Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
KUANDIKA RIPOTI1. Umeteuliwa kama katibu wa tume ya uchunguzi kuhusu vyanzo vya baa la njaa nchini Kenya. Andika ripoti yako. 2. Ufisadi umekuwa saratani katika nchi nyingi zinazoendelea barani Afrika. Jadili mifano mbalimbali ya janga hili na jinsi ya kulitatua. 3. Mchumia juani hulia kivulini. 4. Mlango wa nyuma ulibishwa mara tatu, Ngo! Ngo! Ngo!. Kufungua tu, nikasikia sauti, “ Lala chini¬¬¬......................” (Endelea). MWONGOZO WA KUSAHIHISHIA 1. Insha hii ni ya kiuamilifu kuhusu ripoti, sura ya ripoti kuzingatiwa. (i) Kichwa/Anwani (ii) Utangulizi (iii) Matokeo ya utafiti/uchunguzi/mwili – vijisehemu vidogovidogo (iv) Mapendekezo kuhusu matokeo (v) Hitimisho;maoni ya kamati (si ya Katibu) (vi) Sahihi na tarehe/cheo Vyanzo vya baa la njaa • Ukame • Matumizi/utegemezi wa vyakula vya aina moja • Njia mbovu/duni za kilimo • Uzembe/uvivu • Idadi kubwa ya watu • Watu kuhamia mijini – kupuuza kilimo • Ufisadi – sakata mf – ya mahindi • Njia duni za kuhifadhi vyakula • Hali duni za uchukuzi • Kukosa ardhi (uskwota) Ondoa alama 4 za sura ikiwa haijitokezi – akikosa vipengele 4 kati ya 6 (-4s) Ondoa alama 2 za urefu ikiwa haukuzingatiwa Hoja inapomalizikia ipigiwe mkwaju / ionyeshwe kwa mkwaju. 2. (a). Mifano - Barabarani - Ofisini - Mahakamani - Bungeni - Shuleni - Viwandani - Serikalini - Vijijini - Nyumbani Njia za kutatua - Kuunda tume za kukabiliana na ufisadi - Kulipa mishahara mizuri - Kufunza maadili shuleni - Kutumia dini/mahubiri - Kubuniwa kwa sheria kali - Viongozi wawe mifano mizuri ya uadilifu - Uwajibikaji kazini - Viongozi watangaze mali yao hadharani 3. Maana – Kisawe cha mgaagaa na upwa hali wali mkavu. Anayesumbuka kufanya kazi fulani atanufaika hatimaye • Iwe na kichwa – ingawa si lazima • Maana na matumizi ya methali – si lazima • Kisa/visa – Lazima • Hitimisho – Si Lazima • Mtahiniwa ashughulikie pande mbili za methali vilivyo. Atakayeshughulikia upande mmoja tu asipite C+ (Alama 10) • Atakayepotoka atuzwe D Alama 3 20 • Akitoa maelezo ya moja kwa moja bila kisa/visa amepotoka: D 03 20 4. Mtahiniwa aanzie maneno aliyopewa • Kisa kioane na maneno - Kisa cha kutisha mf. Jambazi, wahuni au askari • Asiyeanzia maneno aliyopewa amepotoka D 03 20 • Atakayeongeza kianzio chake lakini asizidishe maneno matano aondolewe alama 2. • Mtahiniwa ni lazima atumie nafsi ya kwanza na ajihusishe; asipojihusisha amepotoka:. D 03
0 Comments
Leave a Reply. |
Categories
All
Archives
July 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|