Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
Soma makala haya kisha ujibu maswali yafuatayo HAKI ZA BINADAMU Binadamu wana mazoea ya kufikiria kuwa jinsi wafanyavyo, waongeavyo na wafikiriavyo kuhusu vitu ndivyo inavyopasa kuwa. Kama binandamu tunaamini njia yetu ndiyo sahihi, yenye mantiki na inayopasa kufuatwa na kila mtu. Msingi huu huu unakwenda kinyume na kutambua kila binadamu ana haki ya kufikiri, kusema au kuongea na kutenda mradi asikiuke haki ya mwenzake iliyo sawa na yake. Nguzo mojawapo inayogongomelea hoja hii ni Haki za Binadamu. Azimio kutangaza Haki Bia za Binadamu liliafikiwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa tarehe 10 Desemba 1948. Baraza kuu hilo liliyasisitizia mataifa wanachama umuhimu wa kuyasambaza, kuenezea, na kusisitiza kusambazwa kwa azimio hilo katika shule na taasisi za kielimu. Msingi wa uhuru, haki na amani ulimwenguni ni kutambua binadamu wote wana haki sawa. Ingawa kimsingi jamii na mataifa yote ya ulimwengu yanapaswa kuthamini, kusambaza na kuhimiza umuhimu wa Haki za Binadamu zipo jamii ambazo hukiuka haki hizo. Matokeo ya ukiukaji huu yana athari hasi sana kama ilivyotokea nchini Rwanda na Bosnia. Herzegovina kulikotokea mauaji ya halaiki. Azimio la Haki za Binadamu linajumuisha vipengele kadha ambavyo ni mihimili mikuu ya Azimio lenyewe. Kipengele msingi kabisa kinasisitiza kuwa kila kiumbe anazaliwa huru na ana haki na hadhi sawa na kiumbe mwingine. Ukweli wa kauli hii ulikokotezwa na kauli ya mwanafalsafa maarufu Jean Jacques Rosseau aliyesema kuwa kila kiumbe huzaliwa huru lakini huwa katika pingu ulimwengu mzima. Kauli hii ilitambua ukiukaji huu wa kipengele hiki. Kipengele cha pili kinasisitiza kuwa binadamu wote wana haki za kufurahia uhuru wao pasi na kutengwa au kubezwa kwa misingi yoyote ile si rangi, kabila, jinsia, lugha, dini, asilia, utajiri au chochote kile. Vipengele vingine vinatukumbusha kuwa kila mtu ana haki ya kuishi na kupata ulinzi. Hamna mtu anayepaswa kuishi maisha ya utumwa au unyonge wa kutumikishwa kwa namna yoyote ile. Suala hili linasisitizwa na kipengele cha sita kinachokataza kudhalilishwa kwa watu au kutunzwa kwa namna yoyote ambayo inamfedhehesha kama kiumbe. Azimio la Haki za Binadamu linasisitiza kuwa binadamu yoyote nyule ana haki ya kupata ulinzi wa kisheria. Binadamu huyo hapaswi kubaguliwa na ana haki ya kupata fidia ya kisheria taraa haki zake za kimsingi zikikiukwa. Hata hivyo sio watu wote ulimwenguni ambao wanazifurahia haki hizi za kimsingi. Zipo lukuki za jamii ulimwenguni ambako haki za kimsingi zinakiukwa. Katika nchi ambazo zinaongozwa na watawala wa kiimla, si ajabu kuona haki za binadamu zikikiukwa. Viongozi wa aina hiyo huwa wamegeuzwa ng’ombe wa shemere na tamaa, ubinafsi na ukatili usiojua thamani ya utu. Viongozi wa aina hii wanasahau kuwa kila binadamu ana haki ya kuishi maisha huru, asipotumikishwa wala kulanguliwa kama bidhaa. Nchi za kiimla aghalabu huongozwa na itikadi kuwa kiongozi ndiye pekee ambaye ana uwezo wa kufikiri, kuamua na kutenda. Watu wengine wanapaswa kumfuata kisilka kama yule mbwa wa Pavlov ambaye alitokwa na mate kila kengele ilipopigwa. Viongozi wa ama hii hawachelei kuwatenza nguvu raia zao: Kuwadhalilisha kwa namna nyingi. Viongozi wa aina hiyo huiona sheria ya nchi kama iliyowekwa kwa watu wengine bali sio wao. Msimamo huu unakwenda kinyume na kipengele cha saba cha Haki Bia za Binadamu kisemacho kuwa watu wote ni sawa mbele ya sheria. Baadhi ya haki zinazokiukwa katika jamii za kimabavu ni haki ya watu kuungana, kuwaza, kushiriki katika maamuzi ya serikali, kuwa mwanachama wa jumuia waitakayo, kumiliki mali, kutembea, kuishi anakotaka kutohukumiwa bila ya kuwako na utaratibu wa kisheria. Ni muhimu hata hivyo kujua ni muhimu kwa raia wenyewe kujielimisha na kuzijua haki zao. Serikali inapaswa kuwa mlinzi wa sheria zenyewe. Lakini muhimu kujua pia kuwa mlinzi naye hulindwa pia. Maswalia) Kwa maneno kati ya 90 – 100 fafanua Haki Bia za Binadamu zilizoafikiwa na Baraza kuu la umoja wa Mataifa. (alama 10) Nakala Chafu __________________________________________________________________________ Nakala Safi __________________________________________________________________________ b) Kwa nini viongozi wa kiimla hukiuka haki za binadamu. (Maneno 50 – 60). Nakala Chafu __________________________________________________________________________ Nakala Safi __________________________________________________________________________ Mwongozo
a) Kwa maneno kati ya 90- 100 fafanua Haki Bia za Binadamu Zilizoafikiwa na Baraza kuu la Umoja wa mataifa Kila kiumbe anazaliwa humu na ana haki na hadhi sawa na kiumbe mwingine’ • Binadamu wote wana haki za kufurahia uhuru wao pasi na kutengwa au kubezwa kwa misingi yoyote ile si rangi, kabila, jinsia, lugha, dini, asilia au chochote kile. • Kila mtu ana haki ya kuishi na kupata ulinzi • Hamna mtu anayepaswa kuishi maisha ya utumwa, kutumikishwa, kudhalilishwa au kutunzwa kwa namna inayomfedhehesha kama kiumbe. • Haki ya kupata ulinzi wa kisheria • Kutobaguliwa na ana haki ya kupata fidia ya kisheria taraa haki zake za kimsingi zikikiukwa . Alama 8 utiririko alama 2) b) Kwa nini viongozi wa kiimla hukiuka haki za binadamu • Tamaa ya uongozi • Ubinafsi • Ukatili, hawajui thamani ya utu • Kiburi cha kujiona kuwa wao ndio wanaofahamu mambo zaidi • Husahau kuwa binadamu ana haki ya kuishi maisha huru bila kutumikishwa au kutanguliwa kama bidhaa • Hudhani wao tu ndio wana uwezo wa kufikiri, kuamua na kutenda na wananchi wanapaswa kufuata tu • Huona kuwa sheria ya nchi imewekewa wengine na wala sio wao hivyo huwatenza nguvu raia zao Alama 4, utiririko alama 1)
0 Comments
Leave a Reply. |
Categories
All
Archives
June 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|