Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
UFUPISHO (Alama 15)Vipindi mbalimbali vya historia vimeshuhudia kuibuka kwa magonjwa ya ajabu. Magonjwa hayo yamewahangaisha watu na kuzishughulisha bongo za wanasayansi na madaktari katika kutafuta tiba. Magonjwa kama vile tauni, kifua kikuu, homa ya matumbo na ndui ni baadhi ya yale yaliyotisha sana nyakati fulani za historia ya binadamu. Magonjwa haya yaliwauwa maelfu ya watu na kuibua mifumo na taratibu za maisha ya watu. Hata hivyo , magonjwa hayo yaliweza kuchunguzwa na kutafutiwa tiba kabla ya kumaliza kabisa kizazi cha binadamu. Lakini hii ni baada ya kuwasukuma maelfu ya watu kaburini. Ulimwengu wa sasa unashuhudia janga jingine la maradhi sugu ya ukimwi. Neno ‘UKIMWI’ lilitolewa kutokana na athari za ugonjwa huo mwilini. Neno “UKIMWI” humaanisha ukosefu wa kinga mwilini, ambapo herufi za kwanza za maneno matatu ziliunganishwa pamoja na kuunda neno hilo. Ugonjwa huu ambao tayari umewaua mamilioni ya watu kote ulimwenguni unazidi kuenea kwa kasi, mfano wa moto katika kicheka. Kutokana na kasi yake ya kuua watu, ugonjwa wa UKIMWI umepewa majina kama vile “umeme” na pia “ugonjwa wa vijana”. Watu wengi wanaoambukizwa virusi vya UKIMWI ni wale walio na miaka kati ya 15 hadi 49. Kundi hili kwa kweli ndilo linalohesabiwa kuwa na nguvu za kutunza jamii kwa njia nyingi. Iwapo wengi katika kundi hili watakumbwa na maradhi haya, watasalia wakongwe na watoto wachanga wasioweza kujimudu. Nchini Kenya, UKIMWI uligunduliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka wa 1984. Kufikia mwezi wa Juni 1996, inakisiwa kuwa ugonjwa huu ulikuwa umewaua watu wapatao 65,647 nchini. Hivi sasa, inasemekana kuwa takribani watu zaidi ya 500 hufa kila siku nchini Kenya kutokana na janga hili. Aidha, imedhibitishwa kwamba takriban watu milioni mbili unusu tayari watapoteza maisha yao kutokana na kuaambukizwa virusi vya ugonjwa huu humu nchini. Maradhi haya sasa yamekuwa janga la kitaifa. Kutokana na kuongezeka kwa visa vya UKIMWI, hospitali na zahanati nyingi kote nchini zinashindwa kukidhi mahitaji ya wagonjwa. Kwa hivyo, makundi ya kujitolea na mashirika mbalimbali yameundwa ili kuwahudumia wagonjwa wa UKIMWI. Baadhi ya makundi hayo hutoa tiba ya kisaikolojia pamoja na kuwapa ushauri wa hima ya kuishi, badala ya kukata tamaa. Wagonjwa wengi pia huishia kutibiwa nyumbani kwao. Ugonjwa huu umeathiri jamii kwa njia nyingi. Hali ya maisha na woga, ukosefu wa matumaini, ongezeko la mayatima na kuzorota kwa uchumi kutokana na kutoweka kwa kizazi chenye nguvu za kutoa huduma kwa jamii, na baadhi ya athari za maradhi haya. Lakini jambo la kuzingatia ni hili, tujifunze kutokana na historia.Tuwe na matumaini kwamba siku moja, tiba ya ugonjwa huu itapatikana. Hii ni kwa sababu tumethibitishiwa haya kutoka katika historia yetu wenyewe. Ikiwa magonjwa yaliyosababisha vifo vya wengi kutokana na ukosefu wa tiba yalitokomezwa kupitia juhudi za kimatibabu, sembuse huu ugonjwa tulio nao sasa? Huku tukijikinga kutokana na maradhi haya, tusife moyo bali tuwe na matumaini kwani subira hufuta heri. a) Kwa kutumia maneno yako mwenyewe na bila kupoteza maana, fupisha aya nne za mwanzo (maneno 90 - 100) (alama 3 kwa mtiririko) (alama 12 ) Nakala chafu/maadalizi ……………………………………… Jibu ……………………………………………………………… b) Eleza mambo yanayoleta matumaini kwa wagonjwa wa ukimwi kulingana na aya tatu za mwisho (maneno 40- 45) (alama 1 kwa mtiririko) Nakala chafu …………………………………………………… Nakala Safi ………………………………………………………………… MWONGOZO
UFUPISHO a) i) Vipindi mbalimbali vya historia vimeshuhudia kuibuka kwa magonjwa ya ajabu- tauni, kifua kikuu, homa ya matumbo n.k. ii) Magonjwa haya yamewahangaisha watu na kuzishughulisha bongo za wanasayansi na madaktari katika kutafuta tiba. iii) Magonjwa haya yaliwaua maelfu ya watu na kutibua mifumo na taratibu za maisha ya watu / yaliwaua watu wengi. iv) Magonjwa hayo yaliweza kuchunguzwa na kutafutiwa tiba. v) Ulimwengu wa sasa unashuhudia janga jingine la maradhi sugu ya ukimwi. vi) Ukimwi unazidi kuenea kwa kasi. Umewaua mamilioni ya watu kote ulimwenguni. vii) Ukimwi unazidi kuenea kwa kasi ulimwengu (lazima wazo la kazi litokee). viii) Wengi wa walioambukizwa ni kati ya miaka 15 – 49 ix) Kundi hili lina nguvu / linatunza jamii / wanaosalia ni watoto na wakongwe wanaoachwa. x) Ukimwi uligunduliwa Kenya mwaka wa 1984 (lazima ataje Kenya). xi) Watu zaidi ya 500 hufa kila siku xii) Ukimwi sasa ni janga la kitaifa. b i) Mashirika na makundi ya kujitolea kuwahudumia wagonjwa ii) Makundi hutoa tiba ya kisaikolojia na kuwapa ushauri na hima ya kuishi badala ya kukata tamaa. iii) Wengi hutibiwa nyumbani kwao. iv) Matumaini ya tiba kutokea.
0 Comments
Leave a Reply. |
Categories
All
Archives
June 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|