Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
​FASIHI SIMULIZI - soma utungoufuataokishaujibumaswali model14122022001
​Hapo zamani za kale paliishi mtoto katika kisima kimoja. Siku moja mtoto huyu aliokota kijiwe karibu na soko kuu. Kijiwe kilikuwa kikimeremeta kwa rangi mbalimbali na kilizingirwa na pete ya dhahabu. Mtoto huyu na wenzake walianza kurushiana kijiwe hicho. Baada ya muda kilianza kuongezeka umbo na kuonekana kama kiwiliwili cha binadamu. Kikaanza kuwakimbiza wale watoto. Kutokana na ukulele wao watu walikuja kutazama nini kilikuwa cha mno. Walipofika walikutana ana kwa ana na dubwana hilo. Lilizidi kuongezeka umbo na likawameza wote pamoja na mifugo wao. Wachache waliojaribu kukimbia liliwashika kwa mikono yake mipana na mirefu. Kwa bahati njema alikuwepo mama mmoja aliyeona haya yote. Alikuwa mbali na hapo. Aliteremka kutoka kilele cha mlima na kuwapata wakuli mamakondeni na sawia akawajuza kuhusu kitendo kilichomwogofya sana. Wote wakaacha shughuli zao na wakatwaa silaha zao wakaelekea soko kuu.
​Dude sasa lilikuwa limejilaza baada ya shibe, wakulima wale walichagua watu sita ambao walijulikana kwa ushujaa wao. Pamoja walilinyemelea lile nyangarika na kulikata mara moja. Lilitoa mkoromo mkuu kabla halijakata kamba. Punde, wanakijiji kwa uangalifu mkubwa walitoboa tumbo lake wakitarajia kupata maiti za wapenzi wao pamoja na mifugo wao. Wote walijawa na furaha kuu walipoona wapenzi wao wakijichomoza kutoka tumboni, mmoja baada ya mwingine hadi akatoka Yule wa mwisho. Mbuzi, kondoo na ng’ombe wote walitoka mmoja mmoja.
Siku hiyo kuliandaliwa sherehe ya kumshukuru Muumba kwa wema wake. Watoto walishauriwa wasithubutu kuchezea vitu wasivyovijua. ​MASWALI.
a) Ainisha kipera hiki cha fasihi simulizi. (alama.1)
b) Fafanua mambo matatu yanayodhihirisha kuwa kipera hiki ni sanaa. (alama.3) c) Mwasilishaji wa kipera hiki anafaa kuwa na sifa gani? Eleza. (alama.4) d) Onyesha mifano miwili ya fantasia katika hadithi hii. (alama.2) e) Eleza majukumu matatu ya tungo hizi kwa wanajamii. (alama.3) f) Eleza majukumu manne ya mtindo uliotumiwa kuanzisha hadithi hii. (alama.4) g) Fafanua aina tatu za taswira zinazojitokeza katika utungo huu. (alama.3) ​MWONGOZO WA FASIHI SIMULIZI
a) Nganoyamazimwi – kunamatumizimengiya fantasia. Kijiwekuongezeka umbo. (1x1=1)
b)i Kina umbo maalum, kwamfano kina mwanzo. Hapozamaniza kale…. ii) Mandahri/mazingirayamesawiriwakwaufundimkubwa. iii) Wahusikawamejengwakwaufundimkubwailikusawiritabiazawahusikakatikajamii. iv) Lughaimetumikakwaufundi. Kwamfanolughayakitamathali. Kuna tashhisi,Uhuishi, takririn.k (3x3=3) c)i) Awe mbunifuiliabunihadithiupya ii) Ajuehadhirayakenamahitajiyakepamojanakiwango cha elimu. iii) Kuilewanakumudulughayahadhirayake. iv) Kuwajasiriiliasimamembeleyahadhirayake. v) Kuwamcheshiilihadhiraichangamke. vi) Kuwanauwezowakushirikishahadhirayakekwanjiambalimbali. viii) Awe naujuzinaufasahawalughailikuwasilishamawazokwanjiamwafaka. (4x4=4)
d)i) Zimwikuwezakumezaumatiwawatupamojanamifugo.
ii) Watunamifugokutokatumbonimwazimwiwakiwahai. iii) Kijiwekuongezeka umbo nakuonekanakamakiwiliwili cha binadamu. (2x1=2) e)i) Kukashifutabiayauovu, ulafinaukatili ii) Kutahadharishadhidiyakuwanaulafi, ukatilin.k. iii) Kutiamoyowaliodhulumiwakuwawaliowanyanyasawataadhibiwasikumoja. (3x1=2) f)i) Kuvutamakiniyahadhira. ii) Kumtambulishamtambajikwahadhira iii) Kuashiriamwanzowahadithi. iv) Kutoahadhirakutokaulimwenguhalisihadiulewahadithi v) Kushirikishahadhiranamtambaji. (4x1=4) g) Taswiramwendo ✔ kikaanzakuwakimbiza wale watoto. ✔ aliteremkakutokakilele cha mlima. ✔ wakaelekeasokokuu. Taswirahisi ✔ Kitendokilichomwogofyasana. ✔ Lilitoamkoromomkuu ✔ wotewalijawanafurahakuu. Taswiramguso ✔ Na kulikatamaramoja ✔ …uangalifumkubwawalitoboatumbo. (3x1=3
0 Comments
Leave a Reply. |
Categories
All
Archives
June 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|