Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
FASIHI SIMULIZI 7. (a) Eleza maana ya (i) misimu (ii) lakabu (iii) ngomezi (alama 6) (b) Shauri mambo matatu anayopaswa kuzingatia mtu anapohitajika kufumbua fumbo (alama 6) (c) Fafanua umuhimu wa misemo (alama 8) 1. Fasihi simulizi a) maana ya: i) Misimu – lugha ya kisirisiri yenye mafumbo itumiwayo na kundi ndogo la watu katika jamii. ii) Lakabu – majina ya kupanga au utani ambayo watu katika jamii hujipa au hupewa. iii) Ngomezi – fasihi simulizi inayotumia ngoma au zana za kimuziki. (3x2=6) b) Mambo ya kuzingatia katika kufumbua mafumbo i)ufahamu wa lugha iliyotumiwa km takriri, udogoshaji au ukubwa nk ii)ufahamu wa mazingira, utamaduni na hali ya maisha ya watu. Hii ni kwa sababu mafumbo na majibu hutofautiana kutoka jamii moja hadi nyingine. iii)uwezo wa kupata jawabu kwa kulihusisha na mfanano wa hali, tabia au sifa Fulani zinazojitokeza katika kauli ya fumbo. c) Umuhimu wa misemo i) Huogeza ladha katika mazungumzo kwa kupamba lugha. ii) Huonyesha ustaadi wa lugha iii) Hutumika kama tauria (ufunika ukali) km-kata kamba - acha mkono - kututoka iv) Huchochea akili ya mzungumzaji au mzungumziwa (4x2=8)
0 Comments
Leave a Reply. |
Categories
All
Archives
July 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|