Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
SURA YA KWANZA
Chini ya mti mmoja kando ya mto Kiberenge, vijana wawili, amani na Imani wanapunga hewa baada ya kukata kiu. Aidha, wamo safarini kuelekea Sokomoko, kila mmoja na haja yake. Kitambo kidogo tu, wawili hawa wamevunja mwiko kwa kuyanywa maji ya mto kiberenge ambao wenyeji wanaamini kuwa haramu. Muda si kitambo, wenyeji hawachelewi kuambizana na kusimuliana juu ya waja wawili, waliovunja mwiko kwa kuyanywa maji haramu ya Kiberenge na wakakosa kuaga dunia. Kwa kweli, wakati mwingine haramu huweza kuhalalishwa kulingana na watendwa. Imani anayo imani kwamba hakuna haja yoyote ya kuogopa kutenda bila kujaribu.
Ni katika harakati hizi za kukata kiu ndipo wanapokutana na vijana wanaokoga na kupiga mbizi mtoni. Wakati huu, mifugo ya matajiri wanala nyasi baada ya kujitosheleza kwa maji. Fahali mmoja mweusi anaizoa kinywani suruali moja kuukuu linalomilikiwa na na kijana mmoja mnene sana. Wanapogundua linalojiri baada ya kufahamishwa na Imani, vijana wale wanaparamia ukingoni na kuanza kumfukuza Yule fahali lakini wapi, anaposimama, suruali keshaimeza tumboni.
Ndilo vazi la kipekee alilokuwa nayo DJ, kwikwikwi na msononeko zikamkaba yule kijana hohehahe asiye na mbele wala nyuma. Jahazi linaokolewa na Amani anapofungua mkoba wake na kutoa shati moja, akamwita kijana yule na kumpoza shati. Kwa kuwaamini wageni hawa wasiojulikana kutoka kwao, DJ anawasimulia yaliyomjiri. Kazaliwa na kukuzwa na mama mmoja mpishi wa pombe haramu mtaani Madongoporomoka mjini Songoa. Kasingiziwa kuiba na kufungwa jela ya watoto anakotoroka na ndipo kufika Sokomoko anakoajiriwa na mkewe Maozi kama mmoja wa familia. Hatimaye, wanaandamana kuelekea Sokomoko ambako DJ awaelekeza kwa ndugu wawili matajiri, Mtemi Nasaba Bora anayehitaji mchungaji ilhali kakake Mwalimu Majisifu anahitaji kijakaza. Njiani, anawatahadharisha kuhusu udhalilishaji na mishahara duni ambazo wangekumbana nazo. Hapa ndipo Amani kategua siri kadhaa zikiwemo kutafuta njia yakumwokoa amu yake na kufichwa kwa mali ya nasaba yake. Kajitayarisha kukumbana na mahasimu wake, bila dhamira ya kulipiza kisasi. Imani naye kafika kwa kukosa pa kuenda baada ya mastakimu yake kuteketezwa na wasiojulikana. Amani ana umri wa miaka ishirini naye Imani kumi na minne.
0 Comments
Leave a Reply. |
Categories
All
Archives
July 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|