hii ilizidishwa Zaidi na nongwa za kila siku zilizotokana na ukewenza. Familia yam zee Kata ikawa medaniya vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Hali ya mtafaruku iliendelea kuikosesha nyumba yam zee kata amani. Asubuhi moja, Mzee Kata aliamka kama kawaida yake, alijikohoza kama isharaya kutangaza kufika kwake. Daima hakupenda kuzungumza na wakeze asubuhi na mapema. Aliamini kuwa wangemletea nuksi. Kinyume na siku nyingine, mzee Kata hakuitikiwa. Ilibidi kujikaribisha nyumbani mwake. Mara tu alipovuka kizingiti cha kijumba hicho, alitupa macho yake juu yakitanda cha mayoweambapo mke wake alijinyosha twaa kakauka kama ukuni; hanapumzi. Weupe wa macho yake na mapovu yaliyomtoka kinywani yalimhakikishia Mzee Kata kuwa Neema kampungia mkono. Harufu kali ya sumu ilihanikiza hewa kumwarifu kuwa Mzee kata kuwa mkewe kafa kwa kutendwa na mkemwenza
Maisha ya Majaliwa yalichukua mkondo mpya baada ya tanzia hii. Mama wa kambo sasa alipata mwanya wa kumhini majaliwa. Kazi zote za nyumbani aliachiwa yeye.Huku Kutu akiachwa huru kucheza. Majaliwa alipewa chakula hapa; wengine wakila biriani yeye alipewa wali wa kawaida. Mavazi yake yaligeuka matambara.Siku zilivyozidi kusonga ndivyo mateso yalivyoongezeka. Mama wa kambo alizidisha wivu wake kwa majaliwa. Hata Majaliwa alipovunja ungo na wachumba kuja kumposa, mama wa kambo aliwafukuzia mbali. Wenine walihimizwa kumposa Kutu. Wachumba waliochachawa kutaka kumuoa majaliwa wakidai kuwa hawamtaki Kutu kwa sababu ya kiburi chake, walinyeshewa matusi, wakahizinika na kujiendea zao.
Siku moja alitokea kijana mmoja makini .alikuja amavalia gwanda jeusi lililojiinamia kwa uchovu. Viatu alivyovaa vilikuwa vimejichokea kwa kupiga lami. Kofia iliokuwa kichwani pake ilitosha kumhakikishia mama wa kambo kuwa huyu alikuwa fakiri. Mama mtu alikubali mara moja posa ya kijana huyu kwa Majaliwa akijua kuwa angeadhibika. Aliamini amemtokomeza Majaliwa ndani ya lindi la ulitima. Mzee Kata naye hakusita kumwoza Majaliwa kwa kiajana huyu maana aliiona hii kama fursa ya pekee ya kumwepusha vitimbi vya mama wa kambo Majaliwa aliandamana na mume wake hadi Kijiji cha peponi ambako kijana huyu allishi. Wallingia katika nyumba ya msonge ambamo Majaliwa alitarajia kuanza Maisha ya ndoa. Walitayarisha chajio, wakala na kulala.
Asubuhi, Majaliwa aliamshwa na nyimbo za ndege. Alipofunguamacho, alijikuta kalala ndani mya chumba chenye sakafu ya vigae. Ukuta wa chumba hicho ulikuwa wa rangi wa zari. Mapambo ya dhahabu yalitundkwa ukutani. Kumbe kijana aliyemuoa hakuwa maskini kama ilivyodhaniwa! Alikuwa mwana wa mfalme! Na hili lilikuwa kasri hasa! Majaliwa hakueza kuamini! Alikuwa ameamkia Maisha ambayo hakuwahi yawazia.
Alipoingia sebuleni alimpata mama yake mpenzi, akiwa na tabasamu ya milele usoni. Walikumbatiana kwa shauku kuu. Kumbe kijana huyo alikuwa ametumwa na mamake Majaliwa! Mumewe majaliwa alishuhudia kwa umbali. Machozi ya mama mtu na mwanawe yakilovya vifua vyao na kuyeyusha simanzi na kuyeyusha simanzi iliyokuwa imeyaandama Maisha yao. Tangu siku hiyi, watu hawa wallishi kwa raha mstarehe. Hadithi yangu inaishia hapo.
