Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
INSHA
MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA
MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA 1. Mtahiniwa azingatie yafuatayo; Mbinu za kupambana na ufisadi -Kuelimisha wananchi kuhusu madhara ya ufisadi kupitia kwa redio, magazeti, runinga n.k. -Kuwaadhibu wahusika – wapelekwe mahakamani na wafungwa jela. -Wananchi waadilike (wawe na maadili mema). -Viongozi wawajibike katika kazi zao. -Sheria za kupambana na ufisadi zibuniwe na kutekelezwa. -Kubuni nafasi zaidi za kazi -Kuimarisha elimu -Kuongeza mishahara kwa wafanyikazi -Tume zaidi za kukabiliana na ufisadi zibuniwe. SURA YA MAHOJIANO -Insha iwe na kichwa kinacholenga mada -Kuwe na mhoji na mhojiwa -Njia ya maswali na majibu -Njia ya kitamthilia ufuatiwe kwa mfano; Juma: Bakari: TAHADHARI -Atakayefululiza bila kufuata mtindo wa mahojiano aondolewe alama (4) sura baada ya kutuzwa. 2. i) Kilimo cha mboga ii) Upanzi wa miti iii) Utengenezaji wa matofali na kuyauza. iv) Ukarabati wa barabara v) Kushirikiana na polisi katika kutoa usalama kwa umma. 3. Maana ya methali Ikiwa umekwisha jitayarisha kufanya jambo, basi bora ulikabili / ulifanye na ulimalize. -Mtahiniwa aandike kisa kitakachothibitisha ukweli wa methali. -Aonyeshe mtu aliyeanza jambo licha ya vikwazo / matatizo, alijibidiisha kulikamilisha. 4. Sharti mtahiniwa aanze insha kwa maneno aliyopewa bila kubadilisha wala kuongeza. Insha ionyeshe harakati za kumtafuta baba mzazi Asimulie jinsi alivyotambua / alivyokutana na babake kwa mara ya kwanza. Hisia alizozipata kv. Furaha / chuki Iwapo mkutano huu ulifaulisha maisha yake ya usoni au la. Ugunduzi wake ulivyoathiri maisha yake TAZ: Kisa kisimuliwe kwa njia ya kuvutia na kusisimua.
0 Comments
Leave a Reply. |
Categories
All
Archives
June 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|