Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
1. MUHTASARI: (Alama 15) Ponografia na athari zake: Ponografia ni tendo, maandishi, picha au mchoro unaoonyesha au kueleza uchi wa mtu au vitendo vya ngono kwa ajili ya kuchochea ashiki ya kufanya. Mambo haya machafu huwasilishwa ana kwa ana kupitia sinema, video, magazeti, vitabu, muziki, televisheni, wavuti, DVD n.k. Ponografia imekuwepo tangu jadi, hasa katika nchi za magharibi. Lakini sasa limekuwa tatizo sugu. Hii ni kwa sababu imeenea ulimwenguni kote mithili ya moto katika mbuga wakati wa kiangazi. Uenezi umechangiwa na mambo kadha wa kadha. Mchango mkubwa zaidi umetokana na kuimarika kwa vyombo vya teknolojia ya habari na mawasiliano. Matumizi ya tarakilishi, mdahilishi na viungambali vya picha yamesambaza ponografia haraka na kwa wingi. Haifahamiki barabara jinsi ponografia ilivyoanza. Hata hivyo hubuniwa au kutengenezwa na makundi mbalimbali ya watu. Miongoni mwa hawa ni watu wasiojali maadili. Pili, kuna wale wenye matatizo ya kisaikolojia na kijamii. Wao hutengeneza na kueneza uchafu huu kwa lengo la ama kuvuruga maadili katika jamii au kuchukiza wanajamii waadilifu. Kundi lingine ni lile la wanaoichukulia ponografia kama nyenzo ya kutosheleza ashiki zao. Hivi sasa, kundi kubwa ni lile la wanaotumia matusi haya kama njia ya kuchuma. Kwa mfano, kuna wanamziki ambao hutumia ponografia kuvutia wateja na hivyo kuzindisha mauzo yao. Kushamiri kwa wimbi la uonyeshaji ponografia kuna athari kubwa kwa jamii na hasa watoto. Ingawa watu wengine hudai picha hizi haziwaathiri, upo ushahidi kuonyesha kuwa wanaotazama picha za ngono hupata matatizo. Lazima ieleweke kuwa kinachoonekana na jicho au kusikika kwa sikio huathiri fikra au hisia. Picha za matusi zinachangia kwa kiasi kikubwa kuharibu akili. Badala ya kuzingatia mambo muhimu kama masomo watu huanza kutafakari mambo machafu. Vijana wengi ni kama bendera. Hivyo basi huanza kuiga wanayoyaona na kusikia. Hili ni tatizo linalowafanya kuacha mkondo wa maadili. Kutokana na uchafu huu, watu wengi hushawishiwa kuingilia shughuli za ngono mapema kabla hawajakomaa kimwili, kiakili na kihisia. Matokeo yake ni mengi. Haya ni pamoja na ukahaba. Utendaji mbaya shuleni, mahudhurio mabaya darasani na mambo yasiyotarajiwa. Vijana wengi huacha shule kabisa.Wengine wao huambukizwa magonjwa ya zinaa ambayo huwaletea mauti. Inasemekana kuwa akili za binadamu hunata zaidi mambo yanayowasilishwa kwa picha. Si ajabu, vijana huyadumisha matusi haya katika kumbukumbu zao na kuyafanya sehemu ya maisha yao. Wengi huanza kuandama tabia mbovu kama ushoga, ubasha na usagaji. Kuna wale ambao huanza kujichua. Kujichua ni hali ya mwanamke au mwanamume kumaliza haja za kimaumbile bila kufanya mapenzi na mtu mwingine. Ponografia imechangia pakubwa kuenea kwa haya. Jambo hili limegeuza mielekeo ya vijana.Wanaiga mitindo mibaya ya mavazi yanayoanika uchi wao. Halikadhalika, huiga lugha, ishara na miondoko inayohusiana na ngono. Yote haya yanapingana na desturi za mwafrika. Si ajabu visa vya ubakaji vinaongezeka kila kuchapo. Utazamaji wa picha chafu aghalabu huandamana na maovu mengine kama unywaji wa pombe, matumizi ya dawa za kulevya, uvutaji sigara na utumiaji wa dawa za kuchochea