Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
UFAHAMu 1. UFAHAMU Soma habari ifuatayo kisha ujibu maswali Tukilinganisha maisha ya zamani na ya siku hizi tutaona kwamba mambo mengi sana yamebadilika. Si watu wazima, si watoto; sote tumeathirika si haba. Mitindo mipya ya kimaisha na mazingira yanayobadilika kasi ni baadhi tu ya mageuzi haya. Sio katika mavazi, lugha, mienendo, mitizamo, mawazo na mielekeo tu bali katika vipengele vingi vingine. Mavazi ya zama hizo yalikuwa yakitengenezwa kutokana na maganda ya mti au ngozi za wanyama kama vile mbuzi, kondoo, punda, ngamia, ng’ombe na hata pengine wanyama wa mwituni. Kwa vile kila mtu alifuga wanyama wengi, hakukuwa na shida ya kuzipata ngozi kama hizo wakati wowote ule haja itokeapo. Magome ya miti yalipatikana mwituni – na kwa kuwa katika enzi hizo hakukuwa na hifadhi za wanyama wa mwitu wala miitu yenyewe, watu waliweza kuingia katika pori lolote na kubambua maganda au kuua wanyama kama walivyohitaji. Mavazi yalikuwa rahisi kupatikana kuliko zama zetu; licha kwa upande wa ndarama, hata kwa upande wa sheria pia. Zaidi, katika enzi hizo watu hawakujali kwenda uchi au walipachika kipande tu cha vazi mwilini. Siku hizi gharama ya maisha imepanda mno. Siku hizi hatuwezi kuwaua wanyama wa mwituni vururu mtende eti kwa chakula, kama walivyofanya babu zetu. Enzi hizo matunda yalining’inia mitini na njaa zilikuwa si nyingi. Chakula kilikuwa bwerere zaidi ya leo. Vinywaji vilikuwa kwa mpango – wazee wa ngambi walikuwa na vinywaji vyao; wazee wa kawaida, wanawake na watoto hirimu hawakusahauliwa. Watu waliheshimiana; vijana walikuwa wenye adabu na walifahamu fika kuwa walipaswa kuwaheshimu wakubwa kwa vyovyote vile. Siku hizi vyakula ni haba na ghali na vingi vyazua magonjwa tata. Siku hizi kuna weledi wengi, hasa wa sayansi. Mja akitaka kwenda safarini huchukua kidubwasha fulani na huyoo! Kaenda zake; barabarani, angani au hata katikati ya kilindi cha bahari. Leo twajivunia ujuzi na maendeleo ya kiafya na madawa yapunguzayo mno unyofu wa binadamu lakini bado kuna pengo kubwa kati ya vikongwe na watu wa makamo, kinyume na zama hizo. Maisha ya karne hii yamekuwa kama zile nguo ziitwazo“bwaga – mtwae’’, ambazo hazibali kufumka au kukwajuka. Hivi leo, mtu akiumwa na kichwa hukimbilia kwa daktari. Mwingine akiumwa na nyoka popote pale, hukimbilia hospitalini akapate sindano ambayo hata jina lake halijui. Zamani ilikuwa mtu achimbechimbe mizizi ya upuzi upuzi, aitafune na alipata nafuu! Wa kisasa twawapuuza wa kale eti hawakujua elimu ya usafi tuijuavyo sisi, ilhali walikuwa wakiichoma miili ya watu waliokuwa wamekufa kwa ukoma au kifua kikuu. Wakati mwingine walikihama kijiji kilichoingiliwa na maafa ya ndui. Hata sasa wagonjwa kama hao hutengwa hospitalini huku maradhi kama vile UKIMWI bado yakikosa tiba. Mengi tuliyonayo sasa, mathalan tarakilishi na eropleni yalivumbuliwa au kugunduliwa na hao wa zamani. Fanaka zetu zote na ustawi tulionao asili yake ni watu hao wa zamani. Akili ni mali na kila mtu ana zake. Kuongezeka kwa watu duniani, mchanganyiko au matumizi mabaya ya madawa mengi pamoja na uchafuzi wa hali ya anga pia yameongezea kuleta hasara kubwa. Kweli sikio haliwezi kushinda kichwa. (a) Kulingana na mwandishi, kwa nini maisha ya kale na ya sasa hayalingani? (alama 3) .......................................................................................................................................................................................................................................................................................................................... .......................................................................................................................................................................................................................................................................................................................... (b) Kupata mavazi zama zile kulikuwa nafuu. Toa sababu. (alama 2) .......................................................................................................................................................................................................................................................................................................................... (c) Kwa kusema siku hizo, ’chakula kilikuwa bwerere zaidi ya leo,’ mwandishi anamaanisha nini? (alama 2) .......................................................................................................................................................................................................................................................................................................................... (d) Taja sababu za magonjwa na maafa kukithiri siku hizi licha ya hatua kubwa katika elimu na afya. (alama 3) .......................................................................................................................................................................................................................................................................................................................... .......................................................................................................................................................................................................................................................................................................................... (e) Fafanua usemi, ’sikio haliwezi kupita kichwa’ kwa mujibu wa taarifa. (alama 2) (f) Eleza maana ya: (i) Magome – (ii) Vururu mtende – (iii) Hazibali - (alama 3) 1. UFAHAMU (a) Mabadiliko ya maisha/athari za kigeni/mitindo mipya ya kimaisha;, mavazi, chakula, afya nk. Mazingira yanayobadilika – Sheria zinabadilika Teknolojia, tarakilishi nk. Zozote 3 x 1 = 3 (b) Wanyama walifugwa kwa wingi Misitu ilikuwa kocho Watu walikuwa huru hata kuwinda na kukata miti Zozote 2 x 1 = 2 (c) Chakula kilipatikana kwa urahisi mno na bila malipo au gharama kubwa. 1 x 2 = 2 (d) Idadi kubwa/kuongezeka kwa watu duniani Mazingira yanayobadilika mara kwa mara Mchanganyiko au matumizi ya madawa mengi pamoja Uchafuzi wa hali ya anga Zozote 3 x 1 = 3 (e) Vijana si sawa na wazee; watu wazima wana hekima, busara na tajriba ya maisha Watu wa siku hizi hawawashindi wa zamani kimaisha 2 x 1 = 2 (f) (i) Maganda ya miti (ii) Ovyo ovyo bila woga au vikwazo (iii) Hazikawii; hazichukui muda ; hazihimili 3 x 1 = 3
0 Comments
Leave a Reply. |
Categories
All
Archives
July 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|