Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
1. UFAHAMU (ALAMA 15) Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yanoyofuatia. Malengo ya maendeleo ya Milenia Malengo ya maendeleo ya Milenia (yajulikanayo kwa kimombo kama Millenium Development Goals (MDG), Ni malengo manane ya nchi wanachama wa umoja wa mataifa, ambayo nchi hizi zilikubaliana kujitahidi kutimiza kufikia mwaka wa 2015.Azma ya kufikia malengo haya ilizinduliwa rasmi mnamo septemba 2000 katika azimio la millennia la umoja wa mataifa.Wakati wa uzinduzi, mataifa yote 189 wanachama wa umoja wa mataifa yalihusika.Kwa sasa, mataifa wanachama yameongezeka na kufikia 193 na yote yanajizatiti kutekeleza azma hii. Azma ya kwanza ni kukomeza au kupunguza umaskini uliokithiri kwa asili 50 miongoni mwa watu ambao kipato chao ni chini ya dola moja kwa siku.Aidha lazima hii inalenga kupunguza kwa kiasi hicho idadi ya watu wanaokumbwa na dhiki ya njaa kufikia mwaka wa 2015.Kwa kielelezo, kwa mfano vijiji viitwavyo ‘vijiji vya milenia’vilianzishwa katika nchi sahara,ambazo ni Uhabeshi, Ghana, Kenya, Malawi, Rwanda, Nigeria, Senegal, Tanzania na Uganda vilichaguliwa.Wakazi hawa wanapookolewa kutoka kwa ulitima, hatua zilichukuliwa vijijini humu yanaonyesha athari chanya.Kunayo matumaini. Lengo la pili lilikuwa kutimiza elimu ya msingi kwa wote chini ya wito ‘Elimu kwa wote’, yaani kwa kingereza Eduction for All (EFA) kufika mwaka wa 2015.Nchini Kenya, elimu ya msingi ilifafanuliwa upya katika katiba mpya ya 2010, ikawa yaanzia shule ya chekechea hadi kidato cha nne. Aidha imetajwa kuwa ya lazima, kwamba mtoto sharti ahudhurie masomo.Ina maana kuwa mzazi analazimika kumpeleka mtoto shuleni. Lengo pia lipo, kuhakikisha watoto wote wa jinsia za kike na kiume wanahitimu. Lengo jingine ni kuwania usawa wa kijinsia kwa kuhakikisha kuna nafasi sawa kwa wote.Katika janibu nyingi za wanachama wa umoja wa mataifa, wanawake kwa miaka ya ayami walionekana kuwa chini ya wanaume kutokana na taasubi ya kiume, mwanamke alifaa kuwa chini ya mwanamume.Hatua ya kwanza ya malengo ya maendeleo ya millennia inanuia kuondoa tofauti ya uwiano wa wasichana na wavulana katika elimu ya msingi hadi sekondari ifikapo mwaka 2005; na katika ngazi zote za elimu ifikapo 2015. Kuondoa utoro miongoni mwa wahudhuriao masomoni hutahakikisha usawa huu. Lengo la nne ni kupuuza vifo vya Watoto wa umri chini ya miaka mitano kwa theluthi mbili kufikia mwaka wa 2015. Jitihada zinatiwa kuhakikisha kuwa kina mama waja wazito hawazai njiti wala watoto wao hawaagi punde baada ya kuzaliwa.Changamoto imekuwa kwamba watoto wengi katika nchi zinazoendelea hufa kabla kufikia umri wa miaka mitano. Mapambano dhidi ya magonjwa kama vile kifaduro, polia na malaria yaliyosababisha vifo hivi pamoja na jitihada za kujizatiti za kufikia lengo hili. Kunayo azma ya kuhakikisha upatikanaji wa huduma bora za uzi ili kupunguza kwa robo tatu vifo vya uzazi kufikia 2015. Kua kwa wajawazito kunaashiria huduma duni wakati wa kuhimili.Kina mama wengine katika nchi zinazoendelea hawahudhurii kliniki wakati wakati wa kulea mimba.Kwingineko, huduma hizi huwa mbali sana, huku namna za usafiri zikiwa duni.Kina mama huishia ama kuhudumiwa na ‘wakunga’ wasiohitimu au hata kujifungua pweke .Mataifa wanachama wanahimiza kuongezea zahanati na vituo vingine muhimu vya afya.Kadhalika jitihada zinatiwa kuwaelimisha kina mama na jamii kwa jumla kuhusu umuhimu wa kuhudhuria kliniki wakatiwa ujauzito na kuhakikisha mama yu salama wakati wa kujifungua. Magonjwa sugu yanayotishia kuwamaliza walimwengu ni kikwazo cha jitihada za walimwengu kujiendeleza.Ndiyo maana lengo la sita ni kupambana na Ukimwi, malaria na magonjwa mengineyo.Kampeni zinaimarishwa katika jumuiya hii kuzuia kabisa na kupunguza maambukizo mapya ya Ukimwi.Jitihada zinatiwa kupunguza au kuzuia kabisa ugonjwa wa malaria au magonjwa mengine hatari. Vyombo vya habari, vituo tamba vilivyo na maafisa wa nyanjani vinatumiwa nyanjani katika mataifa