Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
Soma taarifa ifuatayo kisha ujibu maswali yoteMgomo uliingia siku ya tano. Asubuhi hii ilikuwa mbaya. Watu mbalimbali walikwisha kamatwa mjini na shamba, wakiwemo wote waliohudhuria kikao maalumu kibandani mwa Fumu. Siku ya pili ya mgomo, Makame aliuawa upenuni pa kibanda chake.Alipatikana amechomwa visu vitano vya mbavu. Mauaji ya kikatili lakini hayakuwa ya siri. Boga, yule kijana aliyehudhuria kikao cha pamoja na Fumu, ambaye toka mwanzo hadi mwisho wa kikao hakusema lolote, saa sita za usiku, aliingia kibandani na kumchopeka Makane visu mbele ya mkewe na wanawe, kisha aliikokota maiti na kuitupa upenuni. Asubuhi, Boga alikuwa mtu wa kwanza katika mkumbo mzima. Yeye alikamatwa kwa uuaji, makosa makubwa zaidi kuliko wenzake. Kukamatwa kwa watu hakukusaidia kitu - mgomo uliendelea. Kule shamba, vilio vya wanawake walioachwa pweke vilisikika. ‘Maskini mume wangu ….maskini, bora, bora ungaliwapeleka hao ng’ombe wakapigwa sindano; kufa kwa ng’ombe si kufa kwa nafsi yako,’ alilia bibi mmoja. ‘Ee, kufa kwa wengi arusi ndugu yangu we. Mimi nimelia we, hata macho yamenivimba kwa mume wangu; ati kakataa kupeleka mazao mjini na kuwajibu askari ufidhuli, lakini halafu nimeona haina maana kulia. Bora tufunge vibwebwe na sisi tuwasaidie kucheza ngoma - wafugaji mia wamekamatwa, wakulima mia mbili na hamsini, na bado wanaendelea kukamata, mji umebaki na wanawake tu; lakini watu wenyewe wana vioja, wanapochukuliwa utawaona wanacheka, sisi tulie nini?’ Mjini kulikuwa na vilio vyake. ‘Mwanangu wamemchukua , wanasema watamfunga au watamwua, kafanyaje? Daima kawatumikia , kapoteza nguvu zake juu yao na sasa…’Alimnung’unikia bibi mmoja. ‘Nini bibi we, wachukuzi na makuli watapata haki zao, na wale wanaozurura iko siku wataajiriwa na watakuta mambo mazuri, na wafanyikazi viwandani watachoka kufukuzwa ovyo ; hivyo ndivyo alivyonambia mwanangu alipokuwa akitoka, pingu mikononi. Nililia bibi, uchungu wa mwana unaujua bibi yangu, lakini baadaye nilipofikiri, nikachanganyisha na yale aliyokuwa akaniambia Ali mwanangu, kila siku; niliuhisi uzito wa maneno yake, nikafuta chozi babu.’ Wasaliti walikuwepo, lakini nafasi ya kusaliti haikupatikana. Kwenye lango la bandarini makuli na wachukuzi walisimama imara na marungu na mapanga tayari kuwang’ariba wahaini wowote. Ng’ambo, vikundi vilitawanyika na kufanya kazi; Wengine walitembea mipini mikononi, tayari kumtia adabu yeyote aliyetokwa na imani ya mgomo. Kikundi kingine kiliwekwa sokoni. Hakuna kitu kilichoingia wala kilichotoka. Magari hayakuwa na safari za shamba wala mjini. Askari walitembea ovyo na kumkamata waliyetaka kumkamata, lakini hakukutokea ghasia wala kupigwa mtu. Mgomo uliendelea, ukimuathiri kila mtu, lakini wale waliodai haki zao hawakuvunja kani. ( Dunia Mti Mkavu-Saidi Ahmed Mohamed) MASWALI 1. Toa anwani mwafaka kwa makala haya. (alama 1) ………………………………………………………………… ……………… 2. Thibitisha kuwa asubuhi hiyo ilikuwa mbaya. ( alama 1) …………………………………………………………………… ………… 3. Mauaji ya Makame yalikuwa ya kikatili. Eleza. (alama 4) …………………………………… …………………… 4. ‘Kufa kwa wengi arusi’. Thibitisha ukweli wa methali hii kwa kurejelea taarifa uliyosoma.(alama 4) …………… ………………………………… … 5. Watu walikamatwa kwa nini? (alama 2) ………………………………………………………… 6. Kwa nini wasaliti hawakupata nafasi yao kusaliti ? (alama 2) ………………………………………………… 7. Eleza maana ya (alama 2) i) makuli …………………… ii) Ukimuathiri ………………………… majibu
MAJIBU
0 Comments
Leave a Reply. |
Categories
All
Archives
July 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|