Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
mahojiano1. Lazima Wewe ni miongoni mwa wanahabari wanaomhoji Inspekta Jenerali wa Polisi katika ofisi yake. Andika mahojiano yenu juu ya hatua ambazo zimechukuliwa kuimarisha viwango vya usalama nchini. 2. Mfumo wa ugatuzi nchini umekuwa na ufanisi na changamoto zake. Jadili. 3. Andika kisa kinachodhihirisha maana ya methali: Mti mkuu ukigwa wana wa ndege huyumba. 4. Andika kisa kitakachomalizikia kwa maneno haya: ... ilinichukua muda mrefu mno kayaamini yaliyonifika. MWONGOZO WA KUSAHIHISHA KISWAHILI KARATASI 102/1 2016 1. Wewe ni miongoni mwa wanahabari wanaomhoji Inspekta Jenerali wa Polisi katika ofisi yake. Andika mahojiano yenu juu ya hatua ambazo zimechukuliwa kuimarisha viwango vya usalama nchini. Hii ni insha ya mahojiano na ni utungaji wa kiuamailifu. Vipengele viwili vya utungo wa aina hii vizingatiwe, yaani muundo na maudhui.
Changamoto za mfumo wa ugatuzi
Kadiria hoja zingine zitakazotolewa na mwanafunzi. 3. Andika kisa kitakachodhihirisha maana ya methali: Mti mkuu ukigwa wana wa ndege huyumba. Mwongozo Hii ni insha ya methali. Maana – Mti mkubwa uangukapo, wote wanaoutegemea mti huo huumia ama huathirika kwa namna moja au nyingine. Mtahiniwa aandike kisa kimoja kinachodhihirisha pande zote mbili za methali hii. Hali zifuatazo zaweza kujitokeza:
Hii ni insha ya mdokezo. Mtahiniwa ahitimishe insha yake kwa maneno haya. Hali zifuatazo zaweza kujitokeza:
MWONGOZO WA KUDUMU KENYA CERTIFICATE OF SECONDARY EDUCATION KISWAHILI 102/1 2011 MWONGOZO WA KUSAHIHISHA INSHA UTANGULIZI Karatasi hii imedhamiria kutathmini uwezo wa mtahiniwa wa kuwasiliana na msomaji na kuwasilisha ujumbe kimaandishi, akizingatia mada aliyopewa. Mawasiliano haya yatategemea ukwasi wa lugha ya mtahiniwa, kwa mfano, kutunga sentensi sahihi zenye mtiririko mzuri kimawazo, lugha ya kuvutia na yenye mawazo asilia, ubunifu mwingi na hati nadhifu. Kwa kutegemea maagizo ya swali lenyewe na umahiri wa lugha, ni lazima kutilia mkazo mtindo, mada na uwezo wa mtahimiwa kufuata maagizo vilivyo. Mtahini lazima asome insha yote huku akizingatia sarufi, hijai, hoja, msamiati na mtindo ili aweze kukadiria viwango mbalimbali vilivyopendekezwa. Viwango vyenyewe ni A,B,C, na D kutegemea uwezo wa mtahiniwa. VIWANGO MBALIMBALI KIWANGO CHA D KWA JUMLA MAKI 01-05
D- (D YA CHINI) MAKI 01-02
C- (C YA CHINI) MAKI 06-07
B- (B YA CHINI) MAKI 11-12
A- (A YA CHINI) MAKI 16-17
USAHIHISHAJI NA UTUZAJI KWA JUMLA Mtahini ni sharti aisome insha yote akizingatia vipengee muhimu. Vipengee hivi ni maudhui, msamiati, mtindo, sarufi na hijai. MAUDHUI
Msamiati ni jumla ya maneno yatumiwayo katika lugha husika. Mtahiniwa anatarajiwa kutumia msamiati unaooana na mada teule. Kutegemea ukwasi wa lugha alionao, mtahiniwa anatarajiwa kuikuza mada kwa kufinyanga lugha kiufundi. Ni muhimu kuelewa kwamba kutokana na maendeleo na ukuaji wa teknolojia na mawasiliano, maneno mapya yanaibuka kila uchao. MTINDO Mtindo unahusu mambo yafuatayo:
Sarufi ndio msingi wa lugha. Ufanisi wa mawasiliano hutegemea uwezo wa mtahiniwa wa kutunga sentensi sahihi zenye uwiano wa kisarufi. Mtahini ataonyesha makosa yote ya sarufi yaliyo katika insha anayosahihisha. Makosa ya sarufi huweza kutokea katika:
Haya ni makosa ya maendelezo. Mtahini anashauriwa asahihishe huku akiyaonyesha yanapotokea kwa mara ya kwanza tu. Makosa ya tahajia huweza kutokea:
ALAMA ZA KUSAHIHISHIA ==Hupigwa chini ya sehemu ambapo kosa la sarufi limetokea kwa mara ya kwanza tu. __Hupigwa chini ya sehemu au neno ambapo kosa la hijai limetokea kwa mara ya kwanza tu.
Maelezo mafupi yanahitajika kuhusu tuzo lilotolewa. Kila ukurasa uwe na alama chini kudhihirisha kuwa mtahini ameupitia ukurasa huo. UKADIRIAJI WA UREFU WA INSHA YA PILI Maneno 9 katika kila mstari ukurasa mmoja na nusu. Maneno 8 katika kila mstari ukurasa mmoja na robo tatu. Maneno 7 katika kila mstari kurasa mbili. Maneno 6 katika kila mstari kurasa mbili na robo. Maneno 5 katika kila mstari kurasa mbili na robo tatu. Maneno 4 katika kila mstari kurasa tatu na robo tatu. Maneno 3 katika kila mstari kurasa nne na nusu. Kufikia maneno 174 insha robo. Maneno 175-274 insha nusu. Maneno 275-374 insha robo tatu. Maneno 375 na kuendelea insha kamili.
0 Comments
Leave a Reply. |
Categories
All
Archives
July 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|