Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
1. UFAHAMUSoma makala yafuatayo kisha ujibu maswali. Ulimwengu unapaswa kuzuka na mbinu za kulitadarukia tatizo ambalo linakwamiza juhudi za maendeleo. Umaskini unaoyakabili mataifa yanayoendelea, unayatosa kwenye dhiki kubwa huku mataifa ya kimagharibi yakipiga hatua kubwa kimaendeleo. Ufa uliopo baina ya mataifa yanayoendelea na yale yaliyoendelea kama vile Marekani, nchi za Ulaya na Ujapani unapanuka kila uchao. Vyanzo vya umasikini huu ni anuwai mathalan,ufisadi uongozi mbaya, turathi za kikoloni, uchumi kuegemezwa kwenye kilimo kinachotegemea mvua isiyotabirika, idadi ya watu inayoupiku uwezo wa uchumi wa taifa linalohusika na ukosefu wa nyenzo na amali za kuwakwamua raia kutoka lindi la umaskini. Ukosefu wa elimu na nafasi adimu za ajira huchangia pia katika tatizo hili. Jamii ya ulimwengu inapaswa kuelewa kuwa umaskini, unaoathiri nchi fulani una athari pana sana. Uvunjifu natokana na umaskini unaweza kuwa mboji ambako matendo mabaya huchipuka. Raia maskini huweza kushawishiwa haraka kujitosa kwenye matendo ya kihalifu ili kujinasua kutoka dhiki ile. Hii inaweza kuwa mbegu ya kuatika maovu kama ugaidi na uhalifu wa kila aina. Mataifa ya magharibi yanapaswa kuyaburia madeni mataifa yanayoendelea kama njia mojawapo ya kupambana na umaskini. Asilimia kubwa ya pato la kitaifa katika mataifa mengi hutumika kuyalipa madeni hayo. Katika hali hii inakuwa muhali kwa mataifa hayo kujikwamua kutokana na pingu za umasikini. Njia nyingine ni kustahabu kutoa ruzuku za kimaendeleo badala ya mikopo kwa nchi zinazoendelea. Kwa upande wake, mataifa yanayoendelea yanapaswa kuibuka na mikakati bora ya kupambana na umaskini. Ni muhimu pawepo na sera zinazotambua ukweli kuwa asilimia kubwa ya raia wa mataifa hayo ni maskini. Pana dharura ya kuzalisha nafasi za ajira, kupanua viwanda hususan vinavyohusiana na zaraa ambayo ni tagemeo kuu la mataifa mengi, kuendeleza elimu na kuimarisha miundo msingi. Ipo haja pia ya mataifa haya kuhakikisha kuwa mfumo wa soko huru unaotawala ulimwengu sasa hauishii kuwa chanzo cha kufa kwa viwanda asilia na kuendeleza umaskini zaidi. Kwa ufupi, maamuzi yote ya sera za kiuchumi lazima yauzingatie uhalisi wa maisha ya raia wa mataifa hayo. MASWALI a) Kwa nini umaskini umetamalaki katika mataifa yanayoendelea? (alama 4) ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… b) Madeni yana athari gani kwa mataifa yanayoendelea? (alama 2) ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… c) Ni mapendekezo yapi ambayo mwandishi anatoa kwa mataifa machanga kuhusu utatuzi wa tatizo la umaskini? (alama 4) ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… d) Mfumo wa soko huru una madhara gani kwa mataifa machanga? (alama 2) ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… e) Ukirejelea kifungu, eleza maana ya: (alama 3) i) Kulitadarukia ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… ii) Kuatika ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… iii) Kuyaburia madeni ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… 1. UFAHAMU a) i) Ufisadi ii) Uongozi mbaya iii)Turathi za kikoloni iv) Uchumi kuegemezwa kwenye kilimo kinachotegemea mvua isiyotabirika v) Idadi kubwa ya watu inayoupika uwezo wa uchumi taifa linalohusika vi) Ukosefu wa nyenzo na mali za kuwakwamua raia kutoka lindi la umasikini vii) Ukosefu wa elimu na nafasi za ajira (4x1=4) b) Asilimia kubwa ya pato la kitaifa katika mataifa mengi hutumika kuyalipa madeni hayo. (1x2=2) c) i) Kuibuka na mikakati bora ya kupambana na umasikini ii) Pawepo na sera zinazotambua ukweli kuwa asilimia kubwa ya raia wa mataifa hayo ni masikini iii) Kuzalisha nafasi za kazi kwa dharura iv) Kupanua viwanda hususan vinavyohusiana na zaraa ambayo ni tegemeo kuu la mataifa mengi v) Kuendeleza elimu vi) Kuimarisha miundo msingi (4x1=4) d) Ni chanzo cha kufa kwa viwanda asilia na kuendeleza umasikini zaidi (1x2=2) e) i)kulitadarukia – kulishughulikia, kulitatua kulikabili ii) Kuatika - kuanzisha , kutia , kuzua iii) Kuyaburia madeni. Kuyasamehe madeni, kuyaondolea madeni (3x1=3)
0 Comments
Leave a Reply. |
Categories
All
Archives
July 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|