wanachama ili kufaulisha kampeni hii. Aidha wanachama wanalenga kuhifadhi mazingira kwa kujumuisha misingi ya maendeleo endelevu katika sera na program za nchi.Zinalenga kuzuia upotevu wa rasilimali ya mazingira kama vile miti na maji.Lengo lipokuhakikisha kuwa katika kipindi hiki wanachama watapunguza kwa asilimia 50 idadio ya watu wanaoshindwa kupata maji safi na salama – hii ni moja wapo ya malengo ambayo, kwa mujibu ya tovuti ya umoja wa mataifa www.un.org/milleniumgoals, kuna matumaini ya kutimiza zaidi ya 2015. Mwisho kuna lengo la kujenga mshikamano wa maendeleo duniani, kwanza kwa kuboresha zaidi mfano wa Fedha na biashara duniani kuhakikisha ni wa usawa, unafuata sheria na kamwe hauna ubaguzi.Utawala bora; kushughulikia mahitaji ya kipekee ya nchi changa kama vile kuziondolea ushuru wa bidhaa muhimu,kuzipunguzia au kuziondolea madeni; kutoa misaada zaidi kwa nchi maskini zinazotia jitihada kutoa umaskini kushughulikia mahitaji muhimu, ya visiwa vidogo na nchi zisizo na bandari miongoni mwa nchi zinazoendelea; kuwapa vijana ajira bora; kushirikiana na sekta za kibinafsi ili kuimarisha teknolojia ya kisasa hasa katika habari na mawasiliano ni baadhi ya yanayozingatiwa kulenga kutimiza mshikamano huu. MASWALI. 1. Malengo ya maendeleo ya milenia ni nini? (Alama 2) ................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................ 2. Ni wachochole wa kiwango gani wanaolengwa kuinuliwa na hatua za malengo ya maendeleo ya milenia? (Alama 1) ........................................................................................................................................................................ 3. Taja vipengele viwili muhimu kuhusu elimu katika katiba mpya ya Kenya vinavyo changia kufikia malengo ya maendeleo ya milenia? (Alama 2) ................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................ ........................................................................................................................................................................ 4. Gusia changamoto tano zinazowakabili kina mama wajawazito katika ulimwengu wa tatu. (Alama5) ....................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................... 5. Kampeni dhidi ya magonjwa sugu inafanywa kwa namna gani. (Alama 2) ................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................ 6. Hali ya maji inatarajiwa kuwaje kufikia 2015. (Alama 1) ....................................................................................................................................................................... 7. Eleza maana ya vifungu hivi. (Alama 3) a) Hawazai njiti ............................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................... b) Vifo vya uzazi. ................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................................ MWONGOZO WA KUSAHIHISHA 1. Majibu ya Ufahamu. 1. Malengo manane ya nchi wanachama wa umoja wa mataifa,ambayo nchi hizi zilikubaliana kujizatiti kufikia mwaka wa 2015. (Alama 2) 2. Maskini ambao kipato chao ni cha chini ya dola moja kwa siku. (Alama 1) 3. i) Inaanzia shule ya chekechea hadi kidato cha nne. (Alama 2) ii) Ni ya lazima, yaani mtoto sharti ahudhurie masomo. (Alama 1) 4. i) Kutohudhuria kliniki wakati wa kulea mimba. ii) Huduma kwa wajawazito kuwa mbali sana. iii) Namna za usafiri kuwa duni. iv) Kuhudumiwa na ‘wakunga’ wasiohitimu au hata kujifungua pweke. v) Ukosefu wa kinga muhimu na lishe bora. (zozote 3 alama 5) 5. Kwa kutumia vyombo vya habari na vituo tamba vilivyo na maafisa wa nyanjani. (Alama 2) 6. Kupunguza kwa asilimia 50 idadi ya watu wanaoshindwa kupata maji safi na salama . (Alama 2) 7. i) ‘Hawazai njiti’ – Mimba hazitoki . (Alama 1) ii) ‘Vifo vya uzazi’- vifo vinavyotokea wakati kina mama wanajifungua. (Alama 1)
0 Comments
Leave a Reply. |
Categories
All
Archives
July 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|