Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
Soma makala yafuatayo kisha ujibu maswali.UFAHAMU Wanasaikolojia wanabainisha kati ya sehemu mbili kuu katika akili ya binadamu; ung’amuzi na ung’amuzibwete. Ung’amuzi ni sehemu ya ubongo ambayo kimsingi hupanua na kudadavua yanayotendeka hususan mchana. Ung’amuzibwete ni kibinimethali chake; hufanya kazi wakati binadamu anapolemazwa na usingizi. Baadhi ya mambo anayoshuhudia binadamu mchana yanaingia kwenye ung’amuzibwete wake na kutokeza katika ndoto zake usiku. Kwa mujibu na mawazo ya Sigmund Freud, mwanasaikolojia wa jadi anayechukuliwa na wengi kama mwasisi wa taaluma ya saikolojia, mambo yanayopatikana katika ang’amuzibwete yana sifa hasi. Freud alidahuli kuwa binadamu huyaficha na kuyabania kwenye ang’amuzibwete mambo ambayo hawezi kuyasema kadamnasi. Alieleza kuwa matamanio yasiyokubalika, makatazo ya jamii, fikra na kauli zilizobaramishwa na miko ya kijamii hubanwa katika ang’amuzibwete. Shehena hiyo ndiyo inayochipuza kwa njia ya ishara za ndoto, mitelezo ya kauli, yaani maneno au kauli zinazotutoka bila wenyewe kukusudia, ishara na lugha ya kitamathalu katika uandishi wa kibunifu na kadhalika. Ung’amuzibwete una uwezo mkubwa wa kuathiri matendo ya bmadamu. Huu ndio msmgi unaowafanya wanasaikolojia wengi, ukiwemo Freud, kusema kuwa tajriba ya mtoto maweza kufichwa kwenye sehemu hiyo na hatimaye kuishia kutokeza katika utu uzima wake. Kwa kuwa tunapoingiliana na binadamu wenzetu kila siku tunayang’amua tuyafanyayo, ung’amuzi unaotuwezesha kutambua jema na ovu unatawala. Ung’amuzibwete unapotawala binadamu wenzetu watashindwa kutuelewa. Hii ndiyo hali anayokuwa nayo mwendawazimu. Ung’amuzibwete wake hutawala. Sisi tunaotawaliwa na ung’amuzi tunashindwa kumwelewa; naye bila shaka anashindwa kutuelewa. Carl Gustav Jung, aliyewahi kuwa mwanafiinzi wa Freud, aliupinga mwelekeo wa Freud na kuungalia ung’amuzibwete kamajaa la mawazo mabaya, matamanio, nia, fikira tuli na dhana ambazo ni hasi. Jung alizuka na dhana mbili muhimu: Ung’amuzibwete wa kibinafsi na ung’a,izibwete jumuishi. Alisema mambo, fikra na uzoefu wowote mbaya unaomuhusu mtu binafsi hupatikana katika ung’amuzibwete wa kibinafsi. Dhana ya ung’amuzibwete jumuishi aliitumia kuelezea sehemu ya akili ya binadamu ambayo inamfanya ayatende matendo fulani kama binadamu wenzake licha ya tofauti zao kiwakati na kijiografia. Kwa mfano, binadamu wengi wana sherehe za kuzaliwa mtoto, kuoa, ibada au mviga unaohusiana na kifo licha ya tofauti zao. Jung alisema kuwa kinachochochea hali hii ni urithi Fulani wa kila mwanadamu. Urithi huo unaopatikana katika ung’ amuzibwete una uwezo wa kuathiri ung’amuzi na matendo ya binadamu ya king’amuzi. Wanasaikolojia wanashikilia kuwa binadamu hawezi kukamilika bila kuzuhusisha sehemu zote mbili kwa sababu zinaathiriana. MASWALI(a) Kwa nini ung’amuzibwete unaelezwa kama kinyume cha ung’amuzi? (alama 2) .……………………………………………………………………………………………… (b) Eleza mtazamo wa Freud kuhusu ung’amuzibwete (alama 3) ……………………………………………………………………………………………….. (c) Kwa mujibu wa Freud yaliyomo kwenye ung’amuzibwete hudhihirika vipi? (alama 4) ……………………………………………………………………………………………….. (d) Eleza tofauti ya mawazo kati ya Sigmund Freud na Carl Gustav Jung. (alama 4) ……………………………………………………………………………………………….. (e) Taja hoja inayowafungamanisha Jung na Freud. (alama 2) .……………………………………………………………………………………………… Majibu
(a) Ung’amuzibwete hufanya kazi mtu akiwa amelala/usiku kinyume na ung’amuzi ambao hufanya kazi mtu akiwa macho/mchana. 1x2 = 2 (b) Mambo yanayopatikana katika ung’amuzi bwete (i) Yana sifa hasi / hubana sifa hasi (ii) Huficha mambo ambayo mwanadamu hawezi kuyasoma wazipeupembele ya kadamnasi (iii) Hubana matamanio yasiyokubalika na jamii (iv) Hubania kauli zilizoharamishwa na miiko ya jamii. 1x3= Hojayoyote mojaAl— 3 (c) (1) Kwa ishara za ndoto (ii) Kwa mitelezo ya kauli (iii) Kwa ishara (iv) Kwa matumizi ya lugha ya kitamathali katika uandishi 4x1= 4 AIa,na-4 (d) Freud anawaza kuwa ung’amuzibwete ni jai la mambo hasi ilhali Jung ana dhana mbili kuhusu ung’amuzibwete (i) Ile ya kibinafsi (ii) Ile ya jumuishi au Freud ana mtazamo wa dhana hasi katika ung’amuzibwete ilhali Jung anawaza dhana ya jumuishi. 2x2=4 Mwanafunzi aonyesha dhana zote mbili ya Freud na ya Jung (e) Ung’amuzibwete una uwezo wa kuathiri ung’amuzi na matendo ya binadamu ya king’amuzi. Al-2
0 Comments
Leave a Reply. |
Categories
All
Archives
July 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|