Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
SWALI LA KWANZA – UFAHAMU Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali. Zamani wanadamu wa kwanza ambao ni mababu wa vizazi vilivyopita waliishi duniani. Habari kuhusu maisha na maumbile yao haikujulikana kwa hakika kwa sababu hawakuwa na uwezo wa kuandika. Lakini mara kwa mara shughuli za wanakioolojia kama Louis Leakey na wengine hugundua mifupa yao ardhini na michoro yao katika mapango. Wataalamu hawa hufukua mafuvu, vyombo na silaha zao za zamani. Kwa kuchunguza vitu hivi tunaweza kubahatisha viumbe hawa walivyokuwa na jinsi walivyoishi. Moja ya mambo yanayofahamika sasa ni kuwa wanadamu hawa wa awali walifanana na Sokwe. Aidha , walitembea kwa kupinda mgongo kama kibiongo. Chakula au uhai wao ulitegemea kukusanya matunda, kokwe, majani ya miti na mayai ya ndege. Vile vile , walitegemea wanyama wadogo, kufukua mizizi na kubambua magamba ya miti walipokabwa na njaa. Maisha yao yalikuwa ya hatari . Walikuwa wakiwindwa na wanyama wakubwa. Hii ni kwa sababu mwanzoni hawakuwa na silaha za kujihami. Hivyo iliwabidi kujificha katika miti na vilima kuepuka uvamizi. Lakini usalama wao ulitegemea kwa kiasi kikubwa kudura za Mungu au pengine miungu. Kwa taratibu wanadamu hawa walijifunza kutengeneza silaha. Walianza kutumia fimbo nene zenye ncha au mawe ya kutupia. Baadaye walichonga mawe ili kufanya kuwa visu, nyundo au vigumba vya mikuki. Hatimaye waliviomoa au kupasua vipande vya mawe na kuvitumia kama mishale. Hapa ndipo walianza kuwinda wanyama wakubwa mithili ya swara nguruwe nyati na ngiri. Pia walioweza kutumia mikuki kundunga samaki majini. Mababu zetu hawakuwa na nyumba . Kwanza walikuwa wakijisitiri kwa kukaa chini ya vivuli vya miti au kujenga vibanda vya matawi na majani ya miti. Hawakuweza kuingia mapangoni asilani kwa kuchelewa wanyama wapori wakali kama vile chatu , simba na mamba waliokaa humo. Kwa bahati, siku moja mmoja wao aligundua moto alipokuwa akipekecha vijiti. Kabla ya ugunduzi huu, wao pia hawakujua kazi ya moto na walikuwa wakiogopa na kukimbia moto jinsi wafanyavyo wanyama wa mbugani mpaka leo. Ujuzi wao wa kutumia moto ulileta mabadiliko makubwa. Baada ya hapo waliweza kukaa mapangoni na kukoka mioto milangoni mwa mapango ili kuaogofya adui. Hali kadhalika, waliweza kuota moto, Kumilikia maskani yao mpya na kuchoma nyama badala ya kuila mbichi. Wanadamu wa awali hawakuwa na mavazi. Waliwezaje kuzuia baridi? Inadhaniwa kwamba nywele nyingi walizokuwa nazo kwenye mwili zilisaidia kuwapa joto. Uvaaji wa nguo ulianza walipoanza kutumia ngozi kutoka kwa wanyama waliowawinda. Walizisafisha ngozi kwa kuzipaa kwa kombe za mawe kuzianika juani. Zilipokauka walizivaa kwa kujifunga na kuzishikanisha kwa mifupa au mikanda ya ngozi. Wanadamu hawa hakuweza hata kuongea. Waliwasiliana kwa kupiga mayowe, Kutoa milio au kunguruma jinsi wafanyavyo wanyama. Polepole walianza kutumia sauti na baada ya muda walizipanga sauti kuibua mifumo ya maneno yenye maana za kipekee. Uimilisi wa kutumia lugha uliwawezesha kupiga hatua kubwa kimaendeleo. Lugha pamoja na matumizi ya moto na silaha viliwarahisishia maisha na kuwawezesha kupata muda wa kupumzika mapangoni jioni wakiota moto. Kutokana na hali hii waliweza kutekeleza jambo moja kuu waliloturidhisha. Walitupokeza zinaa.Kutoka kwao tulirithi fasihi simulizi na kupata nakshi za michoro hii inapatikana katika mapango hata leo hii nchini Ufaransa , Uhispania, Africa kusini na hataAfrika mashariki. Maswali a) Msemo “kudura za Mungu au pengine miungu” inadhihirisha hali gani ya wanadamu wa kwanza. (alama 2) ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… b) Kwa nini wanadamu hawakuishi mapangoni mwanzoni? (alama 2) ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… c) Fafanua mambo matatu yaliyomwezesha mwanadamu wa kwanza kupiga hatua kimaendeleo. (alama 6) ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… d) Taja sifa mbili za kimaumbile zilizowatofautisha wanadamu wa awali na wa siku hizi. (alama 2) …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… Eleza maana ya (alama 3) (i)Walipokabwa………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… (ii) Kijihami……………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………………… (iii) Maskani…………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………………… SEHEMU A: UFAHAMU 1. a) Hawakuweza kujikinga na haieleweki walivyookoka uvamizi b) Wanyama hatari waliishi humo c) (i) Uwezo wa kutumia silaha kujikinga na kupata chakula (ii) Uvumbuzi wa moto ulimwezesha kuishi pangoni d) (i) Walitembea kwa kuinama (ii) Walikuwa na nywele nyingi mwilini e) (i) Walipohisi, walipoona, walipokumbwa (ii) Kujitetea, kujilinda (iii) Makaazi, makao, nyumbani
0 Comments
Leave a Reply. |
Categories
All
Archives
July 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|