Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
UFAHAMU1. UFAHAMU (ALAMA 15) Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali. Mtoto anapozaliwa huwa ni malaika wa Mungu, hutaraji kuongozwa kwa kila njia ili awe mwana mwelekea. Jukumu la kulea mtoto huanzia nyumbani. Wako baadhi ya watu ambao wanaamini kuwa jukumu hili muhimu hutekelezwa bora na mama; wengine husema ni jukumu la baba. Ni kweli kwamba mtoto huwa na mama yake kwa muda mrefu zaidi ya baba lakini kivuli cha baba hakikosi kumwandama na kumwathiri maisha yake. Uongozi wa mama huanzia siku ya mwanawe kuingia ulimwengu kwa hivyo, mama zaidi ya baba huwa ndiye chanzo cha chemichemi ya maisha ya mwanawe. Mtoto wa kawaida ana tabia ya kuiga kila jambo analoliona na kusikia na mambo ya awali ajifunzayo kutokana na mamaye. Je; mtoto huiga kutokana na mama pekee? Kila utamaduni hasa huku kwetu Afrika, una taratibu zake zilizopangwa kuhusu malezi ya watoto. Kwa mfano ; akina baba wengine wanaoishi maisha ya kijadi huonelea kwamba ni jukume lao kuwalea watoto wa kiume. Kwa hivyo mvulana anayekulia katika mazingira haya akishachuchuka kiasi cha kujua lipi zuri na lipi baya huanzia kuwa mtoto wa baba zaidi ya kuwa wa mama. Baba huathiri mtoto wake kwa kushauri kuhusu maneno ya kiada ya wanaume. Hupenda kukaa naye katika uga wake kwa kumshauri kuhusu maneno ya kiada ya wanaume huku akimkataza kukaa jikoni na kumsisitizia kuwa wanawake ni tofauti naye. Aidha, humfunza sifa kama vile ushujaa na uvumilivu kwa namna ambavyo huona kuwa ni ya kiume. Pindi mtoto anapoonyesha tabia za kikekike, baba hujiandaa kuzitadaruki kwa kumkaripia. Baba hutaka kujiona mwenyewe katika hulka ya mwanawe. Baba kama huyu humpa nafasi ndogo sana mkewe ya kumwongoza mtoto wake wa kiume kwa jambo lolote hata kama wakati mwingine ni la heri. Kwa upande mwingine baba huyu huwa na machache ya kuzungumza na bintiye kwa kuwa huona kuwa sistahili yake kufanya hivyo. Mtoto wa kike huachiwa mamake lakini kutokeapo jambo la kulipima mama huona linampita kimo, humwita baba kuingilia kati na angalabu baba naye humwagiza dadake aje atoe suluhisho mwafaka. Ulezi kama huu una nafasi yake katika jamii, lakini ni lazima tukiri kuwa pia unaendeleza maisha ya fawaishi na kuanzia taasubi ambayo hatima yake ni mwanamke kukandamizwa na mwanaume. Wazazi walio na mwelekeo huu katika malezi yao hufikiri kuwa wataishi na watoto wao katika mazingira finyu na kwa hivyo waendelee kuwapulizia pumzi za kuhilikisha. Lakini ni sharti wakumbuke kuwa wao si walezi peke yao na mtoto hawezi kuishi pekee yake na kuwa na tabia ya kipekee. Leo ataishi kwao lakini kesho itambidi atoke aone ulimwengu. Kila atakapotia mguu ataona mambo mapya yatakayompa tajriba mpya na mawazo mapya ambayo aghalabu yataendelea kuathiri hulka yake. Iwapo tabia alizopata kwa wazazi wake hapo awali zilikuwa na misingi isiyokuwa madhubuti na mielekeo finyu, zinaweza kuwa pingamizi katika maingiliano yake na watu wengine. Mambo haya yanatuelekeza katika kufikiri kwamba maisha ya sikuhizi hayaruhusu ugawaji wa kazi ya malezi ya namna baba na mama wa kijadi. Baba na mama ni walezi wa kwanza ambao kwa pamoja wanapaswa kuelekeza watoto wao katika maisha ya ulimwengu iliyojaa bughudha na ghuhuri. Ni lazima wazazi watambue tangu awali kuwa katika malezi hakuna cha ubaguzi. Hakuna, mambo ajifunzayo mtoto wa kiume ambayo hayamhusu mtoto wa kike. Uvumilivu, bidii, utiifu na kadhalika ni sifa zinazomwajibikia kila mtoto kama vile upishi, ukulima na usafi. Mwanamke tangu azali ameumbwa kuwa mama na haipasi kulazimishwa kuchagua baina ya mtoto wa kike na wa kiume. Mapenzi na wajibu wa wazazi yapaswa yasiwe na mipaka bali yawe maridhawa kwa watoto wote. Maswali (a) Toa kichwa mwafaka cha makala haya. (al.1) …………………………………………………………………………………………………..…… …..…………………………………………………………………………………………………… (b) Kulingana na kifungu hiki, taja mambo mawili ambayo yanaweza kuwa hatari kwa malezi ya watoto. (al.2) …………………………………………………………………………………………………..…… …..…………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………………………………..…… (c) Kwa nini baba humpa nafasi ndogo sana mkewe ya kumwongoza mtoto wa kiume katika jambo lolote hata kama wakati mwingine ni la heri. (al.2) …………………………………………………………………………………………………..…… …..…………………………………………………………………………………………………… (d) Eleza mambo mawili ambayo ni ya manufaa katika ulezi wa jadi. (al.2) …………………………………………………………………………………………………..…… …..…………………………………………………………………………………………………… (e) Kulingana na makala haya, ushahidi gani unaonyesha kwamba kutegemeana katika ulezi jadi? (al.3) …………………………………………………………………………………………………..…… …..…………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………………………………..…… …..…………………………………………………………………………………………………… (f) Taja sifa mbili ambazo baba humfundisha mwana wa kiume. (al.2) …………………………………………………………………………………………………..…… …..…………………………………………………………………………………………………… (g) Eleza maana ya maneno yafuatayo kama yalivyotumika katika kifungu hiki: (i) chanzo cha chemichemi… …..…………………………………………………………………………………………………… (ii) Akishachuchuka …………………………………………………………………………………………………..…… (iii) Hulka …………………………………………………………………………………………………..……
0 Comments
Leave a Reply. |
Categories
All
Archives
July 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|