Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
1. MUHTASARI Ingawa baadhi yetu hufanya makosa tunapochagua marafki, ni vyema kuzingatia kwa makini sifa za rafiki yako. Kukosa kufanya hivi kunaweza kututia mashakani kwani rafiki mbaya anaweza kukuambukiza ubaya. Tusisahau kuwa nazi mbovu harabu ya nzima. Kwa sababu hii, sifa nzuri ni nguzo ya urafiki: sifa nzuri hutufanya kufurahia pamoja bila hata wazazi wetu kuhofu chochote kwani urafiki huwa nipe nikupe.Hata hivyo, katika kusaidiana hatuwapi marafiki wetu mali au zawadi tu. Hii ni kwa sababu tunaweza hata kukosa pesa au zawadi za kuwapa marafiki ingawa tunawapenda. Kwa hivyo, katika urafiki tunabadilishana mawazo mbalimbali na kumwonyesha rafiki ni kwa nini tunampenda. Urafiki kama huu huwajenga wote wanaohusika. Katika urafiki, ni vyema kuzingatia ukweli na uaminifu. Iwapo tunaishia kuwaiga marafiki au “kujifanya” ili kuwafurahisha marafiki kutupenda, basi, huenda tusifaidi kwa urafiki. Hii ni kwa sababu hali ya kuvalia ngozi ya kondoo kumbe tu simba mara nyingi huvunga urafiki baina ya watu pale sifa za mtu zinapojitokeza dhahiri kwani ukweli ukidhihiri uongo hujitenga. Hapo ndipo mmoja kati ya wale marafiki anapoanza kusema kuwa “afadhali ningejua.” Hii ndio sababu watu huambiwa kuwa makini sana katika kuchagua marafiki na kuchukua muda kabla ya kuwaamini watu kuwa marafiki wetu wa dhati. Pia, ili kufaidi katika urafiki ni vyema kuwa na rafiki ambaye umri wake na wako ni wa karibu. Rafiki kama huyu atakuwa huru kujadiliana nawe kuhusu yote yanayowahusu. Kwa upande mwingine, rafiki ambaye ana umri mkubwa zaidi ama mdogo sana kwako itakuwa shida kushirikiana naya kwa sababu mtazamo wake na wako kuhusu maswala mengi katika jamii utakuwa tofauti kabisa kama ardhi na mbingu. Hebu fikiri kuwa na rafiki ambaye huna uhuru kuzungumza naye yoyote utakayo kwa sababu unaomwogopa ama nafikiria yeye hataweza kukusaidi kimawazo. Kuna hali nyingine ambayo tunapaswa kuepuka katika urafiki. Tunapofikiria kuhusu marafiki wanaotufaa, tunafaa kutozingatia mambo kama vile utajiri au pesa. Ikiwa tutazingatia swala kama hili katika kuwa na urafiki na mtu, basi, lazima tuwe tayari kwa kuharibika kwa urafiki huu wakati wowote. Hii ni kwa sababu urafiki wenye misingi katika mambo kama hayo huisha wakati wowote mambo yanapokwenda mrama hasa kwa yule ambaye alikuwa akitegemea pesa hizi kwa urafiki. Pia, inaweza kuwa rafiki huyo hakupata pesa hizo kwa njia halali jambo ambalo linaweza kututia matatani. Lakini, hii haimaanishi tusiwe na marafiki ambao wanatoka katika jamii tajiri. Ikiwa urafiki wenu utakuwa na sifa zote zinazofaa bila hata kuzingatia mali yao, basi itakuwa sawa kabisa. Lazima tukumbuke kuwa urafiki ni tunu kubwa kwa maisha yetu hata bila pesa. Kwa ujumla, ni muhimu kuzingatia kuwa urafiki hali kati ya wawili au zaidi anbayo inajengwa kwa muda na utaratibu. Huwezi kusema kuwa mtu ni rafiki baada ya muda mfupi kama hamjajuana kwa muda unaofaa. Ni lazima ichukue muda mjuane vizuri. Kukosana baina ya marafiki ndiko kujuana na kujenga urafiki wenye nguzo inayofa katika jamii. Dondoa sifa kuu za kumchagua rafiki katika aya nne za mwanzo. (maneno kati ya 30-40) utiririko - (alama 6) Matayarisho ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………………………………………… Jibu ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………………………………………… a) Andika kwa ufupi yanayoangaziwa katika aya mbili za mwisho (maneno kati ya 45-55) matayarisho ………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… Jibu ……………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………… 1. UFUPISHO a) i)-Rafiki mweye sifa nzuri ii)-Kupendanahata kama hakuna pesa au zawadi ii)-Urafiki wa kubadilishana mawazo mbalimbali iv)-Kuzingatia ukweli na uaminifu v)-Rafiki mwenye umri sawa vi)-Rafiki mwenye umri mkubwa hamuwezi kushirikiana naye ipasavyo (kila hoja alama 1 jumla alama 6) b) i) Kutozingatia mambo kama utajiri tunapochagua marafiki ii) Urafiki huenda ukaharibika wakati wowote iii) Waweza kuwa matatani ikiwa pesa za tajiri ni haramu iv) Lakini waweza kuwa na rafiki tajiri bila kuzingatia mali yao v) Urafiki ni hali inayojengwa kwa muda na utaratibu vi) Kukosana baina ya marafiki ndiko kujuana (kila hoja alama 1) (utiririko alama 3) (jumla alama 6)
0 Comments
Leave a Reply. |
Categories
All
Archives
July 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|