Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
Tofautisha istilahi zifuatazo za Fasihi Simulizi. (alama 3)Matambiko Sadaka au ada inayotolewa kwa Mungu, mizimu, pepo au miungu ili wasaidie binadamu kutatua mambo magumu, kuomba radhi au kutoa shukrani. Matatizo ni kama vile ukame, magonjwa, kukosa watoto, mafuriko au janga lolote lililomshinda binadamu nguvu na uwezo. Pembezi Tungo za sifa za watu wa aina fulani wanaosifika kwa matendo yao au nafasi walizo nazo katika jamii kv matendo ya kishujaa au kujitolea kwao. Km viongozi, walezi wazuri, waganga, nk Misimu Semi zinazozuka na kutumiwa na kundi fulani la wanajamii kama misemo ya mawasiliano baina ya wanakikundi hicho./ Ni semi za muda na mahali maalum ambazo huzuka tu kutegemea mazingira maalum./ Ni semi ndogo ndogo za kupita. Huzuka katika mazingira fulani na hufa baada ya kutokuwepo kwa mazingira yale.
0 Comments
Leave a Reply. |
Categories
All
Archives
July 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|