uchu wa ngono. Mambo haya huwapa vijana tabia za unyama. Jambo hatari ni kuwa, kuendelea kutazama picha hizi huzifanya nishai na hisia za watu kuwa butu, yaani huondoa makali. Hata katika utu uzima, mtu atapoteza mhemko wa kawaida na kugeuzwa kuwa mtegemezi wa ponografia. Tatizo hili linaenea kwa vishindo mijini na vijijini. Ipo haja ya dharura kuikinga jamii kutokana na maenezi haya yasiyo kizuizi. Jambo la kwanza ni kuongeza ufahamu wa umma wote kuhusu uovu wa picha hizi. Kwa namna hii itawezekana kupunguza mahitaji na uuzaji wa ponografia. Aidha ni vizuri watu wazima wawajibike ili wawalinde hasa vijana kutokana na adhari hizi. Inapasa wenye midahilishi, video na sinema wasiwaruhusu vijana kutazama uchafu huu. Tatizo la kuenea kwa ponografia limeendelea kuwepo kwa sababu ya udhaifu wa sheria. Kilicho basi ni kuweka sheria za kuzuia utengenezaji na usambazaji wa upungufu huu. Kuambatana na haya, hatua kali zichukuliwe kwa wanaovunja sheria hizi. Halikadhalika, ushirikiano wa karibu baina ya wadau uimarishwe katika ulimwengu mzima. Serikali na mashirika ya midahilishi yajumuike kutambua chanzo cha taka hizi kisha wanaohusika wakabiliwe ipasavyo. Jamii ingependa kuona michakato ya kuharamisha utengenezaji, usambasaji na utangazaji wa ponografia ikiwekwa. Wazazi nao wasijipweteke tu bali wasaidie. Ni muhimu washikilie kwa dhati juhudi zao za kuwaelekeza na kuwashauri watoto kuzingatia uongofu na kukwepa picha hizi najisi. Watoto lazima waelezwe kuwa haifai kutazama picha au michoro michafu. Itikadi na imani za kidini na utamaduni wa kiafrika unakataza vikali mtu kuona uchi wa mtu mwingine. Matokeo ya kuasi makatazo haya yana madhara makubwa kwa watu na jamii. Maswali: 1. Ponografia hutengenezwa na akina nani na kwa nini?(maneno 20) (Alama 2) ……………………………………… 2. Eleza sababu za ponografia kusambaa ulimwenguni namna ilivyofanywa.(maneno 10) (Alama 2) ………………………………………… 3. Fupisha aya za mwisho tatu kwa maneno 60. (Alama 7) ……………………………………………… (Utiririko. Alama 2 baada ya kupitia kama wavutia la sivyo pima uwezo wa mtahiniwa.) (Alama 2) ………………………………………………… Muhtasari 1. - Watu wanaotosheleza ashiki zao. - Hutengenezwa na watu wasiojali maadili. - Hutengenezwa na makundi mbalimbali ya watu wasiojali maadili yoyote. (Hesabu maneno) (alama 2 ) 2. Sababu za kusambaa • Akili za binadamu kunata yanayowasilishwa kwa picha. • Mitindo mibaya ya mavazi yanayoanika uchi wao. • Lugha, ishara na miondoko inayohusu ngono. Sentensi moja au mbili zilizo na hoja hizi (idadi ya maneno iwe kati ya 6-13) (alama 2) 3. Kueleza ubaya wa ponografia kwa umma. • Kuweka sheria za kuzuia ueneaji. • Ushirikiano wa karibu baina ya washika dau uimarishwe. • Wazazi kuwaelekeza na kuwashauri watoto wazingatie uongofu na kuepa picha hizi. (Idadi ya maneno kati ya 56 – 63) Muhtasari Tanbihi i) Pitia majibu yote ii) Dondoa makosa ya sarufi na hijai iii) Ongeza alama 2(mbili) iwapo mtiririko ni mzuri (tathmini utiririko wa mtahiniwa) Mfano J = 13 J = jumla ya alama Ut = 2 Ut = utiririko bora 15 S – 1 ½ S = makosa matatu tofauti ya sarufi 13 ½ h = 2 h = makosa manne tofauti ya maendelezi 11 ½ 12
0 Comments
Leave a Reply. |
Categories
All
Archives
July 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|