Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
Maswali na Majibu ya UFAHAMU (Alama15)Soma kifungu kifuatacho kisha ujibu maswali Tokea muundo mpya wa serikali ya ugatuzi uanze kutekelezwa miaka miwili iliyopita, kumeendelea kushuhudiwa matatizo mengi hali iliyopelekea kushuhudiwa kwa msururu wa migomo na maandamano ya raia. Fujo za karibuni kabisa ni zile zinazoshuhudiwa katika miji mikubwa za wachuuzi na wafanyibiashara wakipinga hatua za serikali za kaunti kuwatoza ushuru takribani kwa kila huduma na bidhaa ikiwemo wanyama, kuku na ndege. La kuhuzunisha zaidi katika baadhi ya majimbo imeripotiwa kuwa raia wamelazimishwa kulipa ushuru kwa kutaka tu kuona maiti za jamaa zao kwenye vyumba vya kuhifadhi maiti. Wanasiasa wameonekana kuwa na wakati mgumu kutetea mfumo huu mpya wa ugatuzi huku baadhi wakisema kwamba matatizo yanayoshuhudiwa kwa sasa yametokana na ugeni wa mfumo huo. Wengine wameinyoshea kidole serikali ya kitaifa kwamba ndiyo inayosambaratisha muundo huu. Wengine wanahoji kuwa bado ni mapema na kwamba kunatajika muda mrefu ili kufaulu. Ni wazi kwamba kumekosekana nidhamu bora ya kusimamia maisha ya raia nchini Kenya. Matatizo yanayokumba raia kwa sasa ni dalili kuwa mfumo wa serikali ya ugatuzi umeongezea chumvi kwenye kidonda badala ya kutibu. Swali ni je, hadi lini nidhamu ya kusimamia raia itakuwa ni suala la majaribio na makosa? Hatua ya kuwarundikizia raia ushuru mkubwa ni kitendo cha unyonyaji na cha dhuluma kinachofaa kupingwa. La kufahamishiwa hapa ni kwamba ushuru ndio njia kubwa ya kuzalisha mapato ya serikali zinazojifunga na mfumo wa kimagharibi wa kiuchumi wa kibepari ikiwemo Kenya. Asilimia 90 ya mapato ya serikali za kibepari huegemea ushuru. Kwa hivyo hatua ya serikali za kaunti katika kuwanyonya raia kwa kuwalipisha ushuru si ajabu bali ni thibitisho kuwa jamii ya Kenya inaongozwa na nidhamu ya kiuchumi ya ubepari mfumo wa unyonyaji na ukandamizaji. Ukweli unabakia kuwa ndani ya serikali za kibepari raia ndio hubebeshwa mzigo wa ushuru unaoishia matumboni mwa viongozi! Miito ya mabadiliko ya katiba na ya miundo mipya ya kiutawala si lolote ila ni moja tu ya hatua za mfumo wa kibepari kujipa muda wa kuishi na kuziba aibu zake za kushindwa kusimamia maisha ya watu. Kufeli huku kwa mfumo huu kunashuhudiwa hadi kwenye nchi kubwa za kibepari kama Marekani na Uingereza hivyo nazo zimekumbwa tele na maandamano na fujo za raia wakilalamikia hali ngumu ya maisha. Maswali a) Yape makala haya anwani mwafaka. (alama 1) __________________________________________________________________________ b) Eleza mtazamo wa wanasiasa kuhusu utepetevu wa mfumo huu. (alama 3) __________________________________________________________________________ c) “Ugatuzi nchini Kenya ni mfumo wa kibepari” Thibitisha kauli hii kwa kurejelea makala. (alama 3) __________________________________________________________________________ d) Migomo ni zao la matatizo yaliyogatuliwa kutoka kuu. Toa sababu nyingine zinazosababisha migomo katika serikali za ugatuzi (alama 4) __________________________________________________________________________ e) Thibitisha jinsi mfumo wa ugatuzi umeongeza chumvi kwenye kidonda badala ya kutibu (alama 2) __________________________________________________________________________ f) Eleza maana ya maneno yafuatayo (alama 2) i) Ugatuzi __________________________________________________________________________ ii) Kibepari __________________________________________________________________________ MWONGOZO WA KUSAHIHISHA
MWONGOZO WA KUSAHIHISHA (a) Changamoto za Ugatuzi/Matatatito ya tigatuzi/Ugatuzi ( alama 1x1 = 01) (b) - Ugatuzi ni mfumo geni (Alama 3x1=03) - Serikali kuu kutowajibika - Kudai kuwa mfumo huu unahitaji mda zaidi (c) - Mfumo wa ugatuzi nchini umehusisha matendo ya kibepari kama vile; (alama 3x1=03) - Raia kupewa mzigo wa kulipa ushuru ili kuipa serikali mapato - ushuru ndio njia kubwa ya kuzalisha mapato ya serlkal zinazojifunga na mfumo wa kimagharibi wa kiuchumi - viongozi kuwanyonya raia walio maskini (d) - Hali mbaya ya muundo msingi (alama 4x1= 04) - Viongozi kuendeza ufisadi - Ukosefu wa usawa katika ugavi wa rasilimali - Viongozi kupuuza mchango wa wananchi (e) - Raia kulazimishwa kulipa ili kuona maiti za jamaa zao katika fuo (alama 2x1=02) - Raia kurundikiziwa mzigo wa kulipa ushuru mkubwa - Ushuru unaolipwa na wananchi hauwasaidii wananchi la huishia mifukoni mwa viongozi (f) (i) Ugavi wa mamlaka na raslimali kutoka serikali kuu hadi mashinani (alama 2x1 =02) (ii) mfumo wa kiuchumi wa watu wachache kumiliki raslilmali kwa kuwapora wengine Ondoa nusu alama kwa kila kosa la sarufi hadi makosa sita. Ondoa nusu alama kwa kila kosa la tahajia hadi makosa sita.
0 Comments
Leave a Reply. |
Categories
All
Archives
July 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|