MASWALI
a) Taja na utolee mifano mbinu sita za kimtindo zilizotumiwa katika utungo huu (al.3)
b) Utungo huu unaweza kuainishwa kama ngamo, toa sababu (al.1) c) Fafanua umuhimu nne wa formula ya kumalizia katika utungo huu (al. 4) d) Taja shughuli moja ya kijamii katika jamii ya utungo huu (al. 1) e) Jadili tatizo moja la ukewenza katika utungo huu (al.1) f) Taja na ufafanue dhima tano ya utungo huu katika jamii yake (al.5) g) Taja mambo mawili ambayo fanani anaweza kutekeleza ili kuufanya utungo huu uwe wa kuvutia Zaidi (al. 1) h) Miviga ni nini? (al.1) i) Taja hasara tatu za miviga (al.3) MAJIBU
a) MBINU ZA KIMTINDO
i) Tashbihi -Sura kama kiboko ii) msemo/nahau -Kumtoa nyoka pangoni iii) Nidaa- Ajuza wa miaka mia moja iv) Taswira mnuso- Harufu v) Usimulizi- Hapo zamani za kale vi) Istiara- Mavazi kugeuka matambara vii) Majazi-Neema, Majaliwa, Nduli viii) Tashhisi- harufu kumwarifu ( 1/2x6= alama 3)
b) i) kuna formula ya ufunguzi- hapo zamani za kale
ii) kuna formula ya kumalizia- Hadithi yangu inaishia hapo (1x1=alama 1)
c) UMUHIMU WA FOMULA YA KUMALIZIA
i) Kurudisha wasikizaji kwa hali ya kawaida ii) Kubeba wazo au maudhui au ujumbe wa hadithi iii) Onyesha mwisho wa hadithi iv) Pahsa mtambali anayefuata. Pisha shughuli inayofuata v) Kitulizo kwa hadhira baada ya kumakinika kwa muda vi) Kutoa changamotomkwa hadhira. (4x1=alama 4)
D SHUGHULI ZA KIJAMII
i) Ndoa- Wake wawili, Nduli kukosa kupashashwa, Majaliwa kuolewa 1x1= alama 1
E MATATIZO YA UKEWENZA
i) Wivu- mamake majaliwa kupewa sumu ii) Mateso kwa wana wa wake wenza- majaliwa kuteswa na mamake Nduli (1x1= alama 1)
F DHIMA YA UTUNGO
i) Huelimisha ii) Huburudisha iii) Huadilisha iv) Hukuza utamaduni v) huleta utangamano vi) Hukuza ubunifu vii) Hukuza uwezo wa kukumbusha viii) Hutoa onyo ix) Ni kitambulisho cha jamii x) Hukuza ujasiri xi)Hukuza historia (5x1=alama 5) mwanafunzi atoe maelezo Zaidi ndiposa apewe
G) MAMBO YA KUFANYA HADITHI KUVUTIA
i) Kutumia Ishara kama miondoko ii) Kutumia ala za muziki iii) kutumia maleba iv) Kushirikisha hadhira v) kuimba vi) Kucheka (2x1/2=alama 1)
H) MIVIGA- sherehe za kitamaduni ambazo hufanywa na jamii katika kipindi au wakati maalumu wa mwaka (1x1=alama 1)
I) HASARA ZA MIVIGA
ii) Zingine zimepitwa na wakati kama vile tohara ya wanawake. Huhatarisha Maisha ya waathiriwa ii) Zingine hukinzana na malengo ya taifa kama vile ukeketaji wa Watoto wa kike iii) Zingine hujaza watu hofu kama zile zinazotumia kafara ya binadamu iv) zingine huleta uhasama kati ya koo hasa zile za kufukuza mapepo v) Zingine ni ghali kwani huhitaji fedha nyingi na kusababisha umaskini (3x1=alama 3) b) Fafanua majukumu yoyote manne ya nyimbo katika jamii. (Al 8)Fafanua majukumu yoyote manne ya nyimbo katika jamii. (Al 8)
Nyumbani mwetu mna papai lilioiva lakini siwezi kulichuma – ndugu wa kiume asimuoe nduguye wa kike24/12/2022 Tumia kifungu kifuatacho kujibu maswali yanayofuataa) Nyumbani mwetu mna papai lilioiva lakini siwezi kulichuma – ndugu wa kiume asimuoe nduguye wa kike.I) Bainisha kipera kinachorejelewa (Al 1).
Kitendawili
II) Andika shughuli moja ya Kijamii na moja ya Kiuchumi ambazo huendelezwa katika jamii ya utingo huu. (Al 2)
III) Eleza dhima nne za kipera kinachorejelewa katika jamii yako. (Al 4)
Umuhimu
IV) Wewe ni mwasilishaji wa kipera hiki jukwani. Eleza mambo matano ambayo utazingatia katika uwasilishaji wako. (Al 5)
Eleza umuhimu wa ukusanyaji na uhifadhi wa data za fasihi simulizi. (alama 5)
Fafanua matatizo yanayomkabili mkusanyaji wa fasihi simulizi nyanjani. (alama 10)
Eleza jinsi jamii ya kisasa inavyojaribu kuendeleza fasihi simulizi. (alama 5)Jinsi jamii ya kisasa inavyojaribu kuendeleza fasihi simulizi
Eleza sifa nne za maapizo. (alama 4)
Tofautisha istilahi zifuatazo za Fasihi Simulizi. (alama 3)Matambiko Sadaka au ada inayotolewa kwa Mungu, mizimu, pepo au miungu ili wasaidie binadamu kutatua mambo magumu, kuomba radhi au kutoa shukrani. Matatizo ni kama vile ukame, magonjwa, kukosa watoto, mafuriko au janga lolote lililomshinda binadamu nguvu na uwezo. Pembezi Tungo za sifa za watu wa aina fulani wanaosifika kwa matendo yao au nafasi walizo nazo katika jamii kv matendo ya kishujaa au kujitolea kwao. Km viongozi, walezi wazuri, waganga, nk Misimu
Semi zinazozuka na kutumiwa na kundi fulani la wanajamii kama misemo ya mawasiliano baina ya wanakikundi hicho./ Ni semi za muda na mahali maalum ambazo huzuka tu kutegemea mazingira maalum./ Ni semi ndogo ndogo za kupita. Huzuka katika mazingira fulani na hufa baada ya kutokuwepo kwa mazingira yale. Jadili hatua tano zinazofuatwa wakati wa utafiti. (alama 5)Jadili hatua tano zinazofuatwa wakati wa utafiti. (alama 5)
Fafanua hasara zozote nne za miviga. (alama 4)Fafanua hasara zozote nne za miviga. (alama 4)
Jadili sifa zozote nne za mtambaji bora. (alama 4)Jadili sifa zozote nne za mtambaji bora. (alama 4)
Eleza tofauti kati ya vitendawili na methali. (Alama 5)Eleza tofauti kati ya vitendawili na methali. (Alama 5)
Jadili mifano mitano ya ngomezi za kisasa (alama 5) Jadili mifano mitano ya ngomeziza kisasa. (alama 5)
Eleza maana ya; (alama 5) |
Categories
All
Archives
July 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|