Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
1. INSHA YA LAZIMA Wewe ni katibu wa jopo lililoteuliwa kuchunguza changamoto zinazokabili uchapishaji wa vitabu vya Kiswahili nchini.Andika ripoti hiyo. 2. Samaki mkunje angali mbichi. 3. Serikali za ugatuzi zitakuwa na manufaa kwa maendeleo ya nchi.Jadili. 4. Andika insha itakayomalizika kwa maneno haya......... Niliyakumbuka maneno ya mwalimu mkuu,machozi yalitoka njia mbilimbili.Hayawi hayawi huwa. MWONGOZO WA KUSAHIHISHA SWALI LA LAZIMA Ripoti iwe na yafuatayo: a) Kichwa : Kilenge mada kwa kuonyesha ni ripoti ya uchunguzi wa jopo hii. b) Utangulizi : Utangulizi huonyesha aliyeitaka ripoti hii. - Wanajopo. - Sababu za kutaka ripoti hii itolewe. - Malengo ya ripoti. - Utaratibu wa kupata habari kama kuhoji wazazi, wanafunzi washirika wengine. c) Mwili – Ubebe matokeo ya uchunguzi - Yaandikwe kwa vichwa vidogo vidogo. Mapendekezo – kamati itoe mapendekezo kulingana na uchunguzi waliofanya. Hitimisho – Wito wakatibu , sahihi na jina la katibu. HOJA
TANBIHI.
BAADHI YA MAPENDEKEZO.
Mwanafunzi atunge kisa kinachooana na methali ina maana sawa na: usipoziba ufa utajenga ukuta. Maana
SWALI LA TATU.
INSHA MWONGOZO Utangulizi Karatasi hii imedhamiria kutathmini uwezo wa mtahini wa kuwasiliana na msomoji na kuwasilisha ujumbe kimaandishi, akizingatia mada aliyopewa.Mawasiliano haya yatategemea ukwasi wa lugha ya mtahiniwa .Kwa kutegemea maagizo ya swali lenyewe na umahiri wa lugha, ni lazima kutulia mkazo mtindo, mada na uwezo na mtahiniwa kufuata maagizo vilivyo.Mtahini lazima aisome insha yote huku akizingatia sarufi, hijai, hoja, msamiati na mtindo ili aweze kuikadiria kwa kurejelea viwango mbalimbali vilivopendekezwa. VIWANGO MBALIMBALI D – ( D YA CHINI ) MAKI 01 - 02 1. Insha haina mpangilio maalum na haieleweki kwa vyovyote vile. 2. Kujitungia swali tofauti na kulijibu. 3. Kuandika kwa lugha isiyo Kiswahili au kuchanganya Ndimi. 4. Kunakili swali au maswahili na kuyakariri. 5. Kunakili swali au kichwa tu. D – WASTANI MAKI 04 – 05 1. Mtiririko wa mawazo haupo. 2. Mtahiniwa amepooka kimaudhui. 3. Matumizi ya lugha ni hafifu mno. 4. Kuna makosa mengi ya kila aina. D+ (D YA JUU) MAKI 04 - 05 1. Insha huwa na makosa mengi ya kila aina, Lakini unaweza kutambua kile ambacho mtahiniwa anajaribu kuwasilisha. 2. Hoja hazikuelezwa kikamilifu / mada haikukazwa vilivyo. 3. Mtahiniwa hana uhakika wa matumizi ya lugha. 4. Mtahiniwa hujirudiarudia. 5. Insha itakayozingatia sura lakini ikose maudhui ikadiriwe hapa. 6. Insha ya urefu wa robo yaani, isiyozidi maneno 174 isipite kiwango hiki. C- (C YA CHINI) MAKI 06- 07 1. Mtahiniwa ana shida ya kuwasilisha na kutiririsha mawazo yake. 2. Mtahiniwa hana msamiati wa kutosha wala miundo ya sentensi ifaayo. 3. Mtahiniwa anafanya makosa mengi ya sarufi , ya hijai na ya msamiati na insha haieleweki kwa urahisi. C WASTANI MAKI 08 1. Mtahiniwa anawasilisha ujumbe lakini kwa njia hafifu. 2. Dhana tofauti hazijitokezi wazi. 3. Mtahiniwa hana ubunifu wa kutosha. 4. Mtiririko wa mawazo ni hafifu na hana ufundi wa lugha unaofaa. 5. Amejaribu kuishughulikia mada aliyopewa. 