Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
MATUMIZI YA LUGHA (Alama 40)a) Eleza matumizi ya kiambishi ‘ka’ katika sentensi hizi ( alama 3) (i) Juma alikuja akachukua kitabu akaondoka ……………………………………………………………… (ii) Mti ulikatika ukaanguka ……………………………………………………………… (iii) “Nyanya anashona nguo”.Hamisi akasema ………………………………………………………………………… b) Changanua sentensi ifuatayo kwa njia ya jedwali (alama 4) Watoto wale wanafanya kazi lakini wazazi wao wanazungumza nyumbani. ……………………………………………………………………………………… c) Unda nomino kutokana na vitenzi hivi ( alama 2) (i) Onea …………………………………………………………………………… (ii) Umia …………………………………………………………………………………… d) Akifisha sentensi ifuatayo (alama 2) Tulifika tukaagana na mjomba hamisi aishiye mombasa …………………………………………………………………………………………… e) Kwa kutoa mifano mwafaka, eleza tofauti baina ya dhana zifuatazo (alama 4) Sauti ghuna na sauti sighuna ……………………………………………………………………………… f) Onyesha kiima, yambwa, na yambiwa, katika sentensi hii (alama 3) Mwanafunzi alimfutia mwalimu ubao ………………………………………………………………………… g) Andika sentensi hii kwa usemi wa taarifa (alama 2) “Lo! Kube wazuri hawajazaliwa,” Omari alisema baada ya kumwona kisura huyo. ……………………………………………………………………… h) Tunga sentensi moja moja kudhihirisha matumizi ya (alama 2) i. Posa ……………………………………………………… ii. Poza ……………………………………………………… i) Andika sentensi zifuatazo katika hali zilizo kwenye mabano (alama 4) i. Kijikombe chake kilivunjika baada ya kuangukia kijiwe (ukubwa) ………………………………………………………………………… ii. Mtu yule haachi kuandamana na mbwa wake aliyedhoofika kisiha (udogo) ………………………………………………………… j) Eleza maana mbili zinazotokana na sentensi ifuatayo (alama 4) Mtoto alitimua mbio, kuona nyoka …………………………………………………………………………… k) Andika sentensi ifuatayo katika kauli ya kutendesha (alama 2) Nguo zote zimekaushwa na jua …………………………………………………………………………… l) Tunga sentensi kudhibitisha mwingiliano wa maneno yafuatayo (alama 2) Nomino kuwa kivumishi …………………………………………………………………………………… m) Andika kwa wingi (alama 2) Kuwepo kwa mshauri wake kulimfurahisha waziri ……………………………………………………………………………… n) Geuza sentensi ifuatayo katika hali ya mazoea huku ukiondoa -amba (alama 2) Mtoto ambaye alikula ndiye ambaye alilia ……………………………………………………… o) Kamilisha methali ifuatayo (alama 1) Asiye na nadhari… ……………………………………………………… p) Eleza maana ya msemo huu (alama 1) Kwenda mbago… …………………………………………………………… MWONGOZO
a) i) Mfululizo wa vitendo wakati uliopita
ii) Hali ya kutendeka / kuwezekana kwa jambo iii) Katika usemi halisi (Alama 3) c) i) Maonevu, kuonea (kitenzi jina) ii) Umio, maumivu (Alama 4) d) Tulifika, tukaagana na mjomba Hamisi aishiye Mombasa. (Alama 2) e) i) Sauti ghuna zinapotamkwa husababisha kutikisika kwa nyuzi za glota km /b/, /g/, /w/. ii) Sauti si ghuna zinapotamkwa, nyuzi za glota hazitisiki kg /ch/, /sh/, /h/, /l/, /n/. (Alama 4) f) Mwanafunzi – Kiima Ubao – Yambwa Mwalimu – Yambiwa (Alama 3) g) Omari alishangaa baada ya kuona kisura yule kuwa wazuri hawakuwa wamezaliwa Baada ya kumwona kisura yule, Omari alishangaa kuwa wazuri hawakuwa wamezaliwa (Alama 2) h) Posa – Maombi ya kuoa Poza – Tuliza / poesha (Alama 2) i) i) Kombe lake lilivunjika baada ya kuangukia jijiwe (Alama 2) ii) Kijitu kile hakiachi kuandamana na kijibwa chake kilichodhoofika kisiha (Alama 2) j) i) Alikimbia kwenda kuona nyoka ii) Alikimbia alipoona nyoka (Alama 4) k) Jua limekausha nguo zote (Alama 2) l) Nomino kuwa kivumishi Kijana mkulima alituzwa (Alama 2) m) Kuwepo kwa washauri wao kuliwafurahisha mawaziri (Alama 2) n) Mtoto alaye ndiye aliaye ( Alama 2) o) Asiye nadhari siandamane naye (Alama 1) p) Kuenda kandokando (Alama 1)
0 Comments
Leave a Reply. |
Categories
All
Archives
July 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|