Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
UFUPISHO2. UFUPISHO Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali. Ukimwi ni ufupi wa ukosefu wa kinga mwilini. Uwele huu ni wa zinaa ambao hauna tiba, dawa wala kafara. Insi anaweza kupata wiche ya ukimwi kwa njia ainati. Mathalani ni; kujamiiana baina ya mwanamume na mwanamke japo wote au mmoja ana wiche ya virusi vya ukimwi. Nina aliyehimili anaweza kumtia wiche mtotowe akijifungua au kwa kumnyonyesha. Katika harakati na mikakati ya kutoa damu, au ngeu hiyo kuchangamana na jeraha nyevu. Cheche akilia mfiche kuku, ama fisi akimia mwele funga mlango. Tuupige ukimwi vita shadidi, kwani si lelemama. Tutahadharike kabla ya athari kwani hadi sasa hakuna tiba hususan, ya uwele huu. Tarakimu zinabainisha kwa kina kuwa vijana wengi ndio wanaoathirika. Wengi wao wamefufutika na kugugunwa wakabakia mifupa. Hali kama hii ikishitadi kujiradidi nchi hii yetu itakosa viongozi wa mustakabali. Wimbo mui hauongolewi mtoto. Wazazi wanafaa kuwa kielelezo chema kwa wana wao. Mwana akibebwa hutazama kisogo cha ninake. Ni jambo la fedheha na kukereketa mtima kuwaona baadhi ya wazee wakichana mtaani vipara moto. Vijana hutegwa kwa chachu na kunaswa kwa ulimbo. Pengine huingia mitegoni kwa ghiliba chache tu za pesa nane. Enyi vijana jihadharini! Wazee hawa ni vitaange watawatosa demani. Mila na tamaduni nyingine zimepitwa na wakati. Wala hazina nafasi katika dunia ya sasa. Tunafaa kutembea na wakati kwani tusipoukata utatukata. Swala la kuingia mafa wajane wafaruku limekita mizizi miongoni mwa makabila humu nchini. Hili ni swala nyeti linalohitaji kuvuliwa nguo livaliwe nduruga. Serikali sharti iingilie kati na kukata kauli kuukomesha uozo na uvundo wa namna hii. Ukata na uchochole umechangia pakubwa katika kuupalilia mbolea ukimwi. Kwa sababu ya uchechefu wa fulusi za karo, shababi wengi hawamudu kuendelea na masomo. Kitembo cha elimu hakikiuki elimu ya msingi. Zaidi, mwanamume wa kisasa ambaye bado amefungwa pingu na taasubi za kiume hapendezwi na hali hii na huuma kidole akitamani ya kale. Shingo upande analazimika kukubali kuwa mabadiliko ni jambo la aushi. Mla kunde hunya kunde. Vijana lazima watahadharishwe na malimwengu. Wasije kufa na laiti ningalijua, na chanda kili kinywani. Wengi wamezizika mila na tamaduni katika kaburi la sahau. Hawaoni hawasikii kwa sababu hawana ashiki. Wameuvua utu wakajivika uchu. Matongozi yamejaa tadabui tena, masikio yamejaa komango yasiweze kusikia. Ukimwi unawagegeda na kuwakeketa kama umwa. Utamu unapoisha wanatemwa na kutiwa mavani kama makapi. Wanafaa kuaswa waasike kwa maaso yenye adili. Ulimwengu kokwa ya fuu haiishi utamu, anayeisha ni binadamu. Maswali (a) Fupisha ujumbe unaojitokeza katika aya tano za kwanza za makala haya. [Maneno 50 – 60] [Alama 8,2 za utiririko] Matayarisho …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... Jibu …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... (b) Katika aya za sita na saba, mwandishi anawashauri waja. Toa nasaha hiyo. (Maneno 35 – 45 ) (Alama 7, 1 ya utiririko) Matayarisho …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... ……………………………………………………………………………………………………… Jibu …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... 2. UFUPISHO (a) UKIMWI – Ugonjwa wa zinaa usiokuwa na tiba Mama anaweza kumwambukiza mtoto, wakati wa kuzaa au kunyonyesha Damu ikichanganyika baina ya watu ni hatari Watu waepukane na UKIMWI kwa vile ni hatari Vijana waonywa dhidi ya wazee waasherati Mila zingine zimepitwa na wakati Serikali ina sera mbovu kuhusu mila Umaskini huchangia UKIMWI Ni wajibu wa serikali kupambana na janga hili Zozote 6 x 1 = 6 (b) Watu kuelimika/kuelimishwa waepukane na maafa Vijana waonywa kuepuka maovu Vijana waenzi mila za jamii zao; wasitupe tamaduni/desturi Watu watii wanayoambiwa na wakuu Kuzingatia maadili Kujiepusha na tamaa nyingi za ulimwengu Kuwa na utu – kutahadhari na UKIMWI Zozote 6 x 1 = 6
0 Comments
Leave a Reply. |
Categories
All
Archives
July 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|