6. Ana shida ya uakifishaji. 7. Anafanya makosa mengi ya sarufi, ya hijai na ua msamiati lakini bado insha inaeleweka. C+ (C YA JU) MAKI 09- 10 1. Anawasilisha ujumbe vizuri akizingatia mada lakini bado insha inaeleweka. 2. Dhana tofauti zimejitokeza japo kwa njia hafifu. 3. Kuna mtiririko wa mawazo japo hana ufundi wa lugha unaofaa. 4. Misemo na methali zimetumika kwa njia hafifu. 5. Anashida ya uakifishaji. 6. Kuna makosa ya sarufi ya msamiati na hijai yanayoathiri mtiririko wa mawazo. 7. Insha ya kiwango cha nusu, yaani maneno 175- 274 isizidi kiwango hiki. B – (B YA CHINI) MAKI 11- 12 1. Anawasilisha ujumbe vizuri kwa kueleza hoja tofauti akizingatia mada. 2. Ana mtiririko mzuri wa mawazo. 3. Anatumia mifano michache ya msamiati unaovutia 4. Makosa yanadhihirika / ni kiasi B (B YA CHINI) MAKI 13 1. Anathihirisha hali ya kuimudu lugha. 2. Mawazo yake yanathihirika akizigatia mada. 3. Anateua na kutumia mifano michache ya misamiati mwafaka. 4. Sanja yake ni mzuri. 5. Makosa ni machache. B+ (B YA JUU) MAKI 14 - 15 1. Mawazo yake yanadhihirika na anajieleza waziwazi. 2. Anawasilisha ujumbe kwa njia inayovutia na kwa urahisi akizingatia mada. 3. Ana mchanganyiko mzuri wa msamiati unaovutia. 4. Sarufi yake ni nzuri. 5. Uakifishaji wake wa sentensi ni mzuri. 6. Makosa ni machache ya hapa na pale. 7. Insha ya urefiu wa robo tatu, yaani maneno 274 – 374, isipite kiwango hiki. A- (A YA CHINI) MAKI 16- 17 1. Anadhihirisha ukomavu wa lugha. 2. Mawazo yake yanadhihirika na anaishughulikia mada. 3. Ana mtiririiko mzuri wa mawazo. 4. Msamiati wake ni mzuri na unavutia. 5. Sarufi yake ni nzuri. 7. Makosa ni machache yasikusudiwa. A WASTANI MAKI – 18 1. Anawasilisha ujumbe vizuri kulingana na mada. 2. Anajieleza kikamilifu akitumia lugha ya mnato. 3. Anatoa hoja zilizokomaa. 4. Anatumia msamiati wa hali ya juu na unaovutia zaidi. 5. Anatumia miundo tofauti tofauti ya sentensi kiufundi. 6. Makosa ni nadra kupatikana. A+ (A YA JUU) 19 – 20 1. Mawazo yanadhihirika zaidi na mada imeshughuliwa vilivyo. 2. Anajieleza kikamilifu akitumia lugha ya mnato. 3. Hoja zake zimekomaa na zinashawishi. 4. Msamiati wake ni wa hali ya juu na unavutia zaidi. 5. Sarufi yake ni nzuri zaidi. 6. Anatumia miundo tofauti tofauti ya sentensi, kiufundi. 7. Makosa yote kwa jumla hayazidi matano. ALAMA ZA KUSAHIHISHA = = = Hupigwa chini ya sehemu ambapo kosa la sarufi limetokea kwa mara ya kwanza tu. _ Hupigwa chini ya sehemu au neno ambapo kosa la hijai limetokeza kwa mara ya kwanza tu. ü Hutumiwa kuonyesha hoja inapokamilika pambazoni kushoto. Hutumiwa kuonyesha kuacha kwa neno / maneno. Hutumiwa kuonyesha msamiati bora. Alama hii hutiwa juu ya neno lenyewe. X Hutumiwa kuonyesha msamiati usiofaa. Alama hutiwa juu ya neno lenyewe. Kila ukurasa uwe na alama ya chini katikati ili kuthibitisha kuwa mtahini ameupitia ukurasa huo. Baada ya kutoa tuzo, lazima mtahini aandike udhaifu wa mtahiniwa. Mfano wa kutuza: Robo Tatu C 08/20 Udhaifu Urefu Maudhui Hijai Sarufi
0 Comments
Leave a Reply. |
Categories
All
Archives
July 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|