Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
SWALI LA PILI – UFUPISHO Soma taarifa ifuatayo kisha ufupishe taarifa hii kulingana na maswali yanayofuata. Katika kipindi cha mwongo mmoja, tumeshuhudia mabadiliko na maendeleo makubwa kuhusu vyombo vya habari nchini Kenya. Hapo awali, radio ndicho chombo cha habari cha kipekee kilichotamalaki kote nchini. Familia nyingi ziliweza kumiliki chombo hiki. Runinga ilikuwa miliki ya wachache, hasa mabwenyenye. Sasa hivi, hata akina yahe nchini na mashambani wanamiliki chombo hiki. Runinga kama kifaa kingine chochote cha mawasiliano kina manufaa yake. Kwanza kabisa, ni nyenzo mwafaka ya kufundishia. Vipindi vinavyopeperushwa katika runinga huwa na mafunzo kemkem kwa mtu wa kila rika. Halikadhalika, runinga huweza kuleta vipindi ambavyo huwafahamisha watu mambo yanayoendelea katika mazingara yao ya duniani. Aidha, runinga ikitumika pamoja na michezo ya video huauni katika ukuzaji na ustawishaji wa staidi ya kufundisha au kujielimisha. Michezo ya video, hasa kielimu, huwafanya watu kujenga umakini pamoja na kuchua misuli ya ubongo na kuwafanya watu kuwa macho wanapofanya kazi. Fauka ya hayo, televisheni ni chemichemi bora ya kutumbuiza na kuchangamsha. Hakuna mtu asiyependa kuchangamshwa au kuburudishwa. Televisheni ni mojawapo wa vyombo mwafaka vya kutekeleza hayo kutokana na vipindi vyake. Uburudishaji huu huwa ni liwazo kutokana na shinikizo na migogoro tunayokabiliana nayo kila siku. Uburudishaji huu hupatikana kwa urahisi majumbani mwetu. Kwa upande mwingine, hakuna kizuri kisichokuwa na dosari. Licha ya manufaa yake, televisheni imedhihirika kuwa na udhaifu wake. Kwanza, baadhi ya vipindi vya runinga na video hujumuisha ujumbe usiokuwa na maadili , kama vile matumizi ya nguvu za mabavu, ngono za kiholela, lugha isiyo ya adabu, ubaya wa kimavazi na maonevu ya rangi, dini jinsia , kabila na utamaduni. Si ajabu kuwa baadhi ya vijana wetu wanaiga baadhi ya mambo haya. Vijana wetu siku hizi wameingilia ulevi wa pombe na afyuni, ngono za mapema kabla ya ndoa na mavazi yanayowaacha takribani uchi wa mnyama. Wengi wamekopa na kuyaiga haya kutoka kwa runinga. Ukiwauliza wafanyacho, watakujibu kuwa ni ustaarabu kwani wameupata katika runinga. Mtumizi ya runinga na michezo ya video yasiyodhibitiwa huweza kuwa kikwazo cha mawasiliano bora miongoni mwa familia. Matumizi kama haya huwapa wanafamilia fursa ya kujijenga. Imedhihirika kuwa runinga haichangii kujenga uhusiano bora wa kijamii. Ukilinganisha na vyombo vingine vya burudani ambavyo hutoa nafasi ya watu kutangamana na kujenga uhusiano bora, televisheni haichangii haya. Badala yake, tajriba ya televisheni huwa na kibinafsi. Hali hii inapotokea katika kiwango cha familia, televisheni inaweza kutenganisha wazazi na watoto wao. Hali kadhalika, runinga na video aghalabu hueneza maadili yasiyofaa. Mathalani, baadhi ya vipindi vya televisheni huendeleza hulka ya kuhadaa, ngono za kiholela, kuvunjika kwa ndoa n.k. Hulka hizi zisizoendeleza maadili ya kijamii huchukuliwa kama zinazofaa na zinazofuatwa na waliostaaribika. Huu ni upotovu. Isitoshe, baadhi ya matangazo huhimiza matumizi ya madawa ya kulevya kama tembo na sigara.Vitu hivi vinavyotangazwa, hupambwa kwa hila na udanganyifu mwingi ambao huwavutia vijana na watoto wengi. Si ajabu mtu anapouliza wanaotumia vileo hivi walivyoanza, watajibu kutokana na athari za matangazo katika runinga na vyombo vingine. Utafiti umeonyesha kuwa vipindi vya runinga na video ni chanzo cha matumizi ya nguvu za mabavu miongoni mwa wanafunzi. Wazazi wengi huchukulia vibonzo katika televisheni kuwa vinalenga kuburudisha tu na havina ubaya wowote. Lakini ukweli ni kuwa vipindi vingi vya vibonzo hushirikisha na matumizi ya hila na nguvu za mabavu. Haya huibusha hamu ya vijana na watoto huyaiga.. Kwa hivyo, ni muhimu wazazi na jamii kutambua madhara ya televisheni. Utambuzi huu utawafanya wawaelekeze vujana na watoto jinsi ya kutumia televisheni na video ili kuepakana na madhara yake. Maswali a) Ukitumia maneno 50-60, fupisha manufaa ya runinga. (alama8) Nakala chafu ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… Nakala safi ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… b) Fupisha hasara za runinga ukitumia maneno 70-80 (alama 7) Nakala chafu ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… Nakala safi ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… SEHEMU B: UFUPISHO a) Manufaa Hutumika kama nyenzo ya kufundishia Hufanya watu kuchua “misuli” ya kibongo na kufanya watu kuwa makini katika shughuli Hutumbuiza na kuchangamsha. Hii hupunguza gharama na wakati wa kuandama chemichemi nyingine za burudani. Huendeleza utamaduni, kaida na amali za jamii. Mengi yanayotokea katika runinga huwezi kuakisi mtazamo, mikakati amali za jamii. (alama2 kwa kila hoja na alama 2 kwa muwala) b) Hasara - Wakati mwingi huendeleza hulka ambazo huchukuliwa kama zinazofaa na zinazofuatwa na wastaarabu. Hivyo, vijana huziiga na kuzifuata. - Runinga huweza kuwa kikwazo cha mawasiliano miongoni mwa familia. Haya yanaweza kuwafanya baadhi ya wanafamilia kujitenga. Waliojitenga huwa rahisi kuingisha maovu. -Baadhi ya matangazo ya runinga hupotosha na kuwafanya watu kushiriki katika mambo hatari kama vile ulevi na kuvuta sigara. - Huwafanya watu kuiga tabia ya matumizi za nguvu za mabavu. (alama 2 kwa kila hoja na 2 kwa muwala)
0 Comments
Leave a Reply. |
Categories
All
Archives
July 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|