Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
MATUMIZI YA LUGHA3. MATUMIZI YA LUGHA (a) Akifisha kifungu kifuatacho. (alama 3) nilipowasili tu nilishika tama nikashangaa loo moto huo ulianza vipi na ulikuwa umesababishwa na nini nilishikwa na bumbuwazi magoti yangu yakaanza kuchezacheza. …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... (b) Tunga sentensi moja katika umoja kisha uigeuze ili iwe katika wingi ili kudhihirisha ngeli ya LI – YA. (alama 2) (i) …………………………………………………………………………………………………… (ii)…………………………………………………………………………………………………… (c) Changanua sentensi ifuatayo kwa kutumia jedwali. (alama 2) Baba anafyeka nyasi ilhali mtoto anaambua viazi …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... (d) Andika katika msemo wa taarifa: (alama 4) Zainabu : Aa! Mbona umeketi peke yako kaka? Wenzako wajistarehesha huku na huko, wewe umekaa pweke, kwa nini? Una mkasa gani? Kagame: Sina mkasa wowote, dada, ila nasumbuliwa na ugeni tu. Niliwasili hivi juzi na sijapata sahibu hata mmoja, ndiyo sababu ukaniona katika hali hii ya upweke …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... (e) Sahihisha sentensi zifuatazo bila kugeuza maana. (i) Mtume mwenye wamefika ni mrefu. (alama 1) ……………………………………………………………………………………………………… (ii) Twiga hukimbilia mbio ingawa ni ndefu. (alama 1) ……………………………………………………………………………………………………… (f) Andika kwa wingi: (alama 2) (i) Uta uu huu ndio aliotumia kumfuma swara. ……………………………………………………………………………………………………… (ii) Ugomvi wake ulisababisha kutalikiwa kwake ……………………………………………………………………………………………………… (g) Unda nomino mbilimbili kutoka kwa vitenzi: (alama 2) (i) Fuata ……………………………………………………………………………………………………… (ii) Zika ……………………………………………………………………………………………………… (h) Bainisha maana katika sentensi zifuatazo. (alama 2) (i) Isije ikawa Maria anahusiana naye …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... (ii) Huenda ikawa amepitia njia nyingine. …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... (i) Andika upya ukitumia – o –ote (alama 2) (i) Kitabu kikipendwa na wasomaji wengi huwa maarufu. ……………………………………………………………………………………………………… (ii) Kila askari apitaye hapo humchapa. ……………………………………………………………………………………………………… (j) Tunga sentensi moja itakayodokeza matumizi mawili tofauti yas kiambishi ’ka’ (alama 2) …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... (k) Badilisha hadi katika hali ya udogo. (alama 2) (i) Uta.......................................................................................................................................... (ii) Kijiko....................................................................................................................................... (l) Toa maana mbilimbili kwa kila moja ya maneno haya: (alama 2) (i) Kata …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... (ii) Ua …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... (m) Andika sentensi ifuatayo katika umoja. (alama 2) Nyua zenu zanuka kwa sababu hamzitumii kwa uangalifu. ……………………………………………………………………………………………………… (n) Tunga sentensi moja sahihi ukitumia kivumishi kimilikishi. (alama 2) ……………………………………………………………………………………………………… (o) Bainisha wakati na hali katika sentensi: (alama 2) Utakapofika nitakuwa nimekula. …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………........ (p) Iandike upya sentensi ifuatayo ukifuata agizo. (alama 2) Hakika Mogeni alimcharaza mno Manoti, lakini sidhani kuwa kichapo pekee kingepelekea aliyetwangwa kulazwa hospitalini: (Anza: Sidhani...........................) …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... (q) Eleza maana za: (alama 1) (i) Kuteka nyara ……………………………………………………………………………………………………… (ii) Kujenga nyumba za karata (alama 1) …………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………………......... (r) Taja methali moja inayofungamana na maelezo yafuatayo: (alama 1) Wakati mwingine mtu hujikuta au hupatikana asipotarajiwa, asipokusudia ilhali hana makosa au hitilafu yoyote. ……………………………………………………………………………………………………… (s) (i) Kanusha: Waimbaji walio maarufu wamepata tuzo. (alama 1) ……………………………………………………………………………………………………… (ii) Andika kinyume cha sentensi: Mama alimeza dawa yote. (alama 1) ……………………………………………………………………………………………………… 3. LUGHA (a) Nilipowasili tu nilishika tama. Nikashangaa, “Loo! Moto huo ulianza vipi na ulikuwa umesababishwa na nini?” Nilishikwa na bumbuwazi. Magoti yangu yakaanza kuchezacheza 12 x ¼ = 3 (b) (i) Jitu hilo lilinishtua sana usiku huo. (ii) Majitu hayo yalitushtua sana usiku huo - sentensi zaweza kuwa tofauti 2 x 1 =2 (d) Zainabu alishangaa kumwona Kagame ameketi peke yake amesononeka huku watu wengine wakistarehe. Kagame alimfahamisha kwamba hakuwa na mkasa wowote ila alikuwa anasumbuliwa na ugeni tu; hakuwa amepata rafiki au sahibu Alama 4 (e) (i) Mtume aliyefika ni mrefu Mitume waliofika ni warefu (ii) Twiga hutimka/ hukimbia mbio ingawa ni mrefu 2 x 1 = 2 (f) (i) Nyuta zizi hizi ndizo walizotumia kuwafuma swara (ii) Ugomvi wao ulisababisha kutalikiwa kwao 2 x 1 = 2 (g) (i) Kufuata, mfuasi, mfuatano (ii) Kuzika, maziko, mzikaji, mazishi 4 x ½ = 2 (h) (i) Kuhofia isitokee kuwa hivyo (ii) Kutokuwa na uhakika; kukisia 2 x1 = 2 (i) (i) Kitabu chochote kikipendwa na wasomaji wengi huwa maarufu (ii) Askari yeyote apitaye hapo humchapa 2 x 1 = 2 (j) Alifika nyumbani, akaketi kisha akapiga simu Zozote 2 x 1 = 2 (k) (i) Kijiuta (ii) Kijijiko 2 x 1 = 2 (l) (i) Kata – Eneo la kusimamia watu - Kifaa, hasa cha kuchotea maji - Hali ya kutenganisha k. m. uhusiano (ii) Ua – fisha au toa uhai (kitenzi) - Pambo (wingi maua) (nomino: LI – YA) - Eneo lizungukalo nyumba au boma (wingi nyua – U – ZI) 4 x ½ = 2 (m) Ua wako wanuka kwa sababu huutumii kwa uangalifu 4 x ½ = 2 (n) Changu, letu, mwangu 1 x 2 = 2 (o) Wakati ujao, hali timilifu 2 x 1 = 2 (p) Sidhani kuwa kichapo pekee kingepelekea Manoti kulazwa hospitalini ingawa hakika Mogeni alimcharaza mno Alama 2 (q) (i) Kuvamia au kutia mikononi au kuficha kwa nia fulani (ii) Kuota au kufikiria yasiyowezekana haraka 2 x 1 = 2 (r) Mtego wa panya huingia waliomo na wasiokuwamo 1 x 1 = 1 (s) (i) Waimbaji wasio maarufu hawajapata tuzo (ii) Mama alitema dawa yote
0 Comments
Leave a Reply. |
Categories
All
Archives
July 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|