Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
ISIMU JAMII (Alama10)a) Eleza maana ya istilahi zifuatazo i) Lafudhi (alama 1) __________________________________________________________________________ ii) Pijini (alama 1) __________________________________________________________________________ iii) Lahaja (alama 1) __________________________________________________________________________ b) Eleza njia tatu za kupunguza tofauti za kilahaja (alama 3) __________________________________________________________________________ c) Fafanua sababu zozote zinazosababisha makosa katika matumizi ya lugha ya Kiswahili (alama 4) Mwongozo
a) i) Lafudhi – ni upekee unaojitokeza baina ya watumiaji mbalimbali wa lugha moja. ii) Pijini – ni lugha inayoibuka panapotokea mwingiliano wa watu wanaozungumza lugha tofauti kwa lengo la kurahisisha mawasiliano. iii) Lahaja ni tofauti katika matamshi, maumbo na matumizi ya maneno zitokanazo na tofauti katika maeneo mbalimbali kwa lugha yenye asili moja. b) i) Kusanifisha lugha ii) Kuimarisha njia za usafiri baina ya maeneo ambapo lugha inatumiwa km barabara iii) Kuwepo kwa mfumo mmoja wa elimu ambapo lugha moja inatumiwa iv) Maendeleo ya njia za kupashana habari km simu magazeti, redio n.k v) Kuweka utawala mmoja k.v. muungano wa Afrika Mashariki. c) Lugha ya kwanza Hali – uchovu / ugonjwa wa mzungumzaji Uwili lugha / uwingi lugha Kwa kukusudia km. waigizaji. Kutozingatia ngeli Kutoelewa lugha/msamiati Kutozingatia upatanisho wa ngeli Kutozingatia tahajia/hijai/maendelezo
0 Comments
Leave a Reply. |
Categories
All
Archives
June 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|