Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
MUHTASARI2. MUHTASARI Soma taarifa hii kisha ujibu maswali Sisi vijana wa Kenya inatupasa tuwajibike kufanya kazi kwa bidii na kwa dhati ya mioyo yetu uweze kupata ufanisi na uwezekano wa kuinua nchi yetu changa katika kiwango cha juu. Tukumbuke, “Ajizi ni nyumba ya njaa.” Kwa hivyo basi haifai kulaza damu ikiwa matatizo nchini mwetu yametuzonga. Lazima tofanye kazi kwa busara, adabu njema na jitihada kwa moyo mmoja. Sharti tutilie maanani zaidi elimu ya vijana na watu wazima, kilimo, uchumi na amani katika nchi yetu. Tunahitaji taifa la watu walioelimika, kwani bila elimu itakuwa vigumu sana kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo. Tupende tusipende lazima tuzidishe mazao shambani, kwani kila kukicha idadi ya watu inaongezeka. Ni sharti tuweze kujitosheleza katika vyakula. Zaidi ya hayo lazima tujishughulishe na biashara ambapo kwa sasa ni wakenya wachache sana ambao wanatambua umuhimu wake. Wengi ni wale wenye mawazo kwamba lazima aajiriwe maishani. Yatupasa tujitahidi kuleta uchumi katika mikono ya wananchi wa Kenya badala ya kuwaachia wageni. Mafunzo tunayopata nyumbani, shuleni na hata katika jamii, lazima yatuwezeshe kutambua mbinu za kupitia. Tunahitaji elimu tambuzi ambayo itamfanya mwana Kenya kujua wajibu wake katika jamii. Tumesinywa na elimu pumbao; inayo tumbaza na kufanya tusione mbele. Sisi vijana tukiwa viongozi wa siku zijazo tuwe kielelezo chema kwa wengine. Watu wazima washirikiane na kufikiria kwamba wao ni wamoja, “utengano ni uvundo” lugha ya kitaifa ndicho chombo cha pekee ambacho kinatuunganisha na kuwaza kutuwasilishia mapendekezo, mawaidha na hisia zetu. Kukosa ndiko kibinadamu, wakati tunapokosea na kufanya masahihisho. Mara moja kwani; “usipoziba ufa, utajenga ukuta”. Tusikasirike kwa sababu tumesahihishwa makosa yetu na wenzetu. Lazima tujitoe mhanga na kupigania nchi yetu tukiwa wazalendo halisi. Sisi tukiwa vijana sharti tujishughulishe na kuyaangalia matatizo ya nchi, pia kutafuta njia za kutatua matatizo hayo. Siku zote tutekeleze nidhamu. Ni jambo la kusikitisha kwamba sisi vijana twashtumiwa mara kwa mara kwa kutokuwa na nidhamu shuleni na majumbani mwetu. Utamaduni wa asili unakariri sana kuwa tuwe na nidhamu shuleni na nyumbani mwetu. Ili watu waweze kuishi maisha bora na kuwa na maendeeo, amani na upendo; lazima tuwe na bidii, ushirikiano mwema na kuchagua viongozi wenye mioyo ya maendeleo, tukiwa viongozi ambao hawajishughulishi na maendeleo, basi tutabaki nyuma kama mkia siku zote. Bahati mbaya ni kwamba wananchi wengi siku hizi huchagua viongozi wao kwa kufuata ukoo ama utajiri wake. Kwa hivyo basi tuchagueni viongozi ambao watatuletea ufanisi badala ya viongozi wanaotokana na nasaba au utajiri. (a) Dokeza mambo muhimu yaliyomo katika aya ya kwanza.(maneno 65-70) (al 8,2 utiririko) Nakala chafu ………………………………………………………………………………………………………..…… ..…………………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………………………………………..… ..…………………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………..…… ..…………………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………..…… ..…………………………………………………………………………………………………………… Nakala safi ………………………………………………………………………………………………………..…… ..…………………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………………………………………..… ..…………………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………..…… ..…………………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………..…… ..…………………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………..…… (b) Fupisha aya ya mwisho kwa kuzingatia mambo muhimu yanayopasa vijana kufanya. (maneno 35- 45) (ala 4, 1utiririko) Nakala chafu ………………………………………………………………………………………………………..…… ..…………………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………………………………………..… ..…………………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………..…… ..…………………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………..…… ..…………………………………………………………………………………………………………… Nakala safi ………………………………………………………………………………………………………..…… ..…………………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………………………………………..… ..…………………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………..…… ..…………………………………………………………………………………………………………… ………………………………………………………………………………………………………..…… ..……………………………………………………………………………………………………………
0 Comments
Leave a Reply. |
Categories
All
Archives
July 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|