Maswali na Majibu KCSE Kiswahili
Ufahamu | Ufupisho | Isimu Jamii | Insha | Utumizi wa Lugha
Insha
Mwongozo huu unatumika sambamba na mwongozo wa kudumu wa Insha [102/1]
1. Andika hotuba ya Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kupambana na Ufisadi nchini kwa washika dau wote katika Kaunti ya Kakamega. -Insha ihusishe hoja zisizopungua sita kati ya hizi na nyingine zinazorejelea maswala yoyote ya ufisadi nchini: --Chanzo cha ufisadi k.m. umaskini, tamaa, kuiga wengine, kutaka kuhepa adhabu, n.k. --Kunakotokea ufisadi, k.m. ofisini, hospitali, shuleni, mahakamani, katika vyombo vya usafiri, n.k. --Athari za ufisadi k.m. ufujaji wa pesa, nchi/mashirika kutoendelea, n.k. --Adhabu kwa ufisadi k.m. kushikwa, kufungwa, kufutwa, kulazimishwa kulipia, n.k. --Hatua zinazochukuliwa na shirika lake kupambana na ufisadi. --Mapendekezo yake kwa umma kuhusu jinsi ya kupambana na ufisadi. SURA Ionyeshe kuwa ni hotuba kutokana na kianzio, kinachotambua au kuiamkua haadhira. Pia kiishio. Insha yenyewe iandikwe kwa mtiririko ikitumia nafsi ya kwanza. Adhabu ya kawaida ichukuliwe kwa insha isiyochukua sura inayostahili (-04s) 2. Eleza chanzo cha ongezeko la bei ya bidhaa nchini mwako, huku ukionyesha athari za ongezeko hili. CHANZO --Ufisadi --Tamaa --Shilingi ya Kenya kukosa nguvu dhidi ya Dola ya Marekani.
ATHARI
3. Aiszfuye mvua imemnyea. Ni methali. Insha iwe na kisa (au visa) kinachoonyesha ukweli wa methali. Methali ina maana kuwa anayelizungumzia jambo, kulieleza au kulisifu ana tajriba nab. Insha ionyeshe sifa itolewayo na pia alivyonyewa. 4. “Karne ya 21 imeleta ongezeko kubwa la vyombo tofauti vya habari nchini, pamoja na athari anuwai” Jadili kauli hii. ONGEZEKO Insha ithihirishe ukweli kwamba vyombo vya habari vimeongezeka kwa kutoa mifano ya magazeti, majarida, stesheni za redio, runinga, n.k. atakayejaribu kuipinga kauli hii atakuwa amepotoka. ATHARI Ni nzuri na mbaya • Habari zinapatikana kwa urahisi. • Hakuna usiri usiofaa wa serikali tena. • Kuna burudani tele. • Vinaelimisha. • Watu (hususan wale mashuhuri) wamekoseshwa siri katika maisha yao. • Vyombo vingine vinachochea makabila, n.k. • Kuna ongezeko la picha/habari za ngono. • Maadili yamezorota. • N.K. Insha ihusishe hoja zozote sita au zaidi katiya hizi na nyingine. ZIADA YA JUMLA Tumia mwongozo wa kudumu wa insha ili kutuza insha katika viwango kati ya A+ na D-. hoja katika maswali 1,3 na 4 itambulike kwa mkwaju (‘f) kushoto, pembezoni mwa aya iliyobeba hoja.
0 Comments
Leave a Reply. |
Categories
All
Archives
June 2024
|
We Would Love to Have You Visit Soon! |
Hours24 HR Service
|
Telephone0728 450425
|
|
8-4-4 materialsLevels
Subjects
|
cbc materialsE.C.D.E
Lower Primary
Upper Primary
Lower Secondary
Upper Secondary
|
teacher support
Other Blogs
|